TANESCO Nyamagana ni wazembe na wabovu kiutendaji

Indume

Member
Apr 11, 2011
81
36
Hii ofisi ya TANESCO Nyamagana ni wabovu kiutendaji.

Kuanzia kitengo cha huduma kwa Wateja; Mafundi na Uongozi mzima wa hiyo ofisi. Mteja akiwa na fault ukitoa taarifa inazidi masaa 48 na bado tatizo la mteja halitatuliwi.

Hata ukiomba namba za mafundi hupewi na hata Meneja hawataki kutoa namba zake. Wananchi wanakoswa sehemu ya kutoa malalamiko yao.

Hii inasababisha Serikali kukosa mapato maana Luku hainunuliwi na pia shughuli za Mteja hukwama kusababisha uzalishaji kutokuwepo (mteja hukwama kuzalisha bidhaa na mauzo hupunhua na kodi kwa serikali hukosekana).

Ningeshauri wizara inayohusika iimike TANESCO Nyamagana.

Mbona TANESCO wilaya zingine ulitoa tu taarifa mafundi wanafika ndani ya muda mfupi?
 
Hao tanesco ukiujua ukweli, inabidi kuwahurumia tu!!kuna kipindi nilikuwa na tatizo, nimekaa siku tano gizani!!ila siku walipokuja niliwaonea huruma waliniambia mkoa wote huu wa tanesco, tuna gari moja tu ndio linalotumika! Na hata ukimpigia mkurugenzi huwezi pata msaada wowote kwani anafahamu hali halisi!!ila wanasiasa ndio wapotoshaji!!ukweli tanesco hawana vitendea kazi hadi mafundi ni wachache sana!
 
Hao tanesco ukiujua ukweli , inabidi kuwahurumia tu!!kuna kipindi nilikuwa na tatizo, nimekaa siku tano gizani!!ila siku walipokuja niliwaonea huruma waliniambia mkoa wote huu wa tanesco, tuna gari moja tu ndio linalotumika!!na hata ukimpigia mkurugenzi huwezi pata msaada wowote kwani anafahamu hali halisi!!ila wanasiasa ndio wapotoshaji!!ukweli tanesco hawana vitendea kazi hadi mafundi ni wachache sana!!
Mkuu kwa Nyamagana kama kitovu cha jiji sizani kama watakua na gari moja
 
Gari wanazo! Tunaongea kwenye uhalisia!! Labda tuseme wanataka rushwa tu!

Mbona Ilemela na maeneo mengine hakuna usumbufu huu?? Hebu jaribu kupiga huduma kwa wateja kama utasikilizwa! Maafisa wa TANESCO Nyamagana wana kauli mbaya sana kwa wateja! Imebaki kuwarekodi tu na kumtumia JPM.
 
Mkuu kwa Nyamagana kama kitovu cha jiji sizani kama watakua na gari moja
Kwa nyamagana sijui!!ila mimi ilikuwa tabata (dar)ckuamini kama wanaweza kuwa na gari moja, ila ndio hivyo!!ni kuwahurumia tu, kazi zinakuwa nyingi sana, vitendea kazi ni vichache!!ila ukimsikiliza mwanasiasa bwana!!
 
Hii ofisi ya TANESCO Nyamagana ni wabovu kiutendaji.

Kuanzia kitengo cha huduma kwa Wateja; Mafundi na Uongozi mzima wa hiyo ofisi. Mteja akiwa na fault ukitoa taarifa inazidi masaa 48 na bado tatizo la mteja halitatuliwi.

Hata ukiomba namba za mafundi hupewi na hata Meneja hawataki kutoa namba zake. Wananchi wanakoswa sehemu ya kutoa malalamiko yao.

Hii inasababisha Serikali kukosa mapato maana Luku hainunuliwi na pia shughuli za Mteja hukwama kusababisha uzalishaji kutokuwepo (mteja hukwama kuzalisha bidhaa na mauzo hupunhua na kodi kwa serikali hukosekana).

Ningeshauri wizara inayohusika iimike TANESCO Nyamagana.

Mbona TANESCO wilaya zingine ulitoa tu taarifa mafundi wanafika ndani ya muda mfupi?
Tafadhali tusaidia namba yako ya simu namba ya taarifa na tatizo tukuhudumie

Huduma kwa Wateja

MAKAO MAKUU
 
Huku kukatika kwa umeme kumezidi sasa. Tunaomba kujua kama mgao imeanza au la.
Halafu mnapenda sana kuomba namba za simu za watu. Ndio kusema mnataka kutengeneza database ya namba za simu???. Hebu rudisheni umeme huu uchumi wakati mtauhatibu wenyewe
 
Attachments

  • Screenshot_20210301_073953_com.quoord.jamiiforums.activity.jpg
    Screenshot_20210301_073953_com.quoord.jamiiforums.activity.jpg
    49.9 KB · Views: 3
  • Screenshot_20210301_073953_com.quoord.jamiiforums.activity.jpg
    Screenshot_20210301_073953_com.quoord.jamiiforums.activity.jpg
    49.9 KB · Views: 3
Hao tanesco ukiujua ukweli, inabidi kuwahurumia tu!!kuna kipindi nilikuwa na tatizo, nimekaa siku tano gizani!!ila siku walipokuja niliwaonea huruma waliniambia mkoa wote huu wa tanesco, tuna gari moja tu ndio linalotumika! Na hata ukimpigia mkurugenzi huwezi pata msaada wowote kwani anafahamu hali halisi!!ila wanasiasa ndio wapotoshaji!!ukweli tanesco hawana vitendea kazi hadi mafundi ni wachache sana!
Hii sitaki kuamini kabisa.
kwani kununua magari inagharimu kiasi gani ukilinganisha na mapato wanayoingiza kwa kuuza luku.
 
Tafadhali tusaidia namba yako ya simu namba ya taarifa na tatizo tukuhudumie

Huduma kwa Wateja

MAKAO MAKUU
Hivi namba ya simu ya mtoa taarifa inasaidia nini katika ufanisi wenu wa kazi.
Maana mtoa taarifa kwa maelezo yake huo uzembe unafanywa katika wilaya yote ya nyamagana na sio kwenye nyumba yake peke yake.
Sasa sioni mantiki ya kuomba namba ya simu wakati wilaya ya nyamagana inafahamika ilipo na watumishi waliopo huko wanajulikana.
Yaani unachokifanya ni sawasawa na mtu anayejifanya ana hasira anataka kupigana halafu anawaambia washabiki"nishikeni jamani mimi nitaua mtu leo,nishikeni jamani nisije nikaua leo"
 
Kwa nyamagana sijui!!ila mimi ilikuwa tabata (dar)ckuamini kama wanaweza kuwa na gari moja, ila ndio hivyo!!ni kuwahurumia tu, kazi zinakuwa nyingi sana, vitendea kazi ni vichache!!ila ukimsikiliza mwanasiasa bwana!!
Bado ni uzembe wao tu,kwa nini kukosekane magari na shirika lipo tangu enzi na enzi.
 
Lawama tunawapa wafanyakazi, wakati ni uzembe wa wana siasa?!!ukimsikiliza waziri anakwambia mtu akilipia gharama za kuunganishiwa umeme leo, wiki ijayo avutiwe umeme, nenda tanesco una kuta hakuna mita, hakuna nguzo!!na serikali wanalijua hilo!!
 
kwa nini kusiwe na mita?ni nani anahusika na procurement ya hizo mita?bado tunarudi palepale kwenye uzembe,wanangoja hadi Rais aende kusema ndio wachangamke

Back
Top Bottom