Tanesco kuongeza bei ya umeme

hagg

Member
Jun 12, 2011
12
1
Wadau nimesikia Tanesco wako mipangoni kuongeza bei ya umeme. Kinachonisikitisha sio bei tu bali hata ratiba ya ukataji umeme haieleweki.Pili hi serikali imekua kama shule ya chekeckea mheshimiwa waziri nishati alisema makali ya mgao yatapungua kumbe ni uongo mtupu wanakata mpaka wanapitiliza sikuhizi. Tuliokua mkutanoni mlimani city ya 50yrs construction (engineers, architect, qs na wadau) mkuu wa nchi alitoa direct order ratiba ya mgao wa umeme iwekwe wazi na idara husika kwa wananchi pia nalo halijatekelezwa. Sasa mi nimekua na maswali mengi kuliko majibu hebu nifafanulieni kwa hoja.
 
Bei ya umeme inataka kupandishwa kufidia hasara ya dowans au kutumia mafuta na gesi ambazo bei zake ziko juu? Na ongezeko hilo ni la kudumu hata mungu akatujalia mvua ya baraka hydro system ikarudi kawaida? Nimejiuliza haya maswali mimi binafsi sina jibu. Tumechoka na uongo wa waziri wa nishati eti mgao utapungua hadi mwisho wa august kumbe ndio umezidi sasa. Mtu hajijui akae kazini au aikimbie nyumba sababu ya mgao wa umeme. Nadhani ni bora kieleweke kitu na sio kuengezewa bei kwa ajili ya kufidia hasara ya uzembe wa wahusika feki.
 
Back
Top Bottom