TANESCO ni kama Tembo Kila anaepata nafasi anakata mnofu mpaka shirika linaelekea kufa halafu Leo mnaleta siasa za kijinga kutafuta kiki

Ndugu zangu kwa Tanzania hakuna shirika la uma ambalo limepitia changamoto kama shirika la umeme TANESCO.Shirika hili tangu kipindi Cha Mzee wa ruksa wanasiasa walianza kulitumia kama kitega uchumi Chao .Wakawa wanasaini mikataba ya kihuni lengo likiwa kupata asilimia kumi.
Ikaja awami ya
Mr Clean a.k.a Ben mambo yakendelea hivohivo Tena ilafkia muda shirika likataka kubinafisishwa .

Huyu alikuja na sera ya kutolipa shirika resources za aina yoyote hasa kuajili wafanyakaza wapya lengo likiwa ni kilizoofisha shirika ili hatimae waliuze.Sijajua nini kilitokea hadi likasalimika kuuzwa
Kutokana na shirika kutokua na lasilimali za kutosha kujiendesha mnakumbuka mwaka 2006 mgao wa umeme ulivokua mkubwa hadi wanasiasa Tena wakaingia mikataba ya dhalula kuinusulu Nchi isiwe gizani,mambo ya Richmond na hatimae Lowasa kuachia ngazi.

Awamu ya nne nayo ikaja kwa uchu mkubwa Sana kulimaza shirika kwa mikataba ya kihuni lengo likiwa lilelile la kilimaliza .Waanasiasa kwa kushilikiana na wafanyabiashara wakubwa wamekuwa mabilionea wakubwa kwa kulitumia hili shirika na kilifanya lishindwe kijiendesha .Kwa taalifa yenu tu Tanesco inaijiendesha kwa hasara hivo inapewa luzuku kutoka serikalini.Yote ni kutokana na ufisadi wa kutisha zidi ya hili shirika.

Awamu ya Tano chini ya JPM kwa kuona Hilo ndo wakaja na suluhu ya haya matatizo kwa kukataa Tena kuingia mikataba mipya .Na njia zenyewe ni kujenga Nyerere dam ili hatimae tuwe na umeme wetu wa uhakika.
Sasa Leo anatokea mwanasiasa anadanganya watu eti sitaki umeme ukatike Tena wakati Tanesco wanajiendesha kwa luzuku ya serikali Sasa mtu unajiuliza hivi Hawa jamaa wanatumia akili gani?
Je wamelipa shirika hela ya kufanyia mabolesho ya mitambo na njia za usambazaji umeme wakashindwa?
Nawaomba wanasiasa muache siasa kwenye mambo ya muhimu ya Nchi yetu maana tatizo la Tanesco linajulikana.Shirika halina PESA kwa ajili ya kujiendesha .Tena kama mna Hekima mnatakiwa mtoke mbele ya uma wa Kitanzania muombe msamaha kwa hujuma mlizowafanyia Watanzania.

Nimeandika machache Sana kuhusu hili shirika mnataongezea mengine lakini mkumbike viongozi wazalendo katika Nchi hii ni wachache Sana wengi wapo kwa ajili ya kupoga
Wacha wale lakini kila jambo Lina mwisho hata miaka 100 ijayo ipo siku historia itabadilika
 
Tuondoe kuwa bila Tanesco huwezi pata umeme!turuhusu serikali zote za mitaa zenye uwezo wa kuzalisha umeme zifanye hivyo na ziuzie wakazi wake directly(tanesco wachukue fungu lao la miundo mbinu)turuhusu private people's,vyombo vya kidini vizalishe umeme kama vinauwezo na ilibidi wawauzie tanesco,umeme rafiki hasa wa solar na upepo upewe nafasi ya upendeleo,gawa hili shirika la umeme ziwe kampuni mbili,moja ya uzalishaji tu na nyingine usambazaji tu ili kuua urasimu wa Tanesco,elimu muhimu kwa watumiaji wa umeme upewe kipaumbele kikubwa,zima kila kitu kama hukitumii!vyombo vyote vya umeme chomoa socket kabisa kama havitumiki,kale kataa kekundu kanatumia umeme!
Matatizo yalianza kipindi cha JK akiwa waziri wa nishati na madini, akaingia mikataba na akina Ruge, PAP, leo kamutoa swahiba wake Ruge baada ya JPM kumuadabisha miaka minne yuko nyuma ya nondo.

,.---++++++
Huu Mzozo wa IPTL

Hawa jamaa baada ya kuingia makubaliano na TAnEsCo ya kuzalisha umeme megawati 100..mwaka 1995...walikaa muda kdg bila kuzalisha lqkini walilambq capacity charges

Baaadae hiv waliendqa benk kupata Mkopo.

Kwa kuwa walikuwa na Mkataba na TAnEsCo waliomba mapato Yao ya umeme yawe ni Guarantee Kwa mkopeshaji...

Standard Chartered Hong Kong I think walipewa hiyo Government Guarantee (international)...Benk ikatoa fedha Kwa IPTL ya kutosha..

Sasa hiyo Government Bank Guarantee ilisumbua Sana...

Kwa nini..

IPTL Walidefault bank loan. Kwa hiyo benk ukawa inapambana na serikali walipwe Kwa kuwa Wana Govt guarantee..ila hawa walifungua kesi kudai pesa zao na wakalipwa through Court decree Bill 306 has gone..Judge Utamwa

it was a very interested court case..

Hapo Kati Kati mara kadhaa serikali ilijitahidi kukana makubaliano lqkini ilishindikana.

All that I know...

Mikataba mibovu

1. Bill 320 Za capacity charges zilizokuwa BOT zimelipwa Kwa hawa wanaume wawili Ruge na Seth wa PAP Kwa umeme ambao megawat 100 hazikuzaliswa ipasavyo. Kumbukq 1995 mpaka 2013 nilikuwa na shida Sana ya umeme hasa wakat wa Jk na tulilipishwa Capacity Charges bila kuzingatia Umeme umepata au la..

Mabilion haya 320 ndiyo kiasi cha fedha kinqchojenga Mawizarq yote 26 tena maghorofa hapa Dodoma

2. Kule kwenye Mabenk ya nje wanadai pesa zao USD 200Million kama Bill 400 na wameshinda kesi UK na Malaysia ( Standard Charted Bank) huyu Seth allikopq huko kwao Kwa kuweka mapato ya kutoka Serikali/TAnEsCo kuzalisha hizo Megawat 100..qmbazo pia walishindwa kupata kipato cha kulipa hayo madeni mpaka Leo hii..

Serikali inatakiwa ilipe na riba juu yake

Aisee too tough..

Walipata pesa za kutosha sana
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Kwa kweli January kaingia Wizara na gia feki.
TANESCO yenye madeni ya kutisha ati hatutaki umeme ukatike.
Miundombinubyenye ni dhoofu na ya miaka mingi.
Tuone miujiza ya kubadilisha miundombinu hiyo ndani ya wiki mbili.
Huyu mshemiwa anachekesha Sana,shirika wameliua wanasiasa haohao eti Leo anawatimpia lawama wafanyakaza.
Namkumbusha Tena shida ya Tanesco ni kujiendesha kwa hasara kutokana na mikataba ya wizi inayowanufaisha wanasiasa wezi kwa kushilikiana na matajili wezi .Tanesco Haina bajeti ya kukalabati miundombinu yake Sasa umeme utaachaje kukatika .Hii ni sawa mzazi hutaki kumlipia ada mwanao na unaenda kwa watu kiwambia mtoto hataki shule,Aibu .
 
Matatizo yalianza kipindi cha JK akiwa waziri wa nishati na madini, akaingia mikataba na akina Ruge, PAP, leo kamutoa swahiba wake Ruge baada ya JPM kumuadabisha miaka minne yuko nyuma ya nondo.

,.---++++++
Huu Mzozo wa IPTL

Hawa jamaa baada ya kuingia makubaliano na TAnEsCo ya kuzalisha umeme megawati 100..mwaka 1995...walikaa muda kdg bila kuzalisha lqkini walilambq capacity charges

Baaadae hiv waliendqa benk kupata Mkopo.

Kwa kuwa walikuwa na Mkataba na TAnEsCo waliomba mapato Yao ya umeme yawe ni Guarantee Kwa mkopeshaji...

Standard Chartered Hong Kong I think walipewa hiyo Government Guarantee (international)...Benk ikatoa fedha Kwa IPTL ya kutosha..

Sasa hiyo Government Bank Guarantee ilisumbua Sana...

Kwa nini..

IPTL Walidefault bank loan. Kwa hiyo benk ukawa inapambana na serikali walipwe Kwa kuwa Wana Govt guarantee..ila hawa walifungua kesi kudai pesa zao na wakalipwa through Court decree Bill 306 has gone..Judge Utamwa

it was a very interested court case..

Hapo Kati Kati mara kadhaa serikali ilijitahidi kukana makubaliano lqkini ilishindikana.

All that I know...

Mikataba mibovu

1. Bill 320 Za capacity charges zilizokuwa BOT zimelipwa Kwa hawa wanaume wawili Ruge na Seth wa PAP Kwa umeme ambao megawat 100 hazikuzaliswa ipasavyo. Kumbukq 1995 mpaka 2013 nilikuwa na shida Sana ya umeme hasa wakat wa Jk na tulilipishwa Capacity Charges bila kuzingatia Umeme umepata au la..

Mabilion haya 320 ndiyo kiasi cha fedha kinqchojenga Mawizarq yote 26 tena maghorofa hapa Dodoma

2. Kule kwenye Mabenk ya nje wanadai pesa zao USD 200Million kama Bill 400 na wameshinda kesi UK na Malaysia ( Standard Charted Bank) huyu Seth allikopq huko kwao Kwa kuweka mapato ya kutoka Serikali/TAnEsCo kuzalisha hizo Megawat 100..qmbazo pia walishindwa kupata kipato cha kulipa hayo madeni mpaka Leo hii..

Serikali inatakiwa ilipe na riba juu yake

Aisee too tough..

Walipata pesa za kutosha sana
Inaumiza Sana na hapa ndo Huwa nawaza je kazi ya Usalama wa Taifa ni nini kama sio kuzuia hizi hujuma kama hizi?Je nchi tumekubali kuwapa wanasiasa wezi?Maslahi ya Nchi yetu kiuchumi ni nani mlinzo wake?Je tutaenda hivi hadi lini maana Nishati ya umeme ndo moyo wa nchi .
 
kweli nisehemu yakupigia hela sn nasikia inaingiza zaidi ya tri 3 kwa mwezi cash

bado inategemea na ruzuku kutoka serikali kuu

inaitajika reform ya maana sn shirika liwez kuwa productive na kujitegema kwakwel
 
Tuondoe kuwa bila Tanesco huwezi pata umeme!turuhusu serikali zote za mitaa zenye uwezo wa kuzalisha umeme zifanye hivyo na ziuzie wakazi wake directly(tanesco wachukue fungu lao la miundo mbinu)turuhusu private people's,vyombo vya kidini vizalishe umeme kama vinauwezo na ilibidi wawauzie tanesco,umeme rafiki hasa wa solar na upepo upewe nafasi ya upendeleo,gawa hili shirika la umeme ziwe kampuni mbili,moja ya uzalishaji tu na nyingine usambazaji tu ili kuua urasimu wa Tanesco,elimu muhimu kwa watumiaji wa umeme upewe kipaumbele kikubwa,zima kila kitu kama hukitumii!vyombo vyote vya umeme chomoa socket kabisa kama havitumiki,kale kataa kekundu kanatumia umeme!
Kugawa kampuni ni kuongeza matembo zaidi. Na kila tembo atahitaji mnofu zaid ya mwenzie
 
Kuanzia napata ufahamu sijawahi kusikia kuna wizara yoyote ile ikisifiwa100% rakini kwa hili la Tanesco it's too much

Japo tunaongea sana lakini watanzania tusisahau mwarobaini pekee katika hayo yote na mengineyo ni KATIBA mpya pekee

Tena Katiba mpya kabisaa.sababu ile ya mzee wangu Waryoba ilishachakachuliwa

Tuacheni mzaha katika hili ni miaka 60 sasa hii ni aibu kwa taifa kubwa Kama hili
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Wacha wale lakini kila jambo Lina mwisho hata miaka 100 ijayo ipo siku historia itabadilika
Kwa akili hz za watanzania hata ipite miaka 10000000000 kama akili hazitabadilika, basi hakuna kitachobadilika. Just assume mtu mmoja anatamka "sitaki umeme ukate nawapa week mbili" afu watu wanapiga makofi bila kuuliza je umeweka mikakati gan kuhakikisha huo umeme haukat?

Watanzania n watu wa ajabu sana,, asubuh anaamka anabishana simba na yanga nani kasajili kuzidi mwenzie

Ikifika mchana anabishana mondi na kiba nani ana magari mengi

Ikifika jion ansbishana kati ya mwamposa na sheh ponda ni nan kachanjwa

"Je unafikir mtu kama huyu atapata wapi mda wa kutafakari na kujadili mambo ya kitaifa??
 
Hivi jamani huko Tanzania yale mabwawa maarufu ya kuzalisha umeme ya Kidatu, Mtera, Kihansi,Pangani yaliacha kuzalisha umeme? au ndo stories zilezile zinaendelea kama kawaida.... poleni sana na kaazi iendelee...
Kwani umeme unaotumia kwa sasa ni wa wapi?
 
Biashara ya umeme iwe huria. Mfanyabiashara anayewwza kuzalisha, azalishe na kuuza.
 
Back
Top Bottom