TANESCO nao waja na dili lao. Pres. Magufuli ana kazi kubwa

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,698
4,693
Wakati huu bado tunatatanika na kuulizana imekuwaje rais kuzuia matumizi ya pesa ktk sherehe za kuzima mwenge kipindi cha mwisho. Last minute. Lengo ni kuokoa kiasi fulani cha pesa pamoja na muda wa viongozi walioelekea kusafiri nchi nzima.

Nionavyo, sasa rais anahitaji kutoa adhabu kali kwa tabia hii ya matumizi mabaya ya pesa. Yaonekana wakuu wa taasisi na viongozi wa sehemu nyingi wanahangaika kukwepa maamuzi ya rais na wale wasioonekana, wanapeta.

Jana Tanesco nimewasikia wakitangaza dili yao ya nchi nzima. Wanaiita utafiti wa upatikanaji wa umeme vijijini. walitoa ombi kwa wananchi kuwapokea watafiti hao, nadhani ni baada ya yale yaliyowapata watafiti wa dodoma. Swali la kujiuliza ni taarifa gani haijulikani Tanesco kupitia matawi yake nchini, hadi wilayani? Tanesco ni jipu! Wanahangaika kuchota pesa za shirika toka kila kona na Mbinu.
 
rudia tena kuangalia hiyo habari halafu urudi...elimu elimu..
Ee Mola tujalie elimu waja wako..
 
Utafiti unafanywa na REA na NBS..huyu ngumbalu analeta habari za kisiasa hapa..

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa utafiti huo unafanya na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA) kwa kushirikiana na kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS).
 
Na kila mkoa kutakuwa na watalaam wanne team Yao itaongozwa na mtaalam mmoja
 
Back
Top Bottom