TANESCO: Mikoa 11 kukosa umeme kwa masaa 12 tarehe 15 Novemba 2021

Tuna huyu Waziri yeye ni show off tu za kuvaa mashati meupe ya mikono mirefu na kuyakunja hadi usawa wa viwiko kama Barack Obama, hakuna kitu.

Tunahitaji Mawaziri ambao wako down to earth na wanaleta mabadiliko hapo hapo ya upatikani wa nishati, kila kitu tunacho tatizo nini? Kuzurura zurura kwenye nchi za watu na kuomba omba haiwezi kutusaidia.
Dogo anajali muonekano kuliko vitendo
 
Dogo anajali muonekano kuliko vitendo
Acheni wivu 😆
20211114_130721.jpg
 
Mikoa 11 ya Tanzania itakosa umeme kwa saa 12 Novemba 15 mwaka huu kutokana na matengenezo yanayofanywa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Kidatu hadi Iringa.

Umeme utakatika kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 12 jioni ili kupisha matengenezo yanayolenga kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika gridi ya Taifa.

Kutokana na matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Arusha Kilimanjaro na Tanga.

TANESCO imewaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza.


===
MATENGENEZO NJIA YA USAFIRISHAJI UMEME KIDATU-IRINGA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawafahamisha wateja wake kuwa, Jumatatu Novemba 15, 2021 kutakuwa na matengenezo ya njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Kidatu hadi Iringa kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

SABABU: Kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika gridi ya Taifa. Kutokana na matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Arusha, Kilimanjaro na Tanga. Tunawaomba radhi watejawetu kwa usumbufu utakaojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika, toa taarifa dawati la dharura la wilaya kwa msaada zaidi au Kituo cha Miito ya Simu Makao Makuu:+255 222 194 400 na +255 768 985 100

Source:

Kilimanjaro kila siku wanakata umeme tena kutwaaa , tumeanza kuzoea kwa kweli hata kama hawatoi taarifa
 
Tanesco hawana tofauti na Eskom ya South Africa...umeme shida, maji shida , pesa shida na jua limekuwa Kali kweli kweli. Bora tuhamie Mars tu
 
Haijalishi ni kukomoana au ni kutaka kusujudiwa na watu wajione kuwa wao wana umuhimu sana na wameshundikana.

Hii inaendelea kutupa ushahidi tosha kwa kaisi gani Waafrica kudhaurilika na kuonekana hatuna akili.
Ni usibitisho tosha kuwa Africa tuna upungufu mwingi sana akili hasa wasomi na watendaji wetu wote.
Watu wenye akili hawawezi kutufanyia huu upuuzi na kutuharibia mali zetu eti kisa wanavimbishiana misuli.Huo ni upuuzi na ukosefu wa akili ulipitiliza katika Dunia hii ya Teknolojia

Tanesco msihangaike sana zimeni tu umeme tujue tupo bila umeme tutapata tu namna zingjne.La sivyo akili zenu ni za Hovyo kuwahi kutoka kwa 2000AD.
 
Nafikiri jambo kubwa na la busara ni serikali kuacha kufanya biashara ila itengeneze mazingira mazuri ya kuwekeza basi, ukiangalia kila idara ni usumbufu tu, hawajali mali za wananchi wala hasara wanazopata, ikifika mambo ya kudai kodi wanashadadia kweli
 
Msilie lie nyie , Sa ule mzigo wa majenereta utaisha vp bila ya haya magumashi
 
Ni kweli kabisa tunaendelea kukumbuka zile 1.3 Trilioni zilizoyeyuka mbele ya macho ya Prof Assad.... Namshukuru Nape kwa kutaka uchunguzi wa mikopo yootee aliyochukua ufanyike haraka sanaa...
Unaweza ni nionyesha hiyo t 1.3 kwenye ripoti CAG au highlight hiyo paragraph iliyosema t 1.3 ilipigwa.
 
Unaweza ni nionyesha hiyo t 1.3 kwenye ripoti CAG au highlight hiyo paragraph iliyosema t 1.3 ilipigwa.
Katafute mwenyewe hizo kimbukumbu.mtu kakwambia ni kumbukumbu wewe unakazana akuonyeshe.Au kwavile mlificha taarifa ndo maana unashupaza shingo hapa.
 
Back
Top Bottom