Tanesco: Limeanzishwa mwaka 1903 lakini huduma asilimia 17 tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco: Limeanzishwa mwaka 1903 lakini huduma asilimia 17 tu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kilimasera, Jan 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  LICHA ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kuwa na historia ndefu iliyopitia mabadiliko mbalimbali ya kiutawala na kimfumo, bado ukongwe wake wa miaka 107 hauendani na kasi kubwa ya ukuaji wa mahitaji ya nishati hiyo nchini.

  Kumbukumbu zinaonyesha kuwa tangu kuanzishwa kwa shirika hilo mwaka 1903 mpaka sasa ni asilimia 17 tu ya Watanzania wote zaidi ya milioni 42 ndiyo waliofikiwa na huduma hiyo. Kati ya hao asilimia 15 ni ya wakazi wa mijini na asilimia mbili iliyosalia ni wakazi wa vijijini.

  Maendeleo ya nchi yoyote ile duniani hutegemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa nishati ya umeme katika endesha mitambo viwandani na kwa matumizi mbalimbali majumbani na ofisini.

  Umeme huvutia uwekezaji, huhifadhidhi mazingira, huongeza kipato na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, hurahisisha mawasiliano, upatikanaji wa huduma muhimu na ukuaji wa miji na faida nyingine nyingi.

  Kutokana na umuhimu huo basi ni wazi kwamba bila ya umeme hakuna huduma muhimu na bila huduma muhimu hakuna maendeleo ya kweli. Ili Tanzania iweze kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG) hasa lile la kupunguza umaskini ifikapo mwaka 2025, ni lazima kuweka mkazo katika utoaji wa huduma hiyo hususan vijijini ambako asilimia 80 ya Watanzania wanaishi.

  Tanesco limebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha kuwa nishati hiyo muhimu inasambazwa nchini kote na mchango wake unasaidia kutimiza malengo hayo. Hata hivyo, viongozi wake wamekuwa wakilalamika kukabiliwa na changamoto nyingi hivyo kukwamisha mwendo kasi wake wa utoaji wa huduma ya umeme.

  Changamoto hizo ni pamoja na ukata, ukame katika mitambo inayotumia nguvu za maji huku mingine ikiwa imechakaa na kuharibika mara kwa mara.

  Nyingine ni gharama kubwa za kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme wa mafuta hasa katika Mikoa ya Kigoma, Ruvuma, Rukwa na Wilaya za Masasi, Mafia, Biharamulo na Ngara. Pia kuweko kwa hujuma kwenye miundombinu na kusababisha kero kubwa kwa wateja.

  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, William Mhando anasema licha ya kuweko kwa changamoto hizo, limeanza kuweka mikakati mbalimbali kuboresha na kupanua huduma kwa wananchi. Hiyo ni pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato hadi kufikia wastani wa asilimia 10 kila mwezi.

  Mwingine ni kuongeza usambazaji umeme katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuunganisha wateja 50,000 hadi kufikia Oktoba mwaka huu. Kuweka mitambo ya kuzalisha umeme huko Kibondo, Kasulu, Kigoma na Sumbawanga na kwa ufadhili wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

  Anasema Tanesco limekusanya asilimia 7.3 tu ya deni lake la Sh 300 bilioni kutoka kwa wateja na kiasi kilichosalia kwa sasa ni Sh 278 bilioni. Wadaiwa wakubwa wa Tanesco ni serikali na taasisi zake.

  Anasema serikali imeongeza uwezo wa shirika wa uzalishaji umeme kwa gesi ya asili huko Mtwara 300 MW, Kinyerezi 240MW, Ubungo 100MW na umeme wa mafuta wa 60MW huko Mwanza. Pia jitihada zinaendelea za upatikana wa umeme wa makaa ya mawe, Kiwira na umeme wa nguvu za maji Ruhudji.

  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo anasema mpaka sasa ni asilimia 15 tu ya Watanzania waishio mijini na asilimia mbili vijijini wanaopata umeme kati ya Watanzania zaidi ya milioni 40. Anasema hali hiyo inaonyesha wazi kuwa shirika hilo linakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inawafikia watu wengi.

  Anasema mpango wa shirika wa kuunganisha watu 100,000 kwa mwaka bado ni mdogo hasa ikilinganishwa na mahitaji makubwa ya yaliyopo.

  Pengine kushindwa kupanuka kwa kasi kwa huduma za shirika hilo kumekwazwa na mchakato mzito ambao limepitia tangu lilipoanzishwa mwaka 1903 wakati Tanzania Bara ikijulikana kama Tanganyika chini ya utawala wa kikoloni wa Kijerumani.

  Katibu mkuu huyo analitaka kujiimarisha kifedha, kutafuta suluhisho la miundombinu kuzidiwa uwezo, kasi ndogo ya kupeleka umeme vijijini, kuimarisha huduma kwa wateja, kujenga ushirikiano na wawekezaji, kujenga ushirikiano na sekta binafsi na viongozi kuwa wabunifu na wawajibikaji.
   
 2. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha!Siasa imetawala maamuzi yetu na tumeshindwa kuwa na vipao mbele.Viongozi wetu tunaowachagua kuingia madarakani wameshindwa kusimamia mambo ya msingi kwa taifa.Mara nyingi wanafikiri wanaweza kutatua matatizo yote kwenye kipindi cha uongozi.

  Kwa mfano kama mkwere alipoingia aliahidi kumaliza tatizo la.umeme lakini kumbe mpango mzima ulikiwa kutumia nafasi ya hiyo kujineemesha kupitia Richmond/Dowans.Tumekosa viongozi ambao wangependa kucha kumbukumbu fulani kwa wananchi.Mara kiongozi anapomaliza muda wake ingebidi tuweze kuona hata kitu kimoja kukibwa cha kukumbuka lakini tunachoona na vitu ambavyo vinafanywa juu juu tu.

  Watakwambia wamejenga University of Dodoma...upuuzi mtu!Hardly a decade toka kianzishwe migomo na lawama zidi ya serikali.So hakuna kikubwa wanachofanya ni kugusagusa kila kitu!
   
 3. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Data nzuri sana hizi. Je mahitaji ya Tanzania ni kiasi gani in MW na shirika lenyewe linatumia kiasi gani (TSH) kila mwezi katika kutimiza shughuli zake? Idadi ya wafanyakazi? Mipango iliyopo kuongeza ufuaji umeme?
  Lini (Kikazi kipi tangu sasa) wataweza kuwa na uhakika wa kupata umeme bila matatizo yasiyo ya msingi?
   
 4. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tatizo la Tanesco urasimu na rushwa vimewazidi. wanapenda sana rushwa sana sana waliopo mikoani. There is no way wataweza kusanya pesa zote hizo kwavile waliopo kwenye system niwabovu. Kwanza wanafanyakazi wa Tanesco shida yako nimradi kwao nikama police tu.
  Mikataba hawaielewi at the end of the day wanajikuta matatizoni.
   
 5. K

  Koba JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Kuendelea kufikiri TANESCO watasaidia kumaliza tatizo la umeme na kuipa monopoly TANESCO ni sawa kama mpaka leo tungekuwa na monopoly ya KAMATA,Natonal housing au TTCL,tatizo la umeme TZ ukiangalia vizuri lipo kwenye policy zetu ambazo zinaipa TANESCO monopoly na kuwafanya serious investors kushindwa kuwekeza capital zao kumaliza tatizo,TZ kuna kila source ya energy ya kumaliza hili tatizo na demand ni kubwa sana lakini upuuzi wa politician wetu na IQ ndogo ndio maana wananchi wana suffer na umaskini unaongezeka tuu...time ya kuweka policy mpya kabisa kumaliza hili tatizo sio blah blah za kila siku na story za kina JK na wenzake
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nyerere aliikuta Tanesco inauza umeme mpaka Kenya. Lakini duhh, jamaa lilivyoboronga kwenye uchumi? Limeuwa kila kitu, mpaka anang'atuka kaiacha nchi hohehahe, hakuna kinachofanya kazi.
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  siasa zinalimaliza shirika hili
   
Loading...