TANESCO kupinga malipo ya DOWANS mahakamani

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Monday, 10 October 2011 20:28
Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), leo litawasilisha katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ombi la kutaka kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuilipa Dowans Holidings.

Uamuzi wa kuilipa Dowans uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kupata baraka za Mahakama Kuu chini ya Jaji Emilian Mushi.

Mahakama Kuu iliridhia tuzo ya ICC hivi karibuni ya malipo ya fidia ya fedha kwa Dowans ambayo inaitaka Tanesco kulipa kiasi cha Sh111 bilioni kwa kuvunja mkataba wake na kampuni hiyo. Awali, Tanesco ilikuwa ikidaiwa Sh94 bilioni lakini baada ya kukata rufaa na kushindwa deni hilo liliongezeka riba ya asilimia 7.5.

ICC iliamuru Tanesco kuilipa Dowans Holdings SA(Costa Rica) na Dowans Tanzania kutokana na kukatisha mkataba wa uzalishaji wa umeme kati ya pande hizo mbili mwaka 2008.

Mmoja wa kundi la wanasheria wa Serikali anayeshughulikia suala hilo, Dk Eve-Hawa Sinare alisema jana kuwa ombi hilo la kutaka kukata rufaa litafuatana na ombi jingine la rufaa ya kutaka kuzuia uamuzi wa malipo hayo usitekelezwe kwanza kabla ombi hilo kusikilizwa.

Dk Sinare ambaye pia ni mmoja mawakili katika kampuni ya Rex Attoneys alisema hutua itakayofuata baada ya ombi hilo ni kuomba nakala halisi za mwenendo wa kesi hiyo, hukumu na tuzo iliyotolewa kwa ajili ya kukata rufaa waliyokusudia katika Mahakama ya Rufani.

Alisema kuwa Tanesco walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu kwa sababu waliamini kuwa mahakama hiyo haikuangalia mambo muhimu na yenye utata kisheria katika kesi hiyo yenye manufaa ya umma


Source:
http://www.mwananchi.co.tz/habari/4...9-tanesco-kupinga-malipo-ya-dowans-mahakamani
 
dont expect any changes: guyz we should think fully on how we and our gonna survival in this complicated and vagabond contry.
 
Hawa wote ni wezi tu.
Mwanzo ilikuwa 94bln sasa imefika 111bln, wamepanga wazidi kuchelewesha malipo ili pesa iongezeke.

Walipeni, ili tugange yajayo.
 
Itachukua muda mrefu sana hadi sinema ya Dowans ifike mwisho. Mitambo wameuza na bado tutawalipa 111 billions
 
wanaendellea kuwapa pesa hao mafisadi rex attorney??malipo ya dowans hayawezi kusimamishwa mahakamani bali kwa maandamano ya nchi nzima ambayo ofcourse yanaratibiwa na CDM,...maboss wa tanesco,ngeleja,rex attorneys lao moja...kutaka deni lizidi kuwa kubwa..mafisadi
 
hili zigo tulilipe tu yaishe, kadri tunavyochelewa ndiyo charges zinapanda - ki-sheria lazima tulipe, tumeshaingizwa mkenge watanzania, we have to pay it now way out.
 
Ili yote haya yasitokee TZ,inabidi wananchi tujivue gamba, bila hvyo,hawa akina J. K. KIKWETE,ROSTAM,LOWASSA, wataendelea kutupeleka peleka mpaka tuje kujitambua,tutakuwa tumeshafirisiwa kabisaa,heri ya Mkapa mara kumi ingawa nae simuungi mkono kwa kujenga hotel ya nyota 5 south africa, pia kuiba kinyago cha dhahabu ikulu. Kenge hawa wa blue dowans wasilipwe kwa nguvu zote bhana, nao Tanesco wanapinga nini,kwanini walivunja mkataba wakati muda ulikuwa umebaki mdogo kama si kutafutiana michuzi tu. It was planned, peoples let us stop fraud Tz,its possible, it beggin with u.
 
lakini jamani mnakumbuka dowans ilikuwa bungeni mnawakumbuka kabisa waliokuwa kipaumbele mkataba uvunjwe kwamba hela wanalipwa bure hatakama umeme auzalishwi nakumbuka wabunge fulani waliongoza kupinga malipo hayo walisifiwa sana kwa kusababisha mkataba kuvunjwa hatima mahakama imeingilia kati walipwe kutokana na kuvunjwa mkataba nahao wabunge kana kwamba si wasomi hawajui sheria za mikataba kama ikivunjwa hasara anabeba mzigo nani, leo wabunge wale waliosababisha mkataba uvunjwe wamegeuka wamekuwa ndio vipaumbele wakupinga malipo ya dowans. Jamani msituyumbishe kana kwamba wa tz mambumbu. Tunakumbuka sana sasa hata tukipinga hatimae deni litaongezeka kumbukeni ile ni mahakama. Basi tuamue kupindisha sheria tutumie nguvu kama madikteta natuseme wazi kwa umoja wa mataifa hatulipi na hatuhitaji kushirikiana na umoja wa mataifa na mahakama yenu kwamba ni onevu inatuonea lifanyike hilo tujue moja basi.
 
Hata wakikata rufaa haimaanishi kuwa deni halitolipwa. Kukata rufaa ya kupitia vipengele vya sheria ambavyo wanahisi havikupitiwa, hakuto "reverse" maamuzi ya ICC. Labda itaamuliwa Serikali ilipe badala ya Tanesco. That's all.

Ni njia tu za a) kujaribu kurushiana mpira ni nani alipe b) kutafuta kujikosha mawakili.

Hakuna mahakama duniani ityoamuru Dowans wasilipwe, mitambo walileta na imefungwa na imefanya kazi, na inaendelea kufanya kazi. Kwa nini wasilipwe?

Watanzania wanaoshikilia kuwa Dowans isilipwe au labda ni wavivu wa kufikiri au ni wezi.
 
Hata wakikata rufaa haimaanishi kuwa deni halitolipwa. Kukata rufaa ya kupitia vipengele vya sheria ambavyo wanahisi havikupitiwa, hakuto "reverse" maamuzi ya ICC. Labda itaamuliwa Serikali ilipe badala ya Tanesco. That's all.

Ni njia tu za a) kujaribu kurushiana mpira ni nani alipe b) kutafuta kujikosha mawakili.

Hakuna mahakama duniani ityoamuru Dowans wasilipwe, mitambo walileta na imefungwa na imefanya kazi, na inaendelea kufanya kazi. Kwa nini wasilipwe?

Watanzania wanaoshikilia kuwa Dowans isilipwe au labda ni wavivu wa kufikiri au ni wezi.

bingwa wa kukurupuka na mtu anayejifanya much-know.
 
serikali iwabadili rex au itumie watu wawachunguze kuna mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wahindi awa na wamiliki wa dowans wanachofanya ni kula dili na dowans ili kuongeza riba ya deni wahindi ni watu wenye tamaa sana

kwani serikali imeshindwa kutumia mawakili wengine? cha msingi kiundwe kikosi maalum cha kuwafilisi mali waliohusika ili wawalipe dowans
 
Gov haiwezi kufanya maamuzi magumu walioingia mikataba ndio walipe
 
Lakini mawakili hawa ndiyo waliopinga wanaharakati kuingia kwenye kesi wakidai hawahusiki na kesi kwa hiyo wasiingie katika kesi hiyo.
 
Back
Top Bottom