TANESCO: Mapendekezo ya ongezeko la bei ya umeme na sababu zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO: Mapendekezo ya ongezeko la bei ya umeme na sababu zake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Dec 28, 2011.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (Ewura) , imesema imekamilisha taratibu zote zinazohitajika za kutangaza bei mpya ya umeme na kwamba sasa inajipanga kufanya hivyo, mwanzoni mwa Januari.

  Ofisa Habari wa Ewura, Titus Kaguo alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa hiyo ni baada ya Bodi ya wakurugenzi kukaa na kupitia hoja za Tanesco na wadau mbalimbali kuhusu suala hilo na kujiridhisha.

  "Bodi ya Wakurugenzi ilikutana Disemba 15 na 16 mwaka huu ili kupitia maombi ya Tanesco na wadau hivyo bodi imeamuru kufanyika kwa uchunguzi ambao utatoa majibu sahihi kwa lengo la kutomuumiza mwananchi na mwekezaji," alisema Kaguo.

  Hatua hiyo inafanyika kufuatia Tanesco kuwasilisha Ewura mapendekezo ya kupandisha gharama za umeme kwa bei ya wastani ya kuuza umeme iliyopo sasa ya Sh141 kwa uniti hadi Sh359 kwa uniti kuanzia Januari mwakani ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 155 ya bei ya sasa.

  Mkurugenzi wa Tanesco, William Mhando alisema sababu ya kutaka kupandisha bei hiyo ya umeme ni kuliwezesha shirika hilo kukabiliana na ongezeko la gharama za uendeshaji ili kuondokana na mgao wa umeme. Aidha, alisema kama bei haitaongezwa Shirika litashindwa kufanya uwekezaji na kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya kuuganisha wateja wapya.

  Hata hivyo wadau mbalimbali wa umeme walipinga hatua hiyo wakisema nyongeza itayumbisha uchumi wa taifa na kulitaka Shirika liimarishe kwanza uzalishaji wa umeme ili liweze kupata faida.

  Wadau hao walisema Tanesco ina hali ngumu ya kifedha kutokana na mgawo na kwamba mkakati uwe ni wa kuongeza uzalishaji ili watu wautumie na hapo ndipo wataweza kujiimarisha na kujikusanyia mapato mengi kuliko njia hii wanayo taka kuitumia ya kupandisha bei.

  Mwananchi 27/12/2011


  Mtazamo wangu

  Suala la Tanesco kupandisha bei ya umeme limekuwa ni desturi na utaratibu wa mara kwa mara pale Tanesco inaposhindwa kujiendesh. Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa mwanzon mwa mwaka huu gharama hizi zilipandishwa kwa sababu za aina hii hii. Pamoja na upandaji huo wa mwanzo, hakuna tija yoyote iliyojitokeza zaidi ya Tanesco kugawa giza na umaskini kwa wananchi. Leo Tanesco inakuja tena na mapendekezo mapya ya kupandisha bei iliyopo kutoka Tsh 141 kwa unit hadi Tsh 359 kwa unit sawa na ongezeko la 155% la bei ya sasa. Nadhan wangetuambia kwanza ni tija gani ilipatikana baada ya kupandisha bei kwa mara ya mwisho. Lakini pia kupandisha bei sio suluhisho pekee la namna ya kumudu gharama za uendeshaji. Waombe ushauri wa kitaalam ili waelekezwe namna ya kupunguza gharama za uendeshaji/uzalishaji na sio kila siku kufkiria kupandisha bei za umeme ndiyo suluhisho pekee. Ninaimani kuwa Tanesco wameshajionea wenyewe kuwa kupandisha bei ya umeme sio suluhisho la kudumu la matatizo ya kifedha yanayowakabili, mimi nadhan kuna mengi ndani ya Tanesco yanayofaa kumulikwa.

  Mkurugenzi anatoa sababu kwamba bei isipopanda Tanesco itashindwa kuunganishia wateja wapya umeme, mimi sidhani kama sababu hii ina mantiki yoyote maana wateja wapya wote wanatozwa gharama za kuunganishiwa umeme, gharama hizi ukilinganisha na nchi nyingine bado zipo juu sana, hivyo nashindwa kuelewa Mkurugenzi anaongelea gharama gani hasa. Lakin pia Tanesco ingejiuliza, nchi nyingine zinapata wapi vifaa vya gharama nafuu vya kuungunisha umeme na yenyewe inapata wapi vifaa vya gharama za juu hadi inatesa wananchi hivi ktk uunganishaj wa umeme. Ukichunguza kwa undani utakuta kuna ufisadi mkubwa katika manunuzi ya vifaa hivi vya umeme.

  Waziri Ngereja alilieleza bunge mikakati iliyopo ya namna ya kumaliza mgao wa umeme tena kwa muda mfupi tu, katika sababu alizozitaja Ngereja, hili la kupandisha gharama za umeme kwa kweli hakulitaja. Je, Mkurugenzi unataka kutuambia kuwa Waziri Ngereja alilidanganya Bunge na umma wa watanzania??iko wapi mikakati ya Ngereja ya kumaliza tatizo hili la mgao kwa muda mfupi???Mimi nadhan Mkurugenzi umepoteza kumbukumbu. Rudi kwa Ngereja kamuulize mikakati aliyoitaja bungeni ya kutatua tatizo la mgao wa umeme akueleze. Naona unataka kutufanya tumeshapoteza kumbukumbu ya alichokiongea waziri Bungeni. Rudi kwenye Hansard za bunge kaone mikakati ya ya Ngereja ya kulimaliza suala la mgao tafadhali, huu ni utani kwa watanzania.

  Hii maana yake ni kwamba ama mikakati aliyoitoa Ngereja Bungeni ni ya uongo au sababu anazozitoa Mkurugenzi katika upandishaji wa bei mpya ya umeme ni za uongo. Mimi nadhani ifike mahala watendaji wababaishaji waone aibu na kujiondoa wenyewe kuliko kila siku kutukosesha amani na utendaji wenu wa kibabaishaji huku wakiendelea kula mishahara inayotokana na kodi zetu. Umeme wenyewe haupo, biashara za watu wengi mmeziingiza matatani still mnataka kututoza bei ya juu. Kama kazi imewashinda please kaeni pembeni muwaachie wengine. Hakuna asiyejua sababu za kupanda kwa gharama za umeme ni ufisadi kupitia mikataba ya kipumbavu mliyoingia na wawekezaji wezi, madudu mfanye nyie tena kwa makusudi mazima halafu gharama mtubebeshe sie!! Jaman muwe na huruma na wananchi hawa. Mishahara yenyewe hii ya Tsh 120,000 nani atamudu gharama za maisha?? au mnataka mbaki wenyewe mjini, tumewakosea nini?? Kwa kweli kwa haya tunayofanyiwa na hii serikali, nadhan 2015 tutajirekebisha, tusameeni kwa kuwarudisha tena madarakani, mana ni kama tuliwalazimisha muendelee kututawala wakati wenyewe mlishajichokea kututawala.

  Je wanaJF mnaona mapendekezo haya ya Tanesco na sababu wanazozitoa ni sahihi??? Nini kifanyike?? Toa maoni yako.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Tanesco perse siyo tatizo matatizo ya Tanesco yanapikwa kuanzia Ikulu kwa kuwaingilia na wkuwachagulia viongozi bomu kama yule Idrissa.............Rashid
   
 3. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ungeelezea ubovu wake kiundani zaidi.... na utofautishe na let's say...Mosha or whoever you think was better'.

  Kusema mtu fulani ni mbovu, bila kutoa sababu ni sawa na kumeza sabuni ili utumbo uwe msafi.
   
 4. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Dawa yao kuwahukumu barabarani kama vibaka wengine waishi humo humo makazini mwao si wenzetu hawa
   
 5. Mangandula

  Mangandula Senior Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Tanesco wanasema watashindwa kuwafungia wateja wapya! Mbona mpaka sasa wateja wananunua nguzo wenyewe na hizo nguzo zinakuwa mali yao tanesco! Mimi nadhani Tanesco waangalie mbinu mpya ya kutoa huduma huko wanakokimbilia kupandisha bei bidhaa nyingi sana zitapanda bei.

  Pia serikali iangalie jinsi ya kuacha uwanja huru wa ushindani ili tanesco wajifie wenyewe kama TTCL maana kama kwa wateja hawa wachache walio nao wamechemsha je watanzania wote mil 40 wakitaka hiyo huduma siwatapandisha mpaka asilimia10000! Tanesco kaeni mukaangalia namna nyingine lakini sio hii mnayoileta kila mwaka.
   
 6. a

  adobe JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Ewura wametangaza rasmi kwaqmba liwalo na liwe lazima tanesco watapandisha bei ya umeme,je ewura wako kwa maslahi zaidi ya tanesco au kwa maslahi ya watumiaji wa nishati hiyo?Nakumbuka wakati wanapandisha bei mwaka jana Ewura waliwapa Tanesco masharti mojawapo likiwa ni kuhakikisha wafanyakazi wa Tanesco nao wanalipa bili kawa watumiaji wengine,Je, Ewura wanatuambiaje kuhusu hilo kwa kuwa Tanesco hawakulitekeleza hilo sharti.???????????????

  Kwako mkurugenzi wa tanesco umekuwa unalalamika sana shirika kujiendesha kwa hasara we huoni hwasara mnajitia wenyewe kwa kupeana unit 700 bure kila mwezi wakati sie tukiwachangieni? Tunaomba ufafanuzi.

  Tunaomba Ewura imuombe CAG afanye special audit kujua kama agizo hilo lao lilifanyiwa kazi au la na walohusika wachukuliwe hatua kali za kisheria
  NA JK AINGILIE KATI WANANCHI TUNAPATA TABU UMEME UNAPOPANDA KILA KITU JUUUU
   
 7. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  tulichagua rais legelege sasa naye kawaweka jamaa zake legelege patamu hapo, priorities zake anaweka kwenye sherehe na mapumziko wakati kuna crisis za hikes ya bei ya mafuta kuna inflation double digit, tunatumia notes za aina mbili for almost a year lakini this ndulu guy promised watakuwa wametoa kwenye mzunguko hela za zamani within 3/6? Months.

  Urais is not just because you have the dream and uko ktk right position at the right time but in your head ni hopeless, sloppy you are killing us m"k"were! Hey all these problems start from top before coming down I put all the blames to that guy in magogoni.
   
 8. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Najua Tanesco kupandisha umeme kunaathari kubwa sana kwa serikali yake maana watumiaji wakubwa wa umeme ni maofisi ya serikali hivyo nahisi zoezi hilo litaongeza madeni yake tu.

  Hoja tuone another new movie kwa kipindi cha miezi sita jinsi ukosefu wa ajira utavyoongezeka na mfumko wa bei utavyoshoot!!!!!!
   
 9. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  TANZANIA NI ZAIDI YA UIJUAVYO, HAPO KUNA HOJA ITAKUWA INATAKA KUZIMWA. Tz ni mwendo wa matukio kuzima tukio jingine!
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  acha wakusanye pesa za kuwalipa dowans
   
 11. I

  Issa.Hamis New Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanesco ni wababaishaji. Wameingia Mikataba a-ghali ya kununua umeme kutoka makampuni tapeli sasa wanataka kutubebesha Mzigo.
  Inabidi watanzania tuamke, tusibebeshwe mizigo kizembe-zembe.
   
 12. Kinyengeli

  Kinyengeli JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika wakurugenzi bora kabisa waliowahi kuwa Tanesco Dr Idrisa anaweza kuwa the best!!! Uliza wafanyakazi wa Tanesco na wateja hasa wale wakubwa. Ni wakati gani huduma na maslahi ya wafanyakazi yameboreshwa na stability ya shirika katika kujiendesha. Alipokea Tanesco kutoka kwa Net Group Unsolution ikiwa hoi kimiundombinu, kulikuwa hakuna Meters kwa ujumla vifaa vya kuunganishia wateja wapya, mteja alikuwa analipia gharama za kuunganishiwa umeme lkn anasubiri hata miaka miwili. Net Group kazi yao ilikuwa kukusanya tu mapato. Dr alikuwa Funga kazi bwana!!!
   
 13. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  waongeze tu hiyo bei ili tuheshimiane na wapiga kura!
   
Loading...