TANESCO, kwanini anayetumia umeme mwingi alipe kwa kiwango cha juu?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,870
7,752
Hivi inakuaje kuhusu viwango vinavyotozwa na tanesco anayenunua umeme mkubwa atozwe bei juu. Hebu wajuzi watueleze mbona biashara zote anayenunua bidhaa kwa wingi anapunguziwa bei ila kwa tanesco ndio bei inaongezeka. Hivi hao wanaoitwa watumiaji wa units 75 kwa mwezi ni nani na ni wangapi. Ukichunguza utaona tanesco wala ilikua haijampa unafuu mtu wa kawaida.
 
hapa nadhani kuna haja ya waziri husika kuja na suluhisho la jipu hili.

Namwamini sana ndugu Sospeter ni mtu makini sana aliangalie jambo hili, ikizingatia kwamba kwa sasa shirika linazalisha umeme kutumia ges kwa gharama nafuu.

Hivyo ni vyema sasa watanzania wakaanza kufaidi matunda ya rathilimali zao kwa kupatiwa nafuu ya huduma.
 
Hii ipo kwa ajili ya kumsaidia maananchi wa hali ya chini awe na uwezo wa kutumia umeme, kwa nchi za wenzetu kuna bei kufuatana na maeneo, watu wa suburbs, wanalipa bei juu kuliko watu wa CBD, na watu CBD wanalipa bei juu kuliko watu wa townships, na watu townships wanalipa bei juu kuliko watu wa rural areas. Hivyo inafanya mtu mwenye kupato cha chini kumudu kutumia umeme. Ila kwetu umeme ni anasa, sio nishati ambayo inafanya huyu mwanakijiji ambaye anapigiwa kelele na wanamazingira kuto kata miti ovyo. Atashindwa vipi kukata miti wakati nishati ya umeme ipo juu? naunga mkono zuio la kupandisha umeme, wananchi masikini wanatakiwa kupunguziwa ghalama za nishati umeme/gesi ili waweze kununua.
 
Hivi inakuaje kuhusu viwango vinavyotozwa na tanesco anayenunua umeme mkubwa atozwe bei juu. Hebu wajuzi watueleze mbona biashara zote anayenunua bidhaa kwa wingi anapunguziwa bei ila kwa tanesco ndio bei inaongezeka. Hivi hao wanaoitwa watumiaji wa units 75 kwa mwezi ni nani na ni wangapi. Ukichunguza utaona tanesco wala ilikua haijampa unafuu mtu wa kawaida.
Halafu pia ukiangalia mpangilio wao ni wa wizi. Watumiaji umeme wa majumbani ukitoa wale wa unit 75 wengi hatutumii zaidi ya unit 500 lakini kundi hili limechanganywa na wenye viwanda wanao tumia hadi unit7500 kwanini zisigawanywe hizi category kutoka majumbani na wenye viwanda?
Tanesco wamekaa kiwi wizi na UWURA wanaangalia huu wizi na kujifanya hawaoni.
 
LESkufuatana : 19114863 said:

Isingeweza kuchanganywa kange kuwa na utaratibu mzuri wa ugawanyo wa masikini, mteja wa wajumbani hazalishi, atalipa vipi sawa na wenye kiwanda? Tanesco wangefanya kwa mfano,1-75units, 75-200units, 200-500units, 500-1000units and up 1000units kwa mchanganuo juu mtu atalipa umeme kadiri atumiavyo, kwa 75units ni sawa na huyu mtu anatumia taa, radio, TV na fan tu! Ila kama huyu mtu itakapotaka kutumia jiko la umeme nina uhakika units 75 zitazidi. Hivyo kufanya nishati ya umeme kuwa ya anasa. Umeme utachangia kuleta maendeleo kwa haraka miji midogo na vijijini kama ukifanywa ni nishati mbadala wa kuni na sio nishati ya anasa. Sometimes roho inaniuma Sana ninapoona nchi za wenzetu mwanakijiji masikini wanauwezo wa kumudu kulipia umeme, na hii inatokana na serikali kumjali kutokana inajua huyu mwanakijiji kipato ni midogo.p
 
Halafu pia ukiangalia mpangilio wao ni wa wizi. Watumiaji umeme wa majumbani ukitoa wale wa unit 75 wengi hatutumii zaidi ya unit 500 lakini kundi hili limechanganywa na wenye viwanda wanao tumia hadi unit7500 kwanini zisigawanywe hizi category kutoka majumbani na wenye viwanda?
Tanesco wamekaa kiwi wizi na UWURA wanaangalia huu wizi na kujifanya hawaoni.
yes, kati ya hizo units 75 na 500 ndio wengi residential na ndio wamewekwa kundi la viwanda. hawa wa units 75 ni bulbs 3 bila fridge etc. Nakubaliana na wewe ni viwango vya kijanjajanja kuload kwa wananchi gharama za upigaji dili na ubadhirifu tanesco. Suluhu ya tanesco iko kwenye kupunguza gharama. Kama board na management hawataki watumbuliwe. Mbona tumbuatumbua hatimae imezaa matunda bandarini.
 
Watu wanaotumia units 75 ni wale waliopanga nyumba nzima na anatumia radio, tv na fan lakini huku uswahilini tumepanga chumba kimoja na nyumba inawapangaji 20 kila mpangaji na chumba chake sasa hizo units 75 hazitoshi kutokana na ukubwa wa nyumba na idadi ya wapangaji ingawa ndiyo masikini wanaotakiwa kusaidiwa
 
Nilikua mtumiaji mdogo siku hiyo nikapata hela ya kununua Umeme ili nikae angalau mwezi Na nusu lol ni kaamishiwa tariff ingine,sasa Ni mtumiaji mkubwA Kwa sababu tu nilinunua Umeme wa 30000.
 
Back
Top Bottom