Tanesco, miti ni mingi ila mnasema hamna Nguzo! Umeme umekuwa kwa ajili ya baadhi ya maeneo tu!

Black Mirror

JF-Expert Member
Oct 17, 2019
833
1,041
Salaam mabibi na mabwana, Salaam Mh Kalemani, salaam Dada Subira Mgalu, Rea na Tanesco
Miaka nenda miaka rudi Tanesco mmejificha kwenye kivuli cha kuwa hamna nguzo ndiyo maana umeme wa REA na Tanesco hausambazwi vitongojini au vijijni km inavyotakuwa. Wateja wa Tanesco pia huambiwa na kucheleweshewa huduma ya kufungiwa umeme kwani mnadai hamna nguzo, si rahisi kusema hamna nyaya wala material nyingine bali mnasema hamna nguzo. Naomba kuelimishwa juu ya hili mana misitu yenye miti ni mingi sana hapa Tanzania lakini mnasema hamna nguzo. Mwanzoni niliamini kuna miti maalumu kwa kazi hiyo ndiyo maana mnasema hamna nguzo, nilistaajabu baada ya kuona nguzo ni miongoni mwa miti ya Karatusi ambayo imetapakaa kila kona ya nchi hii kuliko karibia mti wowote hapa Tanzania. Je, inakuwaje mnaseama hamna nguzo? Je,hizo nguzo mnazosema ninyi zina sifa zipi ambazo huwa vigumu kuzipata kwa wakati?
Ningeomba shirikia hili lije na majibu juu ya kero hii, serikali ilikuja na jambo jema sana la umeme wa REA lakini mpaka sekunde hii kati ya takribani vijiji 12,380 vya nchi hii vingi havina umeme japo inakadriwa ni karibia vijiji elfu 8 vina umeme tayari lakini huu ni umeme wa kwenye makaratasi! Na hii ningetamani Mawaziri, Makatibu na Viongozi wengine wajue hadi ikiwezekana na Mh Rais ajue kuwa umeme unasimikwa tu kwenye maeneo ya shule,zahanati nk sehemu muhimu kwenye kijiji lakini maeneo mengi yanabaki bila umeme. Unakuta kwenye kijiji ni kama 2% tu wanaopata umeme ila 98% wanabaki bila umeme. Ni vijiji vichache sana ambavyo hupata umeme kwa 100% na ukiona hivyo jua kuna msukumo flani nyuma yake. Ningeomba sote kwa pamoja tutafakari haya
1) Kwanini ukosefu wa nguzo umekuwa ni kigezo kikuu cha kusababisha watu wasipewe huduma hii muhimu?
2) Je, ni miti aina gani hutakiwa kwa ajili ya kupata hizo nguzo?
3) Hapa Tanzania hakuna uwezekano wa kupata nguzo hizo kwa urahisi?
4) Wakandarasi huelekezwa kusambaza umeme kwenye maeneo muhimu tu?
5) Kama nguzo za miti imekuwa changamoto hatuwezi kupata mbadala wa nguzo?
6)Kwanini kila mtanzania anayehitaji umeme asifungiwe umeme hata kwa mkopo alafu mkawa na mkataba wa jinsi ya kulipia taratibu?
7)Mbona huwa hatuambiwi hakuna nyaya, au materials nyingine tofauti na nguzo?
8) Mnajua umeme ulivyo nguzo muhimu sana katika kuinua maisha ya kila Mtanzania kuliko karibia kitu chochote?
9)Kama Tanesco inaelemewa kwanini wasitafute wasaidizi wengine?
Mh Kalemani na Mh Mgalu hii kazi ni ngumu kweli lakini jaribuni walau kuwa wazi kwa raia kuliko kuwa mnawapa matumaini hewa juu ya kila raia kupata huduma ya REA.
 
1) Kwanini ukosefu wa nguzo umekuwa ni kigezo kikuu cha kusababisha watu wasipewe huduma hii muhimu?


Kuna jamaa yangu pale Moro anazungushwa nguzo hamna wiki ya nne sasa lakini ukipita pale Msamvu karibu na njiapanda ya mwenda MUM na International School nguzo zinaoza na kuna baadhi ya maeneo wameweka nguzo 2 kwenye umbali wa mita 10, huwa siwaelewi kabisa Tanesco
 
Uhaba uliopo ni wa kutengeneza ili wapige pesa. Amka! Umeme wa REA ni chenga tupu. vijijini wanaweka umeme centre ya kijiji wanasepa. Robo tu ya kijiji ndio inakuwa na umeme
 
Uhaba uliopo ni wa kutengeneza ili wapige pesa. Amka! Umeme wa REA ni chenga tupu. vijijini wanaweka umeme centre ya kijiji wanasepa. Robo tu ya kijiji ndio inakuwa na umeme
Hili jambo linanikera sana, sijui Mh Rais Magufuli asiwamulike hawa watu, yaani ni kero hadi basi sijui wataacha lini. Mimi ningewashauri hili shirika walibinafsishe au watoe umeme kwa mkopo wananchi wafungiwe umeme alafu wawekeane mikataba ya kulipa hizo gharama lakini wasitwambie mambo ya elf 27 kumbe chenga tuu
 
Hii ni kero sugu kwa nchi nzima!
Hata DSM kuna maeneo hayana umeme.
Watu wanaomba huduma lakini hawapewi, wanazungushwa kwa blablaa za hakuna nguzo.

Hawana ubunifu, hili wazo la kufunga umeme kwa mkopo walifanyie kazi haraka. Tena ni rahisi, wanaweza wakaweka system mteja analipa mkopo kila anaponunua umeme kwa kukatwa kiasi kidogo hadi atakapomaliza mkopo.
 
Ni sawa na watu wa Mamlaka za Maji safi, maombi ya wadau kuunganishia maji ni mengi, lakini utasikia Hakuna mita. Ni kero kwa kweli
 
Back
Top Bottom