Tanesco/serikali yalipa mawakili 25bn/- kwa kazi isiyokuwa na tija! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco/serikali yalipa mawakili 25bn/- kwa kazi isiyokuwa na tija!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Mar 16, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wadau: Habari hii inasikitisha sana -- kuona jinsi serikali/Tanesco ilivyoridhia malipo ya mabilioni kwa mawakili kwa kazi isiyokuwa na tija. Wakiambiwa kwamba huko ni kuzidi kudidimiza hali za wananchi wanakuja juu na kusema wanataka kuleta machafuko. Angalieni hasa pale penye red.  Mikataba ya Mwinyi, kikwete kufilisi nchi

  Viongozi waliongiza serikali katika mikata mikubwa mitatu ya utata, wameliandalia taifa mzigo mkubwa wa madeni yasiyolipika hata katika miaka 50 ijayo, MwanaHalisi limeelezwa.

  Wakati Dowans wanadai Sh 94 bilioni, IPTL wanadai zaidi ya Sh 248.6 bilioni kwa serikali/Tanesco kuvuruga mkataba wake.

  Mikataba yenye utata na inayotishia kuliangamiza taifa ni ile ya kuzalisha ya makampuni ya IPTL, Richmond na Dowans iliyosainiwa wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi na Rais Jakaya Kikwete.

  Pamoja na makampuni hayo kuikaba koo serikali na kuifikisha katika mahakama na tume mbali mbali za kimataifa za usuluhishi, gharaqma za serikali kujitetea zinaendelea kuongezeka.

  Katika kipindi cha miaka mitano tu iliyopita, serikali imetumia zaidi ya Sh 23 bilioni kujitetea, kwa kulipa makampuni ya uwakili. Gharama hizi zinaongezeka mwaka hadi mwaka kufuatia kesi kuchukua muda mrefu na hata kufumuka kwa kesi mpya.

  Sehemu ya mabilionim hayo ya shilingi imelipwa kwa makampuni ya wanasheria ya Mkono and Company Advocates ya Tanzania na Hunton and William ya Marekani kwa kutetea Tanesco iliyoshitakiwa na kampuni ya IPTL.

  Mabilioni mengine yamelipwa kwa makampuni ya mawakili ya Rex Attorney ya Tanzania na Reed Smith ya Uingereza kwa kuitetea Tanesco katika kesi iliyofunguliwa na kamopuni ya Richmond Dev. Co. LLC.

  Rex Attorneys na Reed Smith wamelipwa au watalipwa pia mabilioni ya shilingi kwa kutetea Tanesco katika shauri lililofunguliwa na makampouni ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Limited (DTL) katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa kibiashara (ICC).

  Nyaraka zinaonyesha kuwa tayari Mkono and Company Advocates wamelipwa na Tanesco kiasi cha Dola 11,818,542.89 (sawa na karibu sh 17 bilioni).

  Kampuni ya Mkono and Company Advocates inamilikiwa na mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono.

  Aidha, kampuni ya Mkono imelipwa pia kiasi cha Sh 8.5 bilioni kwa kusimamia shauri lililofunguliwa na benki ya Standard Chartered Bank ya Hong Kong dhidi ya serikali katika shauri la kukatisha mktaba wa IPTL. Serikali na IPTL waliingia mkataba mwaka 1994.

  Nyaraka zinaonyesha kuwa Rex Attorneys na mwenzake walilipwa kiasi cha Dola 3,574,351.51 (karibu sh 5.2 bilioni katika shauri lililofunguliwa na makampuni ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania limited (DTL) katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa kibiashara (ICC).

  Mawakili hao pia wamelipwa dola 860,056.71 (karibu sh 1.2 bilioni) kwa kazi ya kutetea Tanesco dhidi ya kesi iliyofunguliwa na kampuni ya Richmond Dev. Co. LLC na kusikilizwa katika Falme za Kiarabu (UAE).

  Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja mwezi mmoja baada ya mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba kuibua kile kilichodaiwa “taarifa juu ya upatikanaji wa umeme nchini” ambapo tarehe 3 februari 2011 alitaka waziri wa nishati na madini, William Ngeleja kueleza hatua zinazochukuliwa na Tanesco katika kukabiliana na mgao wa umeme na mzigo wa kesi unaolikabili.

  Katika barua hiyo, Makamba anasema “Katika viambatanisho vya hukumu ya ICC kama ilivyosajiliwa mahakama kuu ya Tanzania zipo nyaraka zinazoonyesha kwamba mwanasheria aliyeishauri Tanesco kuvunja mkataba na Dowans – kwa kusema kwamba siyo mkataba halali na kwamba hakuna madhara ya kisheria kuuvunja – ndiye huyohuyo pia aliyeshauri benki ya Stanbic kutoa mkopo wa dola zaidi ya 120 milioni kwa Dowans – kwa kusema kwamba ni kampuni halali, inayokopesheka na ina mkataba halali na Tanesco.”

  Anasema, “Ni mwanasheria huyohuyo aliyewakilisha Tanesco kwenye kesi iliyofunguliwa na Dowans, kewsi ambayo ilitokana na ushauri wake, na baada ya hukumu ndiye huyohuyo, kwa mujibu wa maelezo yako mheshimiwa waziri ya tarehe 6 Januari 2011, aliyetoa ushauri kwamba hakuna njia nyingine zaidi ya kuilipa Dowans.”

  Makamba alitaka serikali kueleza suala hilo kwa ufasaha ili kuondoa kile alichoita “picha inayoweza kuonyesha serikali ilikosa umakini kwenye jambo hili zima na maadili hayakuzingatiwa.”……………………
  ………………………………


  ……………………………..Kwa mujibu wa uchunguzi wa MwanaHalisi, kampuni ya Mkono ililipwa na Tanesco – miezi miwili kabla ya uchaguzi, yaani 19 Agosti 2010 kiasi cha dola 1,088,550.00 (karibu sh 1.6 bilioni). Malipo hayo yalifanywa kupitia Ankara Na 124/10.

  Aidha kabla ya Mkono kuchukua kitita hicho cha fedha, tarehe 15 Julai 2009, Tanesco walilipa mwanasheria huyo kiasi cha dola 2,177,100.00 (karibu sh 3.7 bilioni. FGedha hizo zililipwa kupitia Ankara na 069/09.

  Nayo Rex Attorneys, imelipwa na Tanesco kiasi cha dola 47,552.25 kupitia Ankara Na.456/10 ya 28 Septemba 2010 kwa kazi ya ushauri katoka kesi Na. 15910 iliyofunguliwa na kampuni ya Richmond katika mahkama ya ICC dhidi ya Tanesco.

  Malipo mengine ya dola 472,000.00 yamefanyika 23 Juni 2010 kupitia Ankara Na 34/10 kwa ajili ya usuluhishi katika kesi Na 15910 kati ya Tanesco na Rchmond. Dola 83,504.46 zililipwa kama gharama za kukodisha chumba cha kusikiliza usuluhishi kati ya Tanesco na Richmond kwa kesi hiyo hiyo.

  Source; MwanaHalisi.
   
 2. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  MMMnnnh!!!:A S-confused1:
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Huyo wakili aliyekuwa highlited in red ni yule aitwaye Fungamtama. Mbona hakamatwi kwa ulaghai na utapeli? Hii serikali jamani, mbona ime-stoop so low kwa mafisadi? Tutafika wapi kwa mwenendo huu? Au JK naye alikuwa anapata huo mgao?

  Ni kweli, CDM wakitamka hayo wanaambiwa wanataka kutamka nchi kwa nguvu -- lakini Makamba anawaambia huo huo ukweli.

  Ningependa CCM itokomee hata kesho ikiwezekana!
   
 4. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  We mwanzisha mada, kazi haina tija kwa nani? Specify
  Jiulize mawakili hao, kampuni hizo za mawakili zilizolipwa ni za kina nani?
  Kwa nini ni kampuni hizi tu kila kesi? na kesi zote wanapoteza!
  Law chambers ziko ngapi bongo?
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,909
  Trophy Points: 280
  michongo.. Ndio maana hawa jamaa hawatakubali kuiachia nchi iendoke bure bure bila ya mziki kama wa tahrir square
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Asante kwa angalizo: Nimebadilisha headline.
   
 7. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Duh! Yaani shule hazina waalim, madawati, vifaa vya maabara; na huduma za afya ziko kombo kumbe kuna watu wananyonya maziwa ya watoto kilaini hivyo.

  CDM endeleeni na maandamano mpaka kila mwenye masikio asikiye na mwenye macho aone madudu yanayofanywa na hawa wanasiasa
   
 8. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  walichota ccm kwa ajili ya uchaguzi
   
 9. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Juzi Professor Wangare Madhai wa Kenya wakati akiongea na BBC alisema: People deserve for leaders they have chosen. We really deserve.
   
Loading...