TANESCO siwaelewi kuhusu makato ya kodi ya majengo

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,132
2,000
Ndugu wanajamvi mbona Kama siwaelewi vizuri Tanesco. 29 Aug nilinunua Luku wakakata hela ya tozo sh 2000 ambayo katika maelezo Yao inasema Ni kwa ajili ya mwezi wa July sh 1000 na August sh 1000. Na baada ya Hapo wanasema watakuwa wanakata sh 1000 kila mwezi kwa sisi wenye nyumba za kawaida.

Juzi tarh 17 mwezi huu nilinunua Tena umeme wakakata tozo Yao sh 1000 na kukaa na message Hadi leo 21 Sep ndio message inakuja.

Jamani labda Ni uelewa wangu tu, nadhani ukinunua leo na wao kukata tozo Yao nadhani hapa katikati hawakati Hadi mwezi uishe.

Sasa Kama kila ukinunua luku unakatwa tozo mbona wenye kununua za hela ndogo kuanzia 2000, 3000 Hadi 10000 wataumia Kama unit zikiisha kabla ya kipindi cha mwezi kuisha. Hapa tutajikuta unachangia Kati ya sh 5000 kila mwezi Kama tatizo hili halitaondolewa.

Wamelazimisha pawepo tozo, wananchi wamekaa kimya hakuna alieandamana kupinga lakini Sasa wawe wawazi kusema kuwa tozo Ni muda wowote unaponunua luku.

Hapa tunaoweka umeme wa vibaba tutaumia Jamani. Mamlaka zijitokeze warekebishe na waseme Ni kwa Nini hii Hali ijitokeze.
 
kwamsangaze

Member
May 27, 2020
12
45
Tozo ya kodi ya majengo ni sh. 1,000 kwa mwezi. Ukinunua umeme kwa mara kwanza katika mwezi, kwa mfano tarehe tano mwezi Septemba 2021 utakatwa sh. 1,000 na ukijakununua tena umeme katika mwezi huo huo wa Septemba hutakatwa tena sh. 1,000 hadi mwezi wa Oktoba utakaponunua umeme ndipo utakatwa kodi ya mwezi huo.
 
ngendabanka

Member
Aug 5, 2020
29
45
Makato yalianza tangu July,hivyo kama ulinunua umeme mwezi Aug ,makato yake ni she 2000/=,i.e for July and August. Kwa miezi iliyobaki utakuwa unakatwa shs 1000/=hadi utakapotimiza jumla ya shs 12000/=ambazo kodi halisi ya majengo.
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,434
2,000
Ndugu wanajamvi mbona Kama siwaelewi vizuri Tanesco. 29 Aug nilinunua Luku wakakata hela ya tozo sh 2000 ambayo katika maelezo Yao inasema Ni kwa ajili ya mwezi wa July sh 1000 na August sh 1000. Na baada ya Hapo wanasema watakuwa wanakata sh 1000 kila mwezi kwa sisi wenye nyumba za kawaida.

Juzi tarh 17 mwezi huu nilinunua Tena umeme wakakata tozo Yao sh 1000 na kukaa na message Hadi leo 21 Sep ndio message inakuja.

Jamani labda Ni uelewa wangu tu, nadhani ukinunua leo na wao kukata tozo Yao nadhani hapa katikati hawakati Hadi mwezi uishe.

Sasa Kama kila ukinunua luku unakatwa tozo mbona wenye kununua za hela ndogo kuanzia 2000, 3000 Hadi 10000 wataumia Kama unit zikiisha kabla ya kipindi cha mwezi kuisha. Hapa tutajikuta unachangia Kati ya sh 5000 kila mwezi Kama tatizo hili halitaondolewa.

Wamelazimisha pawepo tozo, wananchi wamekaa kimya hakuna alieandamana kupinga lakini Sasa wawe wawazi kusema kuwa tozo Ni muda wowote unaponunua luku.

Hapa tunaoweka umeme wa vibaba tutaumia Jamani. Mamlaka zijitokeze warekebishe na waseme Ni kwa Nini hii Hali ijitokeze.
Ni sahihi, Siku yoyote ya Kwanza kununua umeme katika mwezi watakata tu.

Mfano Mwezi August ulinunua umeme mwingi ambao ulikaa mpaka september 30 ukaisha. Hapo ukinunua umeme hiyo September 30 utakatwa, na huo umeme tuseme ukikaa siku tatu tu ukaisha October 2 labda ukanunua utakatwa Tena bila kujali umekatwa siku 2 zilizopita.
 
TANESCO

JF-Expert Member
Jul 12, 2014
3,586
2,000
Ndugu wanajamvi mbona Kama siwaelewi vizuri Tanesco. 29 Aug nilinunua Luku wakakata hela ya tozo sh 2000 ambayo katika maelezo Yao inasema Ni kwa ajili ya mwezi wa July sh 1000 na August sh 1000. Na baada ya Hapo wanasema watakuwa wanakata sh 1000 kila mwezi kwa sisi wenye nyumba za kawaida.

Juzi tarh 17 mwezi huu nilinunua Tena umeme wakakata tozo Yao sh 1000 na kukaa na message Hadi leo 21 Sep ndio message inakuja.

Jamani labda Ni uelewa wangu tu, nadhani ukinunua leo na wao kukata tozo Yao nadhani hapa katikati hawakati Hadi mwezi uishe.

Sasa Kama kila ukinunua luku unakatwa tozo mbona wenye kununua za hela ndogo kuanzia 2000, 3000 Hadi 10000 wataumia Kama unit zikiisha kabla ya kipindi cha mwezi kuisha. Hapa tutajikuta unachangia Kati ya sh 5000 kila mwezi Kama tatizo hili halitaondolewa.

Wamelazimisha pawepo tozo, wananchi wamekaa kimya hakuna alieandamana kupinga lakini Sasa wawe wawazi kusema kuwa tozo Ni muda wowote unaponunua luku.

Hapa tunaoweka umeme wa vibaba tutaumia Jamani. Mamlaka zijitokeze warekebishe na waseme Ni kwa Nini hii Hali ijitokeze.
Ndugu mpendwa Mteja wetu!

Kama ambavyo Serikali ilivyotangaza kuwa kodi ya majengo italipwa kupitia manunuzi ya umeme hivyo basi zoezi lilianza Mwezi wa nane 2021 ambapo wateja walikatwa makato ya mwezi wa Saba (Tsh 1000) na wa nane ( Tsh 1000) jumla Tsh 2000 kwa miezi miwili.

Kwa wateja ambao hawajakatwa kodi husika Mwezi wa Saba na wa Nane watapaswa kulipia kiasi cha Tsh 3000 ili kulipia kodi ya majengo ya mwezi wa Saba, Nane na Tisa 2021.

Wateja ambao hawajakatwa miezi hiyo wanashauriwa kununua umeme wa zaidi ya shilingi 3000 ili waweze kupata token

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

Makao Makuu
 
kifaruu

Senior Member
Aug 15, 2015
106
225

Hili suala la TRA mkuu Tanesco ni Gate tuu ya kupitia mkuu
 
Lubengera

Senior Member
Jun 21, 2019
183
250
Ndugu mpendwa Mteja wetu!

Kama ambavyo Serikali ilivyotangaza kuwa kodi ya majengo italipwa kupitia manunuzi ya umeme hivyo basi zoezi lilianza Mwezi wa nane 2021 ambapo wateja walikatwa makato ya mwezi wa Saba (Tsh 1000) na wa nane ( Tsh 1000) jumla Tsh 2000 kwa miezi miwili.

Kwa wateja ambao hawajakatwa kodi husika Mwezi wa Saba na wa Nane watapaswa kulipia kiasi cha Tsh 3000 ili kulipia kodi ya majengo ya mwezi wa Saba, Nane na Tisa 2021.

Wateja ambao hawajakatwa miezi hiyo wanashauriwa kununua umeme wa zaidi ya shilingi 3000 ili waweze kupata token

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

Makao Makuu
TANESCO.
Nafahamu mwanzo ni mgumu,lakini katika hili kuna sehemu haiko sawa na inahitaji marekebisho!

Kumtunzia mtu deni, wakati alikuwa na umeme sio haki hata kidogo! ukweli mchungu, tunaenda mbele hatua tatu, then tunarudi nyuma hatua 3x3.

Wataalamu kaeni muendelee kuboresha jambo hili, kimsingi haliko sawa, na mbaya zaidi linafifiza juhudi zenu wenyewe za upatikanaji wa umeme kwa ajili ya maendeleo na maisha bora.

Mtu akisikia tozo hizi, ata hamu ya kuwa na umeme kutoka kwenu anakosa, anabaki kupambania Solar.
 
Chikuvi2021

Senior Member
Aug 3, 2021
137
250
TANESCO
Kwa kuwa Kodi ya majengo inakusanywa kupitia Luku,
(1)Kama ikiwapendeza ongezeni nguzo na mita ili wateja wengi ambao wameomba huduma ya umeme Kanda ya Chanika,wapatiwe umem
(2)Hii itaongeza wigo wa walipa Kodi ya majengo(mapato mengi yanapotea).
(3).Kwa mfano kuna wateja wengi wa mitaa ya Taliani, Nyeburu,Zavala,kinyamwezi,Mbondole nk, waliomba umeme tangu mwaka May 2000 wilayani kisarawe na baadae May 2021 kuhamishiwa kituo kipya Cha Chanika,lakini mpaka hivi leo bado kupewa huduma hiyo-( ndiyo kwanza) -mwezi wa nane wamefanyiwa upimaji(survey) mtaa wa Taliani,
(4).Ukifuatilia TANESCO Chanika unaambiwa hakuna nguzo au mita.
(5).Kuna Waombaji zaidi ya 25 wanataka umeme eneo la Taliani ( na zinatakiwa Nguzo tano, kuwafikia wote),lakini TANESCO Chanika wanasema hakuna nguzo,lakini hawa watu wanaikosesha Serikali Kodi ya Majengo na TANESCO maduhuli yake.
(6). Ushauri kwa Tanesco Makao Makuu au Kanda ya Mashariki na Pwani waliangalie suala hili,na ikiwapendeza kulipatia ufumbuzi, (nyumba nyingi ambazo hazijapatiwa umeme Dar es Salaam na miji mingine , hawalipi kodi ya majengo).
Na kazi iendelee.
 
TANESCO

JF-Expert Member
Jul 12, 2014
3,586
2,000
TANESCO
Kwa kuwa Kodi ya majengo inakusanywa kupitia Luku,
(1)Kama ikiwapendeza ongezeni nguzo na mita ili wateja wengi ambao wameomba huduma ya umeme Kanda ya Chanika,wapatiwe umeme ili kuongeza wigo wa walipa Kodi ya majengo(mapato mengi yanapotea).
(2).Kuna wateja (wengi wa mtaa wa Taliani, Nyeburu,Zavala,kinyamwezi,Mbondole nk,) waliomba umeme tangu mwaka May 2000 wilayani kisarawe na baadae May 2021 kuhamishiwa kituo kipya Cha Chanika,lakini mpaka hivi leo bado kupewa huduma hiyo-( ndiyo kwanza) -mwezi wa nane wamefanyiwa upimaji(survey) mtaa wa Taliani,
(3).Ukifuatilia TANESCO Chanika unaambiwa hakuna nguzo au mita
(5). kwa mfano Kuna Waombaji zaidi ya 25 wanataka umeme eneo la Taliani lakini zinatakiwa Nguzo tano, kuwafikia wote,lakini wanasema hakuna nguzo,lakini Hawa Watu wanaikosesha serikali Kodi ya Majengo na TANESCO mapato.
(6). Ushauri kwa Tanesco makao Makuu au Kanda ya Mashariki na Pwani waliangalie suala hili,na kulipatia ufumbuzi, nyumba nyingi ambazo hazijapatiwa umeme Dar es Salaam na miji mingine , watakuwa hawalipi kodi ya majengo.Na kazi iendelee.
Tumepokea ushauri tunatambua umuhimu wa umeme kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya Nchi yetu ndio maana tumeendelea kuongeza kazi ya kufungia wateja umeme, wateja ambao hawajafikiwa na huduma tunawaomba wawe wamuvulivu kwa kuwa shirika linaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ambayo italeta tija
 
Goodguy

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
352
1,000
Sijaona tatizo hapo, wewe ulinunua umeme August ukakatwa kodi ya mwezi wa 7 na 8, uliponunua mwezi wa tisa haijarishi ni tarehe ngapi na umenunua umeme unaoweza kutumia miezi mingapi ukakatwa Kodi ya mwezi wa tisa, mwezi wa kumi pia utakapolipa utakatwa kodi.

Ushauri wangu,
Kwakuwa unapaswa kulipa kodi kila mwezi na haiwezekani kuilipa kodi yote ya mwaka kwa pamoja kwanjia ya luku basi bila kujali umenunua umeme unaoweza kuutumia kwa muda mrefu basi kila mwezi uwe unalipa iyo 1000 kwajili ya kodi huku ukiendelea kutumia umeme mwingi ulioununua kwajili labda ya matumizi ya miezi miwili
 
Nipo huru

JF-Expert Member
Jul 20, 2021
924
1,000
Ndugu mpendwa Mteja wetu!

Kama ambavyo Serikali ilivyotangaza kuwa kodi ya majengo italipwa kupitia manunuzi ya umeme hivyo basi zoezi lilianza Mwezi wa nane 2021 ambapo wateja walikatwa makato ya mwezi wa Saba (Tsh 1000) na wa nane ( Tsh 1000) jumla Tsh 2000 kwa miezi miwili.

Kwa wateja ambao hawajakatwa kodi husika Mwezi wa Saba na wa Nane watapaswa kulipia kiasi cha Tsh 3000 ili kulipia kodi ya majengo ya mwezi wa Saba, Nane na Tisa 2021.

Wateja ambao hawajakatwa miezi hiyo wanashauriwa kununua umeme wa zaidi ya shilingi 3000 ili waweze kupata token

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

Makao Makuu
Mnapoteza muda kujibu wapumbavu kama hao ambao lengo ni kuchafua serikali iliyopo kwa hoja za kipumbavu, mwenyewe amesema amekatwa 2000 mwezi August kwa malipo ya july na august baadaye mwezi septemba amekatwa 1000 ya mwezi septemba sasa sijui analalamika nini kama upumbavu tu.
 
Nipo huru

JF-Expert Member
Jul 20, 2021
924
1,000
TANESCO.
Nafahamu mwanzo ni mgumu,lakini katika hili kuna sehemu haiko sawa na inahitaji marekebisho!

Kumtunzia mtu deni, wakati alikuwa na umeme sio haki hata kidogo! ukweli mchungu, tunaenda mbele hatua tatu, then tunarudi nyuma hatua 3x3.

Wataalamu kaeni muendelee kuboresha jambo hili, kimsingi haliko sawa, na mbaya zaidi linafifiza juhudi zenu wenyewe za upatikanaji wa umeme kwa ajili ya maendeleo na maisha bora.

Mtu akisikia tozo hizi, ata hamu ya kuwa na umeme kutoka kwenu anakosa, anabaki kupambania Solar.
Hiyo siyo tozo bali ni kodi ya jengo ambayo inakusanywa na TRA wao TANESCO wanatumika kama wakala tu na kodi hiyo hata kama hutumii umeme wa TANESCO utailipa tu kwa sababu kodi hiyo miaka yote ipo isipokuwa hivi sasa imetumika mbinu ya kuipata kwa uhakika zaidi kutoka kwa wengi na watabaki wachache tu ambao hawatumii umeme ndio wataendelea kufuatiliwa kupitia serikali za mitaa kama ilivyokuwa zamani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom