Tanesco kuomba leseni upya

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
Usanii mwingine huu! Eti wanataka kuilazimisha Tanesco iombe leseni kwa kufanya hivyo waruhusu makampuni yao ya kifisadi nayo yazalishe, kusambaza na kuuza umeme. Hawa hawa mafisadi na sera zao za kipumbavu zilizotuletea IPTL, Richmonduli, Netgroup solutions ndio waliohusika kuiweka hali ya kifedha ya Tanesco katika njia panda leo hii wanataka kuimaliza kabisa! Umeme Tanzania utakuwa ni kwa mafisadi tu maana bei itakuwa haishikiki na Watanzania walio wengi. Haya ndio maisha bora kwa kila Mtanzania.

Tanesco kuomba leseni upya

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima

SERIKALI imesema kuwa, Shirika la Umeme nchini (Tanesco), litalazimika kuomba upya leseni za kuendesha shughuli zake, iwapo sheria mpya ya umeme itapitishwa na Bunge na kusainiwa na rais.

Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, sheria hiyo mpya, ambayo muswada wake ulikuwa unajadiliwa jana, inatarajia kufungua milango kwa mashirika na kampuni nyingine binafsi kutoa huduma ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme hapa nchini na nje ya nchi, kitu ambacho kitaondoa ukiritimba wa Tanesco kama shirika pekee lililokuwa na haki ya kufanya hivyo.

Hata hivyo, akizungumza katika kikao hicho kilicholenga kukusanya maoni ya wadau kuhusu sheria hiyo mpya, Karamagi alisema kuwa, kupitishwa kwa sheria hiyo hakutamaanisha kuwa Tanesco itakuwa imepoteza haki zake kama shirika linalojihusisha na uzalishaji na usambazaji wa umeme.

Akifafanua, alisema kuwa kwa kuwa wadau wengine watatakiwa kuomba leseni ili kupata haki ya kufanya shughuli hizo, Tanesco nayo, kama mdau mpya, itatakiwa kuomba leseni hizo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Madini (EWURA).

"Na hii haina maana kwamba Tanesco itanyang'anywa, hapana, ila sheria ikishapita itabidi aombe leseni kwa kila kitu kimoja, kuanzia kusafirisha, ugawaji na usambazaji, tofauti na sasa ambapo ina ‘operate' kwa ujumla katika vitu vyote," alisema Karamagi.

Awali, akielezea madhumuni ya kutunga sheria hiyo mpya, Karamagi alisema kuwa Sheria ya Umeme iliyokuwa ikitumika, ilitungwa mwaka 1931 na imeshafanyiwa marekebisho mara 11 na kwamba hivi sasa sheria hiyo haikidhi matarajio tena kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza.

"Sheria hiyo pia haiendani na sheria ya sasa ya EWURA, pia haiweki wazi mamlaka na shughuli za serikali, mabadiliko ya sasa ni makubwa hatuwezi kuweka viraka tena kwenye sheria ya zamani," alisema.

Karamagi alisema kuwa mkakati wa kuwa na sheria mpya ya umeme unajenga mkakati wa upatikanaji wa umeme bora na wa uhakika na wa bei nafuu kwa kuruhusu makampuni binafsi kutoa huduma ya umeme.

Alisema sheria hiyo pia ina mkakati ambao madhumuni yake ni kuondoa ukiritimba ambao upo Tanesco, ambayo peke yake ilikuwa imeruhusiwa kuzalisha kusambaza na kusafirisha umeme.

"Sasa kuruhusu sekta binafsi kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme, inaruhusu kuhamasisha biashara ya umeme nchini na nchi nyingine," alisema.

Aidha, baadhi ya wadau waliotoa maoni juu ya sheria hiyo, waliipongeza serikali kwa hatua iliyochukua, huku baadhi yao wakisema kuwa sheria hiyo imechelewa kwa kile walichokieleza kuwa ucheleweshaji wa huduma na gharama kubwa zinazotozwa na Tanesco hivi sasa.

"Ilifika kipindi tulikuwa tunabembeleza Tanesco haki yetu, mazingira ambayo yalitengeneza rushwa," alisema mmoja wa wadau.

Hata hivyo, walionyesha wasiwasi juu ya udhibiti wa gharama endapo kampuni binafsi zitaruhusiwa, kitu ambacho Karamagi alisema sheria ya EWURA inaipa nguvu mamlaka hiyo kudhibiti bei na kwamba sheria hiyo hairuhusu mwekezaji kupanga bei.

Mbali na hayo, pia alisema kuwa sheria hiyo itawabana wawekezaji ambao watasitisha kutoa huduma bila sababu maalum, pia inalinda haki za mtumiaji.

Watu wachache walijitokeza kutoa maoni juu ya muswada huo, hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, William Shelukindo (Bumbuli-CCM), alisema kuwa endapo kuna mtu yeyote anayetaka kuwaandikia maoni, basi afanye hivyo na kamati itashughulikia.

Mkutano huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo, Mkurugenzi wa Tanesco, Dk. Idris Rashid, Mkurugenzi wa EWURA, Nasibu Masebu, watu mbalimbali kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), wanasheria kutoka Wizara ya Madini na wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo.
 
Salaam wanaJambo.... Duh hapo mimi naona kuna kautata au ka-plan ka mchezo mkubwa. Manake leo TANESCO wanaambiwa waombe leseni upya na imeshoneshwa kwamba kutakuwa na matawi matatu hapo (minimum being Generation, transmission and distribution). Sasa hapo kwa haraka, nimesema kwa haraka haraka naona kuna ifuatavyo:

1. TANESCO kama kampuni moja, iombe leseni ya kufanya biashara mara tatu - sitashangaa tukiambiwa kwamba haitawezekana na hivyo shirika livunjwe (parts ziuzwe kurahisisha uendeshaji)

2. TANESCO waombe leseni waambiwe kwamba hawana uwezo wa kufanya kazi zote tatu - hapo najua lazima Mtera, Kihansi etc (mabwawa yetu matakata) yapigwe mnada kwa vile TANESCO hawatakuwa na uwezo wa kuyaendesha (so they will say)...

3. TANESCO wachukue leseni zote, lakini ipitishwe sheria mpya ya mazingira (uhifadhi wa misitu/maji etc ambako kutapelekea TANESCO kukwama uzalishaji kwenye "their old school power generators" hivyo kufanya umeme ununuliwe kutoka Richmondia/DOWANS, KIWIRA Power, IPTL (na nyingine nyingi za wakubwa).... Hapo umeshaiona "D-Coy" hiyo?? Hapo ni win win tu hakuna kukosa hapo!!

4. TANESCO iamue kuwa kwa vile wamekwama kiutendaji na kimtaji kujiendeleza waombe kuachia baadhi ya majukumu kati ya yale ma3 na kutokuomba leseni zote 3 - "death warrant to all of us"

Haya ni mawazo yangu tu manake kwa kweli baada ya siku chache zilizopita ndio nimegundua kuwa kila dogo lianzalo na sisi tukadhani ni la manufaa kwetu wote limebadilika (!!!!) na matokeo yake ndio haya tunayoyaona.....

Baada ya kusema hayo machache, naomba niseme kwamba sikatai au kupinga mswaada (ambao haujapitishwa) kwamba ni mtego lakini kwa kuangalia Bunge letu lilivyo (elimu na uelewa wa waheshimiwa wengine pale mahali) kwa kweli sidhani kama kuna "light at the end of the tunnel" kwa waTanzania............Mwanga unaweza ukawepo lakini "only to the self selected few"
 
....., naomba niseme kwamba sikatai au kupinga mswaada (ambao haujapitishwa) kwamba ni mtego lakini kwa kuangalia Bunge letu lilivyo (elimu na uelewa wa waheshimiwa wengine pale mahali) kwa kweli sidhani kama kuna "light at the end of the tunnel" kwa waTanzania............Mwanga unaweza ukawepo lakini "only to the self selected few"


Naam Morani!
Naomba nikuunge mkono kwa kukubali kwamba kubinafsishwa kwa sughuli za uzalishaji na usambazaji wa umeme ndiyo njia pekee iliyobaki inayoweza kutunusuru Watanzania kuondokana na Dudu hili linaloitwa TANESCO. Tumeliunda wenyewe, ni letu lakini du, kama kuna mzazi anayemkataa mwanaye, basi naona inabidi iwe hivyo, huyu kamshinda mzazi!

Nasema hivyo kwa sababu ilivyo hivi sasa, TANESCO haisimamii tena maslahi ya watumiaji na Nchi kwa marefu na mapana yake. Ni zimwi ambalo nafikiri litatumaliza. Ingekuwa hivyo, tusingeweka mikataba inayoifilisi, ambapo inapelekea nayo kupandisha umeme, ambao nao unaifanya nchi yetu kutokuwa kivutio cha wawekezaji kwa sababu ya gharama kubwa za uendeshaji wa miradi ya kiuchumi, ambapo bila hiyo tutaendelea kuwa soko la bidhaa za kenya na china na "sauzi" na..., Katika mazingira hayo itabidi vijana wetu waendelee "kuzamia" kwa wenzetu wakitafuta kazi. Tumeruhusu, kwa kupitia TANESCO, makampuni yaendelee kabaka uchumi wetu ..

Kuruhusu wazalishaji wengine, kama ilvyokuwa kwenye Mawasiliano, kunaweza kutupa ahueni, moja kwa sababu mikataba ya TAnesco na hawa Wabakaji itakuwa voided, (sina hakika na hili), jambo ambalo lingetufanya watanzania tushangilie kucha.

Pili, ushindani ni muhimu katika utoaji wa huduma, ikiwepo huduma ya umeme. Sioni ni kwa nini Morani asiruhusiwe kuzalisha na kuwauzia umeme wenzie kijiji kwake badala ya kusubiri TANESCO ambao wameshindwa, au kama wakiweza ni kwa bei na kero za ajabu.

.... Duh hapo mimi naona kuna kautata au ka-plan ka mchezo mkubwa. Manake leo TANESCO wanaambiwa waombe leseni upya na imeshoneshwa kwamba kutakuwa na matawi matatu hapo (minimum being Generation, transmission and distribution). Sasa hapo kwa haraka, nimesema kwa haraka haraka naona kuna ifuatavyo:

1. TANESCO kama kampuni moja, iombe leseni ya kufanya biashara mara tatu - sitashangaa tukiambiwa kwamba haitawezekana na hivyo shirika livunjwe (parts ziuzwe kurahisisha uendeshaji)

2. TANESCO waombe leseni waambiwe kwamba hawana uwezo wa kufanya kazi zote tatu - hapo najua lazima Mtera, Kihansi etc (mabwawa yetu matakata) yapigwe mnada kwa vile TANESCO hawatakuwa na uwezo wa kuyaendesha (so they will say)...

3. TANESCO wachukue leseni zote, lakini ipitishwe sheria mpya ya mazingira (uhifadhi wa misitu/maji etc ambako kutapelekea TANESCO kukwama uzalishaji kwenye "their old school power generators" hivyo kufanya umeme ununuliwe kutoka Richmondia/DOWANS, KIWIRA Power, IPTL (na nyingine nyingi za wakubwa).... Hapo umeshaiona "D-Coy" hiyo?? Hapo ni win win tu hakuna kukosa hapo!!

4. TANESCO iamue kuwa kwa vile wamekwama kiutendaji na kimtaji kujiendeleza waombe kuachia baadhi ya majukumu kati ya yale ma3 na kutokuomba leseni zote 3 - "death warrant to all of us"

Haya ni mawazo yangu tu manake kwa kweli baada ya siku chache zilizopita ndio nimegundua kuwa kila dogo lianzalo na sisi tukadhani ni la manufaa kwetu wote limebadilika (!!!!) na matokeo yake ndio haya tunayoyaona.....

Naam, hapa ndipo penye tatizo !!...
Katika Uchumi kama nakumbuka, kuna kitu kinaitwa PARETO Optimality." Kwa kifupi maana yake ni kwamba siyo lazima kuongezeka kwa kipato kwa mmoja kuwe kunaambatana na kupungukiwa kwa mwingine - inawezekana kukwawepo na win-win kwa wadau wote. Kwa mantiki hiyo hiyo nafikiri hayo anayoyasema Morani hapo juu yakafanyika, lakini na sisi watanzania tupate vile vile, kama haiwezekani kabisa kutokufanya huo ufisadi. Pateni kwa kuiba, kama ni lazima, lakini na sisi je? Mnatuacha wote kwenye mataa?

Kuruhusu ushindani kuna manufaa makubwa mbeleni, lakini kutahitaji usimamizi mzuri sana kuweka misingi ya kulinda walaji.
 
kwani tatizo kubwa la tanesco ni lipi,Je ni mfumo gani ambao sasa tunatakiwa kuufuata baada ya mswada mpya kupitishwa.
Ina maana hata mimi leo naweza kufunga generetor yangu na kuwauzia watu umeme ?,binafsi sijahelewa hasa hii biashara itakuwaje baada ya muswaada mpya kupitishwa kwa kweli mimi nipo gizani.hapa kijijini kwetu kuna makampuni mengi ambayo yanauza umeme na gas,unapo hama kutoka kampuni moja unachofanya ni kubadilisha kadi,kama mita yako ni pay as you go,au kama unalipa kwa mwezi basi wao hubasilisha kwa kuwasiliana kampuni kwa kampuni hata simu ni hivyo hivyo sasa kwa bongo mambo ni aje.
Mwenye kujua kwa undani hatufahamishe.nisije peleka kageneretor kangu nikambulia patupu
 
kwani tatizo kubwa la tanesco ni lipi,Je ni mfumo gani ambao sasa tunatakiwa kuufuata baada ya mswada mpya kupitishwa.
Ina maana hata mimi leo naweza kufunga generetor yangu na kuwauzia watu umeme ?,binafsi sijahelewa hasa hii biashara itakuwaje baada ya muswaada mpya kupitishwa kwa kweli mimi nipo gizani.hapa kijijini kwetu kuna makampuni mengi ambayo yanauza umeme na gas,unapo hama kutoka kampuni moja unachofanya ni kubadilisha kadi,kama mita yako ni pay as you go,au kama unalipa kwa mwezi basi wao hubasilisha kwa kuwasiliana kampuni kwa kampuni hata simu ni hivyo hivyo sasa kwa bongo mambo ni aje.
Mwenye kujua kwa undani hatufahamishe.nisije peleka kageneretor kangu nikambulia patupu

KT,
Muswada huo utatupeleka kwenye utaratibu kama huo hapo kijijini kwenu uliko. Kwa uelewa wangu mdogo, ni kwamba watakuwepo wazalishaji binafsi wengi inavyowezekana ambao watakuwa wanawauzia wasambazaji waliosajiliwa ambao na wanawauzia watumiaji. Kwa kuwa wazalishaji wote wataunganishwa kwenye Grid moja, inawezekana kukawepo na mnada wa wauzaji wa umeme. Msambazaji nitanunua kwa mzalishaji mwenye bei nafuu, na anawasha mashine zake tunaanza kuhesabiana kiasi (Kwh, MWh nk) na kulipana. Ni kama bidding inavyofanyika kwenye internet (eBay) na kwingineko.

Labda utudokezee tofauti ya bei kati ya kampuni moja na nyingine huko, tuone kama kuna cha kujifunza. Ni muhimu sana maswala haya yakashirikisha maoni mengi iwezekanavyo, (kama watataka kuwepo uwazi na kusikiliza) hasa kwa kujifunza kwa wengine ili kuwa na mfumo mzuri na endelevu kwa sababu tatizo tulilo nalo ni kwamba ubinafsishaji umekuwa wa manufaa sehemu nyingi ulikofanyika kasoro hapa kwetu kwa sababu haufanywi na kusimamiwa kwa maslahi ya umma.

Pia tunawaomba waelewa wa mambo ya umeme watuelimishe hapa. Kwa mfano wasambazaji wapya watatakiwa kujenga miundombinu yao au hiyo hiyo iliyowekwa na Tanesco inaweza kutumiwa na msambazaji yeyote kwa makubaliano fulani n. k.?
 
Back
Top Bottom