TANESCO kutoa mikataba ya uunganishaji umeme kwa makampuni binafsi

Wawe makini tu na quality ya kazi, umeme na porojo ni kuleta majanga, Tz ajali za moto sababu ya miundombinu ya Tanaesco ni chache, hivyo privatizations isitumike kama uchochoro wa kupunguza ubora.
Nani kasema hiyo ni privatization?
 
Unasema hapa tulipo hakuna unafuu, Sasa Kama hakuna unafuu hao subcontractors watasimamiwaje?
Hao hawapo independent, kila kitu kinabaki kuwa chini ya tanesco
Ndio maana nikasema tusubiri tuone watapewa kazi za aina gani.

Kwa mfano, Tanesco inaweza ikaweka utaratibu wa kampuni kupewa leseni cha kuwa "Muunganisha Umeme" na hayo makampuni yakawa yanajulikana. Mwananchi unapewa gharama za kuunganisha umeme unachagua kampuni, inapewa mkataba wa kufanya hiyo kazi kwa siku kadhaa. Ikishindwa kufikia ufanisi wa kiasi fulani inapokonywa hiyo kazi; na hakuna malipo bila kazi kukamilika.

Kwa uzoefu wangu, makampuni binafsi yanafanya kazi vizuri kuliko serikali. Leo hii nyumba ikiwaka moto, piga simu kampuni binafsi na serikali uone tofauti yake. Au nenda kampuni binafsi za internet, walipe pesa yako halafu uone inachukua muda kukuletea internet nyumbani kwako.

Nadhani ni hatua nzuri kwa Tanesco kukiri kwamba zoezi limewashinda, wanataka msaada; private sector ikishindwa; basi tukubali kwamba imeshindikana mazima.
 
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema linatarajia kuanza kuzipa kandarasi kampuni binafsi kazi ya kuunganisha umeme, ili lenyewe lijikite kwenye uzalishaji na usafirishaji wa nishati hiyo muhimu.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Maharage Chande wakati wa mkutano wa Tanesco na wadau uliofanyika juzi jijini hapa na kusema hatua hiyo na nyingize zitasaidia kumaliza tatizo la watu kuchelewa kuunganishiwa umeme.

“Watakaopewa kazi ya kuunganisha umeme watalipwa kwa ‘commission’ kulingana na kazi itakayofanywa na tutakuwa tunafuatilia na kubaini iwapo kutakuwa na ucheleweshaji na kuchukua hatua. Lengo ni kumaliza changamoto ya kuchelewa kuunganisha umeme,” alisema Chande bila kufafanua lini hasa wataanza.

Hata hivyo, Chande alisema wameanza majaribio na pindi wakapoanza rasmi suala la kuunganishwa umeme litakuwa si shida tena, kwani urasimu utapungua.

“Pamoja na kwamba tunaendelea na hilo kwa utaratibu huu wa sasa tunatarajia walioomba kuunganishiwa umeme wote wataunganishwa ndani ya miezi sita ijayo,” alisema.


Chanzo: Mwananchi
Makamba kashaanzisha kikampuni chake cha upigaji...
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom