Tanesco + luku = ufisadi au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco + luku = ufisadi au?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sabode, Mar 29, 2011.

 1. Sabode

  Sabode Senior Member

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ndugu wanajamvi nina suala naomba kuwasilisha juu ya jambo ambalo limenikera kabisa kuhusu tanesco na huu utaratibu wa kutumia mita za luku. Hapo awali nilitaraji kuwa ungekuwa utaratibu muafaka kuondoa kero na misongamano ya kuwalazimisha tanesco kukusanya pesa kulipia umeme ambao walitusambazia nasi tukautumia. Linanalo nikera ni kuwa kuna rafiki yangu mmoja ambaye nilimuona kuwa ni mhangaikaji wa ukweli na mwenye nia ya ukweli ya kujiondoa katika umasikini, jamaa yangu huyu huku akiwa mfanya kazi wa kawaida kabisa kama mimi lakini amepiga hatua kubwa kimaisha kuliko mimi (nakubari hilo na nimejifunza toka kwake) huku akiwa na kipato kidogo zaidi ya changu, kwa kutumia kidogo akipatacho mshikaji aliamua kujinunulia kaploti akatafuta fundi na ramani akachimba msingi yeye mwenyewe na kwa mikono yake mwenyewe na maelekezo ya fundi ambaye ni mshikaji wetu pia kwa malipo ya kishikaji alifanikiwa kujenga kibanda chake. japo kidogo lakini kimekaa mkao wa maana sana. Akapalangana zaidi mara umeme ndani, kwa kuwa alikuwa amebakiwa na kauchache kidogo akaamua kuondoa udhia wa kukatikiwa na units za umeme ndani kipindi kifupi hivyo akanunua za kutosha ambazo zilimsukuma kwa miezi kaa minne hivi. zilipo kata bila yeye kukumbuka aliamua kujaza wa elfu kumi kufika kwenye kununua akakuta anadaiwa cjui charges gani hizo ambazo ni za miezi ambayo alikuwa bado anatumia unit ambazo alinunua hapo awali na hvyo buku kumi yake ilikuwa ni ya kulipia madeni tu na bado anadaiwa.

  Sasa wanajamvi hii ishu mi naona ni kero kabisa kwa nini wasiweke utaratibu wa ulipe hayo mauvundo yao pale unapolipia, vipi kama ukisafiri miezi tisa ukafunga nyumba si unaweza kukuta deni la millioni hapa? Anyway kwa kifupi sijaelewa haka kautapeli kamekaa vipi anaye fahamu hebu anifafanulie vema maana naona hapa panaweza kuwa mrija mwengine wa kifisadi.

  Nawasilisha hoja.
   
 2. Sabode

  Sabode Senior Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mchango wa mawazo elimu au chochote au haliwagusi hili jamani mi nadhani tanesco wana tuhujumu hapa au mnasemaje wanajamvi?
   
 3. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hawa Tanesco ulikuwa huwajui?
  Kero zao ni nyingi sana, bora hiyo yako ndogo. Kuna mita zengine Unit zinakwenda kwa spidi ya ajabu hata kama umezima kila kitu. Nchi hii hatuna wa kututetea
   
 4. Sabode

  Sabode Senior Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Du ni kweli mkuu maana nasikia kutapika cku hiz kila ninaposikia tanesco na umeme uso kuwepo kanchi haka kamevundaaaa!! inabidi kakaushwe kwa dawa kali sana.
   
Loading...