TANESCO na ujenzi holela kwenye njia kubwa ya kupeleka umeme kwenye Kituo cha Ubungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO na ujenzi holela kwenye njia kubwa ya kupeleka umeme kwenye Kituo cha Ubungo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by taffu69, Aug 6, 2012.

 1. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia matukio ya maafa makubwa yakiwakumba wananchi ambao wamejenga na kuendesha shughuli zao za kujikimu kimaisha kwenye maeneo hatarishi kama kwenye mabonde na fukwe za bahari pasipo kuchukua tahadhari yoyote. Katika hili mamlaka husika zimekuwa kimya mpaka pale maafa yanapotokea ndiyo mamlaka hizo zinatoa maelekezo ikiwamo kuwataka wahusika kuondoka kwenye maeneo hayo hali ambayo inaambatana na bomoa bomoa ya majengo hivyo kupelekea hasara kubwa kwa wahusika.Katika pita pita yangu hususan kwenye maeneo ya Ubungo, Kimara, Mbezi hadi Kibamba nimeshuhudia nyumba kadhaa za makazi zikijengwa chini ama pembezoni mwa Gridi kubwa ya Umeme inayopeka umeme kwenye kituo cha Ubungo. Hali hii imekuwa ikiendelea na hakuna hatua zozote za tahadhari zinazochukuliwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Jambo la kujiuliza ni kuwa:i. Hakuna mpaka halisi unaojulikana kisheria kwa ajili ya njia hiyo kubwa ya kusambazia umeme kama ilivyo kwa upande wa barabara?;ii. Kama mipaka hiyo ipo, kwa nini TANESCO isiweke alama kama inavyofanya TANROADS ili kuepusha hasara na usumbufu kwa wananchi wasiolewa mipaka halisi na pia kuepusha maafa yanayoweza kutokea pale nyaya zinapokatika ama kutokea kwa hitilafu yoyote; naiii. Ni nini wajibu wa EWURA katika kuhakikisha usalama wa jamii kama inavyoelekezwa kwenye Sheria ya Umeme Na. 10 ya mwaka 2008?Ni vyema mamlaka husika zikawa zinachukua hatua za tahadhari mapema badala ya kungojea hadi pale maafa yanapotokea ndiyo hatua za dharura zinachukuliwa.
   
Loading...