TANESCO: Mvua zikiendelea kunyesha katika mabwawa, changamoto ya upungufu wa umeme itapungua

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,239
24,099

Changamoto za Upungufu wa umeme Kupatiwa Ufumbuzi

Mkurugenzi mkuu wa TANESCO Bw. Maharage Chande akizungumza na waandishi wa habari leo December 2, 2022 kuhusu hatua za muda mfupi na muda mrefu kumaliza upungufu wa umeme .

Mkurugenzi ameongeza kuwa mvua zinazonyesha muda huu nchini bado hazijaweza kutiririka katika mito ya maji inayoingia katika mabwawa ya umeme.

Hivyo juhudi zimeelekezwa mitambo ya gesi na kukarabati mitambo huku mvua zinazoendelea kunyesha hatimaye kujaza mito inayotiririsha maji katika mabwawa ya umeme.

---
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ameelezea mikakati yao wanayoendelea nayo pamoja na changamoto wanazokutana nazo katika harakati zao za kurejesha huduma ya umeme.

Amesema “Tayari tumeshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa LM6000 katika kituo cha Ubungo namba III na umeshaanza kuingiza megawati 35 za umeme katika Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 25 Novemba 2022 kama tulivyoeleza hapo awali.

“Tayari tumeshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kidatu na umeshaanza kuzalisha megawati 50 za umeme katika Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 30 Novemba 2022.

“Matengenezo ya mtambo mmoja katika kituo cha Kinyerezi namba II yameshakamilika na tayari umeshaanza kuzalisha megawati 215 za umeme kuanzia tarehe 24 Novemba 2022.”

Kuhusu juhudi zao za muda mfupi, amesema majaribio ya mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I yanaendelea, na kwa sasa mitambo hiyo inaingiza jumla ya megawati 65 za umeme katika Gridi ya Taifa. Pia wanategemea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Disemba 2022, mitambo hii itakuwa inazalisha jumla ya megawati 90 kama tulivyoeleza hapo awali;

Ameongeza kuwa bado wanaendelea na kazi za matengenezo ya mitambo miwili ya Ubungo namba III ambapo baada ya kukamilika mwishoni mwa Disemba 2022, itazalisha jumla ya megawati 40 za umeme.

JITIHADA ZA MUDA WA KATI ZINAZOENDELEA KUFANYIKA
Ameseme “Tunategemea mitambo mingine miwili kuanza kufanya kazi katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I kuanzia mwezi Februari 2023 ili kuingiza megawati 90 za umeme katika Gridi ya Taifa.

“Iwapo mvua zitaendelea kunyesha katika mabwawa yote ya kufua umeme na matengenezo yaliyobakia kukamilika kama yalivyopangwa, basi tunategemea hali ya umeme itaendelea kuimarika na hivyo tunatarajia kiasi cha upungufu wa umeme kwa siku kuendelea kupungua kutoka wastani wa kati ya megawati 300 hadi 350 wiki iliyopita hadi kufikia megawati 215 za umeme wiki hii.”
 
JPM akiongea bungeni akasema kuna watu wanapunguza kina cha maji ya Mtera ili mtaani pawe na mgao mkali wa umeme ili wapigaji wapate sababu ya kutajirika.

Mpaka anakufa hakuna ushahidi wowote wa maana uliowekwa wazi wa tuhuma za wizi huo wa TANESCO!, Ni shirika kubwa la umeme lenye kuingiziwa siasa na wanasiasa wanaotafuta popularity za mitandaoni.

Tukiwa wabunifu kidogo tu tunaweza kuwa na vyanzo mbalimbali vya umeme na maisha yakawa yanaendelea pasipo haja ya kuwa na migao ya umeme inayorudisha nyuma juhudi mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.
 
Mkurugenzi mkuu wa TANESCO Ndugu Maharage Chande amesema tatizo la Ukame ambalo limepelekea upungufu wa umeme bado lipo, japokuwa ya mvua kuanza kunyesha baadhi ya maeneo nchini.

Amesema kuwa bado mvua hazijanyesha maeneo muhimu kwa uzalishaji wa umeme kwa kupitia maji na kina na cha maji kwenye mabwawa mbali mbali bado kinaendelea kushuka.

Hivyo wamejikita zaidi katika kuongeza uzalishaji wa umeme kupitia gesi. Amesema hayo akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 02/12/2022.
 
Kwahio makato ya umeme kila kona yapo palepale hadi kieleweke? Mwendo wa kukata tu na kugawana mafungu.
 
Huwa najiuliza kwanini hayo marekebisho makubwa ya mitambo anayodai ya lazima, wanayafanya kwa pamoja, na kwa wakati mmoja, hivyo kusababisha kuleta upungufu mkubwa wa umeme?

Kwanini wasingefanya hayo marekebisho kwa vituo vichache kwa wakati, ili vituo vingine viendelee kuzalisha umeme na kuepusha haya makali ya mgao wa umeme uliopo kwa sababu ya kufanya kwa vituo vyote kwa wakati mmoja?

Hivi kwa akili ndogo kama hii, amekosekana kabisa mtu huko serikalini wa kuwashauri hawa jamaa waache huu ujinga wao wanaotufanyia? kwa namna hii watu wakiamini huu mgao ni wakutengeneza ili wauze majenereta watakataa vipi?

Bad enough, huyo Maharage anatumia neno "endapo" marekebisho yatakwisha kwa wakati, hii maana yake hawa jamaa wanatuliwaza kwa ujinga wa makusudi wanaotufanyia, neno "endapo" linaonesha hawana uhakika na kazi zao, hawa ni matapeli na waongo, hawafai kabisa.

Huu mgao uliopo sasa Tanzania Bara sitashangaa kama utaenda kwa muda mrefu ujao, ikiwezekana mpaka mwakani, kwasababu hawa kina Maharage wanachofanya ni kutuliwaza tu kisaikolojia na hizi press zao, lakini kimsingi hawako serious, wanatuchezea tu kama watoto wadogo.
 
Mkurugenzi mkuu wa TANESCO Ndugu Maharage Chande amesema tatizo la Ukame ambalo limepelekea upungufu wa umeme bado lipo, japokuwa ya mvua kuanza kunyesha baadhi ya maeneo nchini. Amesema kuwa bado mvua hazijanyesha maeneo muhimu kwa uzalishaji wa umeme kwa kupitia maji na kina na cha maji kwenye mabwawa mbali mbali bado kinaendelea kushuka. Hivyo wamejikita zaidi katika kuongeza uzalishaji wa umeme kupitia gesi. Amesema hayo akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 02/12/2022.
Wafanye wanavyofanya.. Kikubwa wasiuze Tanesco tuu maana tumewashtukia kigambo wala njama.. Wakiongozwa na yule jamaa mvaa suti alafu kichwani akili imevaa magunia
 
Wehu kweli, sisi hatuhitaji hizo bla blah zenu unatubinulia mdomo mtoto wa kiume vipi wewe bana, sisi tunataka umeme kwakuwa tunalipia na uwezo wa kulipia tunao.
 
02 December 2022

Changamoto za Upungufu wa umeme Kupatiwa Ufumbuzi

Source : millard ayo
Mkurugenzi mkuu wa TANESCO Bw. Maharage Chande akizungumza na waandishi wa habari leo December 2, 2022 kuhusu hatua za muda mfupi na muda mrefu kumaliza upungufu wa umeme .

Mkurugenzi ameongeza kuwa mvua zinazonyesha muda huu nchini bado hazijaweza kutiririka katika mito ya maji inayoingia katika mabwawa ya umeme.

Hivyo juhudi zimeelekezwa mitambo ya gesi na kukarabati mitambo huku mvua zinazoendelea kunyesha hatimaye kujaza mito inayotiririsha maji katika mabwawa ya umeme.

More info:

30 December 2022

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeelezea sababu za uwepo wa upungufu wa umeme kuwa unasababishwa na ukame pamoja na matengenezo kinga na marekebisho makubwa kwenye vituo na mitambo, na kusababisha upungufu wa jumla ya megawati 300 hadi 350 za umeme kwa siku za hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Maharage Chande alisema upungufu wa umeme unasababishwa na ukame pamoja na matengenezo ya mitambo.

“Upungufu huu unasababishwa na mambo makubwa mawili, ukame mkubwa ambao nchi yetu inapitia na matengenezo kinga na marekebisho makubwa ya mitambo ambayo ni lazima yafanyike” alifafanua Bw. Chande.

Aidha, Bw. Chande aliviainisha vituo vya kufua umeme vilivyoathiriwa na ukame ambavyo ni Kihansi kinachozalisha megawati 17 badala ya megawati 180 kwa hiyo megawati 163 hazizalishwi; Pangani kinachozalisha megawati 10 badala ya megawati 68 kwa hiyo megawati 58 hazizalishwi.

Vituo vingine ni Mtera kinachozalisha megawati 75 badala ya megawati 80 kwa hiyo megawati 5 hazizalishwi na Nyumba ya Mungu kinachozalishaji megawati 3 badala ya megawati 8 za umeme, kwa hiyo megawati 5 hazizalishwi.

Vilevile, Bw. Chande alivitaja vituo vilivyo katika matengenezo kinga kuwa ni Kidatu kinachozalisha megawati 150 badala ya megawati 200, kwa hiyo megawati 50 hazizalishwi; Ubungo III kinachozalisha megawati 37 badala ya megawati 112, kwa hiyo megawati 75 hazizalishwi.

Kituo kingine ni Kinyerezi II kinachozalisha megawati 205 badala ya megawati 237, kwa hiyo megawati 32 hazizalishwi. Alifafanua jumla ya umeme ambao hauzalishwi kwa sababu ya ukame na matengenezo ni megawati 388 za umeme hadi kufikia 23 Novemba 2022.

Akieleza mipango ya muda mfupi ya kunusuru hali ya upungufu wa umeme, Bw. Chande alisema ni kuharakisha matengenezo ya mtambo katika kituo cha Ubungo III ili kuingiza megawati 35 za umeme hadi kufikia leo, kuharakisha matengenezo ya mitambo miwili ya Ubungo III ili kuingiza megawati 40 za umeme mwishoni mwa mwezi Disemba 2022.

Sambamba na kukamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kidatu ili kuingiza megawati 50 za umeme tarehe 30 Novemba 2022 pamoja na kuharakisha ufungaji wa mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi I ili kuingiza megawati 90 za umeme kabla ya mwisho wa mwezi Disemba 2022.

“Iwapo matengenezo haya yatakamilika kama yalivyopangwa, yatatupatia jumla ya megawati 277 kwenye uzalishaji na kupunguza kadhia hii ya umeme,” alisisitiza Bw. Chande.

Aidha, Bw. Chande alisema juhudi za muda wa kati ni ukamilishaji wa ufungaji wa mtambo mwingine katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi I ili uanze kufanya kazi ili tuingize megawati 90 za umeme kwenye uzalishaji ifikapo mwezi Februari 2023 na kufikisha jumla ya megawati 337 za umeme.

Akihitimisha, Mkurugenzi Mtendaji alisema jitihada za muda mrefu ni kuharakisha ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere.

“Hatua za muda mrefu ambazo ni zaidi ya miezi 12 mpaka 18, ni matumaini yetu, nguvu zetu na nia yetu bwawa la Julius Nyerere likamilike ili upungufu wa umeme uwe umekwisha” alihitimisha Bw. Chande.

Source : TANESCO - CHANGAMOTO ZA UPUNGUFU WA UMEME ZAPATIWA UFUMBUZI

🙄🙄🙄🙄
 
Back
Top Bottom