TANESCO ni mdudu hatari kwa maendeleo yetu

Nsaji Mpoki

JF-Expert Member
Nov 5, 2007
396
65
Hatuna hakika Kama viongozi wetu wanafahamu Kuwa shirika hili la umma limekuwa kero kwa wananchi hasa wateja wake.

Hivi unawezaje kuchukua fedha ya mteja Halafu ukamwambia utampatia huduma baada ya mwezi Mmoja kupita. Wananchi wanalipia kwa lengo la kufungiwa umeme, wengine zaidi ya shillingi laki tano Lakini baada ya kulipa majibu NI kusubiri huduma mwezi mzima. Hivi tunakwenda wapi.

Tunakamata vishoka wa nini wakati chanzo ni shirika lenyewe? Tafadhali mhe. Simbachawene shughulikia hili. Customer care ni extremely low.
 
Hii mambo ni mchanganyiko mkubwa. yapo yanay0fanyia kwa uwezo duni wa tanesco unaosababishwa na ufisadi wa ccm, na yapo ya uzembe na hulka ya huduma mbovu za serikali kwa wananchi.

Tunaomba number ya mkurugenzi makao makuu, tumwambie yanayofanywa na Tanesco ambayo yeye bila shaka hayajui wala hawezi kuridhia.

Wekeni number yake hapa tutiririke!
 
MIMI hapo kwenye service charge za kila mwezi 7250 ndipo napo choka na hao mafisadi ccm
 
Yaani tanesco ni majinga tu yamejaa humo, customer service ni sifuri, umeme wenyewe ghali, halafu Isitoshe wanakata umeme kila siku huku tukipo sisi, jana wamekata saa nane usiku na kurudisha saa moja jioni, leo yamekata saa kumi na moja mpaka sasa umeme haujarudi, hayawezi kazi na serikali inalazimisha hawa wapumbavu wawe wasambazaji pekee wa umeme nchini. Wenyewe ccm wanajua kazo ya gesi ni kuuzwa tu hawafikiri hata kuhakikisha wadhamini wanatatua tatizo la umeme, kisa wanajua hayo mafuta yanayoendeshea mitambo ni dili lao. Maisha ya mjini yanategemea asilimia kubwa umeme halafu hawa wajinga wanakata kata umeme kila siku hata mida ya kazi, cha kushanganza wanajifanya wanataka kupeleka umeme vijijini, wana unit gani za kulifanikisha hilo wakati mjini yenyewe umeme shida?? Yaani hawawezi kazi ni uozo mtupu huko, swala la umemw ni la kubinafsishwa hii serikali haijawahi kusimamia tatizo likatatuliwa ni ujinga ujinga ujinga tu. .huyu kikwete kakuta tatizo la umeme na analiacha halafu anajisifu kwa kuwapa wanawake uongozi? Hiyo imetunufaishaji sisi watanzania wa chini? Tumepata maji safi kutokana na hilo? Limetatua tatizo la umeme? Pesa imepanda thamani? Yaani mtu yeyote anayeipiga kura ccm ningekua na uwezo ningemlaani kabisa
 
Ref BR10ZW502
Meter 01340309141
Receipt EVG310200361
Units 27.50KWH

Token 0995 1895 7347 7648 7976

Cost TZS 8196.72
Tax TZS 1803.28
Total TZS 10000
eSign
Kwa hali hii solar ina umhimu wake. Mtu mfanyakazi wa serikali kwenye mshahara unakatwa kodi kama elfu therethini na kitu kila mwezi. Ni afadhari mpunguze kodi ili tuweze kulipa charge kama hizo za umeme. Ukinunua umeme kuna kodi ya mwezi elfu 7000 na ushee halafu kila mwezi kuna kodi inakatwa kila mteja akinunua umeme kama inavyoonyesha hapo juu. Ninaishi nyumba ya kupanga natamani nijenge yangu niweke solar.
 
Kweli Tanzania maisha ni gharama hata kwa vitu tunavyozalisha sisi wenyewe inafika wakati mtu unajilaumu kwa nini ulizaliwa mtanzania.
 
Back
Top Bottom