TANESCO: Kupanda bei ya umeme hakutaathiri wateja wa kawaida

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939

Shirika la umeme nchini TANESCO limesema halina mpango wa kupandisha bei za umeme kwa watumiaji wadogo na badala yake mpango huo upo kwa watumiaji wakubwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema kuwa hakuna haja ya wananchi kuwa na wasiwasi kuhusu mapendekezo yaliyo wasilishwa na mamlaka ya udhibiti wa huduma Za nishati na maji EWURA.

“Niwatoe hofu wananchi kwamba yale mapendekezo tuliyoyapeleka wananchi wa kawaida wale wanaotumia umeme mdogo bei zao hazitaathirika sana. Kuna jambo moja ambalo tumelitazama kwa mtazamo tofauti, unajua sasa hivi we mteja wa kawaida unalipa sawasawa na kampuni zinazoweka mabango barabarani ambazo ni kampuni za kibiashara,” alisema Mramba.

“Sasa katika mapendekezo tuliyopeleka EWURA tulikuwa tunamuomba aangalie kwamba yale makampuni yanayofanya biashara za mabango ya matangazo yasilipe sawasawa na mteja wa nyumbani bei yake iende juu zaidi.”
 
Asitaje tu mabango ya barabarani bali hata makampuni yanayozalisha bidhaa mbalimbali.Kama akipandisha umeme kwa makampuni ambayo vilevile ndio yanaweka mabango barabarani hii ina maana gharama za uzalishaji zitaongezeka hivyo bei ya bidhaa itaongezeka.Hii maana yake ugumu wa maisha utaongezeka hasa kwa sisi ambao anasema hatatuongezea bei ya umeme.
 
Makampuni wapewe mita zao tofauti na hizi za Wananchi wa kawaida vinginevyo huo wote ni usanii tu
 
hao ndio wasomi wetu wa TZ, ukimpandishia gharama za umeme bakharesa si atapandisha bei ya sembe, mtu wa chini si atazidi kuumia? Hivi akina muhongo si walituahidi tanesco wakianza kutumia gas umeme utashuka sn bei? kweli wa tz tumelaaniwa
Great vission Gombea Urais 2020.
 
Shirika la umeme nchini TANESCO limesema halina mpango wa kupandisha bei za umeme kwa watumiaji wadogo na badala yake mpango huo upo kwa watumiaji wakubwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema kuwa hakuna haja ya wananchi kuwa na wasiwasi kuhusu mapendekezo yaliyo wasilishwa na mamlaka ya udhibiti wa huduma Za nishati na maji EWURA.

“Niwatoe hofu wananchi kwamba yale mapendekezo tuliyoyapeleka wananchi wa kawaida wale wanaotumia umeme mdogo bei zao hazitaathirika sana. Kuna jambo moja ambalo tumelitazama kwa mtazamo tofauti, unajua sasa hivi we mteja wa kawaida unalipa sawasawa na kampuni zinazoweka mabango barabarani ambazo ni kampuni za kibiashara,” alisema Mramba.

“Sasa katika mapendekezo tuliyopeleka EWURA tulikuwa tunamuomba aangalie kwamba yale makampuni yanayofanya biashara za mabango ya matangazo yasilipe sawasawa na mteja wa nyumbani bei yake iende juu zaidi.”
Huyu mkurugenzi wa TANESCO katuona watanzania ni mapoyoyo na tusiosoma na kwa ujinga wetu tumeanza kukubali kuwa ombi lao kwa EWURA halijahusisha bei kupanda kwa wateja wa majumbani huo ni uongo mkubwa. Ni kweli kuwa wametenganisha watumiaji wa kawaida na watumiaji wa umeme wa minara na mabango ya tangazo kwa kutengeneza tariff class mbili yaani T1 na T1b kutoka iliyokuwa T1, lakini bei za umeme zimeombwa kupandishwa kwa tariff zote yaani D1,T1,T1b,T2 na T3 kwa asilimia tofauti tofauti. kwa maelezo Zaidi angalia attachment niliyoiweka.
 
Attachments

  • TANESCO%20Tariff%20Adjustment%20Application%20for%20year%202017.pdf
    1.6 MB · Views: 69
Wamei miss service charge hawa hamna lolote unataka upandishe umeme umnufaishe nani? Wakati huyo unaye mpandishia na yeye anajua kwa kwenda kufidia ambaye ni Mwananchi? Yaani wasomi wetu sijui pombe,vyakula wanavyo kula vinawatoa ufahamu yaani sijui kama tutafika.Ivi kweli kuna watu au taasisi ya kumshauri mtu wa mawinguni au wote ni vilaza?
 
shida ubinafsi ndo utatuangamiza watu weusi,,,hata kwenye mwendosi utakuta mtu kajitanua kama mbuzi inazaa mlangoni watu wanapumuliana mdomoni,,tuache ubinafsi,,kama huyo bwenyeye hajui hata lini alilipa bili ya umeme..wao si ndo wanapewa unit sijui ngapi kila mwezi vyumba vyote viyoyoz,,,nilihama nyumba ya mfanyakz wa tanesco karibu nilie,,umeme ulikua unatumia chochote kinachotumia umeme na bado luku ilikua namba zimejaa kwenye screen ya luku,,,dadaaaa
 
Shirika la umeme nchini TANESCO limesema halina mpango wa kupandisha bei za umeme kwa watumiaji wadogo na badala yake mpango huo upo kwa watumiaji wakubwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema kuwa hakuna haja ya wananchi kuwa na wasiwasi kuhusu mapendekezo yaliyo wasilishwa na mamlaka ya udhibiti wa huduma Za nishati na maji EWURA.

“Niwatoe hofu wananchi kwamba yale mapendekezo tuliyoyapeleka wananchi wa kawaida wale wanaotumia umeme mdogo bei zao hazitaathirika sana. Kuna jambo moja ambalo tumelitazama kwa mtazamo tofauti, unajua sasa hivi we mteja wa kawaida unalipa sawasawa na kampuni zinazoweka mabango barabarani ambazo ni kampuni za kibiashara,” alisema Mramba.

“Sasa katika mapendekezo tuliyopeleka EWURA tulikuwa tunamuomba aangalie kwamba yale makampuni yanayofanya biashara za mabango ya matangazo yasilipe sawasawa na mteja wa nyumbani bei yake iende juu zaidi.”

HAPA NDIPO WAHESHIMIWA WANAJITOA UFAHAMU. YAANI WAFANYA BIASHARA NA MIMI MWENYE TAA MBILI TARRIF YETU NI SAWA. (MOJA)
 
Hao watumiaji wakubwa ndio wazalishaji wakuu wa bidhaa. Kuwaongezea gharama za umeme kutasababisha kupanda kwa gharama za bidhaa zao hali itakayowaathiri wananchi wa kawaida ambao ndio watumiaji wa mwisho. Serikali isimamie hilo kuhakikisha kuwa hakuna kupanda kiholela kwa gharama za umeme
 
Back
Top Bottom