Tanesco mnataka kuwaibia wakazi wa Mtwara na Lindi?

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,830
4,726
Kufuatia shirika la umeme Tanzania TANESCO kuruhusiwa kupandisha bei ya umeme kuna dalili za shirika kuwaibia wakazi wa Mtwara na Lindi. Hii ni kutokana na sababu waliotoa zinazopelekea kupandisha bei, sababu kubwa wanayosema ni kupungua kwa kina cha maji jambo litakalopelekea umeme kuzalishwa kwa mafuta na Gas.
Sasa Lindi na Mtwara tangu kitambo wanatumia umeme wa Gas tu, hawatumii umeme wa maji wala hawajaungwa kwenye grid ya taifa.
Je Tanesco inaweza kutoa sababu za msingi za kuwapandishia bei ya umeme wakazi wa Mtwara na Lindi?
Je kupandishwa kwa bei kutawahusu pia wafanyakazi wa TANESCO au wataendelea na utaratibu wao wa kujiuzia unit 700 kila mwezi kwa bei ya kutupa (chini ya elfu kumi)?
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom