TANESCO mita zenu mpya zina shida gani? Zinakata umeme wakati upo

Kweli hizi meter mpya zina sense low voltage na kukata umeme automatically ili kulinda vifaa vya umeme visiharibike. Tafadhali Tanesco rekebisheni tatizo la low voltage hasa vijijini ni shida.
Wapangaji wangu wana lala giza kila siku hadi najisikia vibaya maana wamelalamika sana,

mwanzo walihisi ni shida ya umeme kwenye nyumba , nikaita mafundi wakasema shida ya line wakahamisha lakini wapi

Yani imesha kuwa kama desturi kila siku usiku lazima wajiandae kulala giza bila umeme
 
Nilikuwa na tatizo kama hili la kukatika umeme usiku wakati umeme upo, tatizo linaweza kuwa;
1. Low voltage, hata ukiwa na 3 phase, line moja ikiwa na low voltage au haina umeme kabisa basi inazima umeme usiingie tofauti na meter za zamani.
2. Unaweka remote mbali na meter ya LUKU, especially kama una kagorofa, kama meter ipo juu bas na remote ishinde/ilale juu (nadhani kuna mawasiliano zinafanyaga)
 
Back
Top Bottom