Tanesco na mgao wa umeme na bili isipungua

Ngoiva Lewanga

Senior Member
Aug 19, 2011
160
19
Ndg zangu wanajamii nisaidie kwa hili la mgawo wa umeme na bili isibadilika. Kabla ya mgawo matumizi yangu nyumbani ni unit 85-100, cha kushangaza mgawo ulipoanza rasmi ambao hadi siku mbili hakuna umeme, bili ni vilevile. Je, kunani tanesco?
 
Pole,lakini nadhani kabla ya kulalamika ungefanya kautafiti kidogo................kama unatumia mita ya kawaida jenga utaratibu wa kuisoma mita yako tarehe ambazo tanesco wanasoma mita ili kulinganisha readings za mita na zile zinazoandikwa kwenye bili yako.....ukiangalia bill yako ina namba zinazoandikwa kama previous readings,hizi ni zile namba zinazosomeka kwenye mita kabla ya matumizi ya umeme kwa mwezi husika,halafu kuna current readings,hizi ni zile namba zinazosomeka baada ya matumizi ya umeme,tofauti ya namba hizi ndio matumizi yako kwa mwezi husika.kwa mujibu wa maelezo yako kuna uwezekano wa matatizo mawili.1.inawezekana tanesco hawasomi mita vizuri au hawasomi kabisa na badala yake kukadiria bill yako.2.kwa kawaida kunapokuwa na mgao wa umeme majumbani matumizi ambayo huwa yanapungua sana huwa ni matumizi ya umeme yanayotokana na kuwasha taa tu,kumbuka kuwa matumizi ya taa huwa hayazidi 20%ya matumizi yako; matumizi mengine kimsingi huwa hayabadiliki sana;fikiria kwa mfano idadi ya nguo unazopiga pasi kukiwa kuna mgao wa umeme au hakuna ni ile ile n.k.kama unatuma luku jibu la pili linaaply. Sitaki kuamini kuwa kuna ujanja wowote unaofanywa na tanesco kuhakikisha mapato yao hayashuki.nawsilisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom