Tanesco na Waganga wa Kienyeji

Frank King

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
1,311
2,000
Nilishawahi kuhoji hili jambo hapa jukwaani wala sikupata majibu yenye kuridhika

Nauliza hivi?Hivi kweli TANESCO na TTCL wameshindwa kabisa kuwapigia simu Waganga wote walio gongelea matangazo yao juu hizi nguzo zetu?Yani inatia aibu kuona vijibao vimetapakaa nchi nzima vya hawa sangoma na mbaya zaidi kilicho Tangazwa hapo ni tofauti na maadili yakitanzania"PESA ZA MAJINI,KUJIUNGA FREEMASON,KUMVUTA MPENZI,NGUVU ZA KIUME,ZINDIKO n.k..Ebu ona sasa nini hiki?

Tena kwenye nguvu za Kiume huwa kwangu ni kero KUU!Yani hii nchi naistajabiaga kwamba yale mambo ya msingi kabisa ambayo yanauwezo wakuipotezea Nchi sifa wala hakuna mwenye habari nayo.
Lakini mambo meengi yasiyo na maana ndio yatabebwa kwa uzito wa ajabu

Au wamewafungu???nawafungua in the Name of Jesus..ondoeni huo uchafu kwani hauna faida yeyote zaidi yakufundisha watu tabia za ajabu..

Nimeshawasaidia sehemu kubwa kwa upande Falme na mamlaka kazi iliyobakia ni ndogo mno yaani kupitisha fagio nakutoa huo uchafu nchi nzima.

By
Mchungaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom