Luku haipatikani na TANESCO hamtoi taarifa kwa Wateja kuhusu matengenezo mnayoyafanya na juhudi zenu kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili zimefika wapi. Kuweni wastaarabu.
 
Luku haipatikani na TANESCO hamtoi taarifa kwa Wateja kuhusu matengenezo mnayoyafanya na juhudi zenu kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili zimefika wapi. Kuweni wataarifu.
Naam ni kweli, hata mimi nimepata tatizo hili kwa siku tatu au nne sasa. LUKU inasumbua
 
Tanesco naomba kuuliza. Hivi Mgao wa umeme Mkoa wa Songwe, Utaisha lini?? maana ni muda mrefu sasa. naomba majibu tafadhali maàna hata sasa hivi hakuna umeme
 
Huduma ya luku imesharejea na wateja wanafurahia umeme wa Tanesco
Hello! Nimenunua luku kwa T-shirt. 15,000/= leo asubuhi kwa m-pesa, mita namba 37135433441. Pesa ishakatwa lakini umeme sijapata hadi sasa, tatizo nini? Pia naombeni mshughulikie nahitaji umeme muda huu.
 
Na katika sehemu gani umeme wa Luku unapatikana kwenye Mpesa, Tigo pesa au mobile bank
 
Hakika Shirika hili linahitaji Uongozi mpya kwani utendaji Wa viongozi waliopo umekuwa Wa mazoea.Suala la Luku ni suala nyeti sana nilitegemea lingeshughulikiwa Kwa umakini na uharaka Mkubwa.

Lakini uongozi Wa Tanesco ulitangaza kuwa suala hilo lingeshughulikiwa kutoka saa 4 usiku mpaka saa7 usiku lakini mpaka sasa ni saa 5 hakuna Huduma.

Tanesco hebu TUONEENI HURUMA wanyonge.
 
Na katika sehemu gani umeme wa Luku unapatikana kwenye Mpesa, Tigo pesa au mobile bank
Waongo hawa hakijarudi kitu, MPESA,TIGO zimefeli, nimeenda kwa wakala hakuna kitu, DTB inafeli.

Wamehamisha mitambo yao ila system zilizounga kwao bado zimeelekezwa kule kwa zamani hii kitu hadi watu waingie kazini monday or later.
 
Back
Top Bottom