onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,346
- 1,303
Ndugu wanajamvi mbona Kama siwaelewi vizuri Tanesco. 29 Aug nilinunua Luku wakakata hela ya tozo sh 2000 ambayo katika maelezo Yao inasema Ni kwa ajili ya mwezi wa July sh 1000 na August sh 1000. Na baada ya Hapo wanasema watakuwa wanakata sh 1000 kila mwezi kwa sisi wenye nyumba za kawaida.
Juzi tarh 17 mwezi huu nilinunua Tena umeme wakakata tozo Yao sh 1000 na kukaa na message Hadi leo 21 Sep ndio message inakuja.
Jamani labda Ni uelewa wangu tu, nadhani ukinunua leo na wao kukata tozo Yao nadhani hapa katikati hawakati Hadi mwezi uishe.
Sasa Kama kila ukinunua luku unakatwa tozo mbona wenye kununua za hela ndogo kuanzia 2000, 3000 Hadi 10000 wataumia Kama unit zikiisha kabla ya kipindi cha mwezi kuisha. Hapa tutajikuta unachangia Kati ya sh 5000 kila mwezi Kama tatizo hili halitaondolewa.
Wamelazimisha pawepo tozo, wananchi wamekaa kimya hakuna alieandamana kupinga lakini Sasa wawe wawazi kusema kuwa tozo Ni muda wowote unaponunua luku.
Hapa tunaoweka umeme wa vibaba tutaumia Jamani. Mamlaka zijitokeze warekebishe na waseme Ni kwa Nini hii Hali ijitokeze.