Tanesco njooni mtutengenezee umeme huku mbweni baharini unacheza kati ya volt 70 mpaka 270

Nyikanavome

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
463
250
Tokea jana usiku hapa kwetu umeme unacheza kati ya volti 70 mpaka 270 na unahatarisha usalama wa vyombo vyetu. Yaani hapa nimezima kila kitu. Tatizo la umeme mdogo ni la siku nyingi hapa mbweni baharini karibu na chuo cha usalama wa taifa.
Tatizo hili la kuyumba kwa umeme kila baada kama ya dakika kumi kwa kupananda na kushuka mpaka vitu vyote vinazimika lilianza jana usiku.

Nawaomba TANESCO TAGETA AU WENGINE MNAOHUSIKA MSHUGHULIKIE SWALA HILI MAPEMA, MHAKIKISHE TUNAPATA UMEME WENYE VOLTI ZA KUTOSHA SIO KILA SIKU UMEME UNASHUKA NA INABIDI KILA KITU UTUMIE STABILIZER INAYOWEZA KUPANDISHA UMEME KUTOKA 100VOLT MPAKA 220. UNAPOSHUKA MPAKA 70 VOLT NDIPO MAJANGA YANAPOANZA.

TIMIZENI WAJIBU WENU NDIO MTUTAKE TULIPIE BEI KUBWA
 

Nyikanavome

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
463
250
Waliukata kama dakika 40 hivi ulivyorudi hauchezi tena sana ila bado tatizo la low voltage lipo pale pale kwani sasa una range kati 160 hadi 175 volt. Hapa kama unatumia fridge guard au ac guard imekula kwako kwani zile umeme chini ya volt 190 haziwaki.
Tanesco kama mmeunganisha watu wengi kwenye transformer ndogo tubadilishieni. Mtu unashidwa hata kufunga hata ac kwenye nyumba kwani haiwezi kufanya kazi kwa umeme wenu huu wa kutupimia kwenye kijiko.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom