TANESCO: Kumetokea hitilafu katika Kituo cha kupoza na kusambaza Umeme cha Ubungo (Gridi ya Taifa)

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,630
10,243
Mitamboumeme UBUNGO,imepata hitilafu,nchi nzima haina umeme !

====

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA KWA HITILAFU KATIKA GRID YA TAIFA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake na Umma kwa ujumla kuwa kumetokea hitilafu katika Kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza Umeme cha Ubungo, hitilafu hiyo imesababisha Grid ya Taifa kutoka na kusababisha Mikoa yote iliyounganishwa katika Grid ya Taifa kukosa Umeme.

Mafundi wanaendelea na jitihada ya kurejesha Umeme katika hali yake ya kawaida.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makuu
 
Nilisikia USA wakidai eti baada ya matokeo yao ya uchaguzi kudukuliwa, mdukuaji alikuwa na mpango wa kudukua vinu vya kuzalisha umeme pia. Hiyo imekaaje kwa TZ!?
 
NI KWELI, HAPA JIJINI DSM UMEME UMEKATIKA HATA KWENYE TAA ZA KUONGOZEA MAGARI!!!
 
Nipo karibu na ubungo mida ya kumi na mbili alfajiri nilisikia mlio mkubwa utadhani boom na umeme ukakatika.kumbee ni tanesco hapo sawa
 
aiseee!....GIZA...ndo wapambane tupate umeme oooooh!.....asante kwa taarifa
 
Mimi nipo sumbawanga umeme huku haukatikagi sijui ni uchawi au sielewi elewi.....
Teh teh teh teh....
 
Dah kwa hiyo adui akitaka kufanya yake analipua tu ubungo kazi imekishwa ?

Sijui ni lini tutakuwa na plan B,C,D,E,F,G ......
Badala yake tunafukuzana na walio print Tshirt za njaa
 
Ok nilizani mgao umerudi kumbe kuna hitilafu, ahsante kwa taarifa pia cjui baada ya muda gani tatizo litaisha?
 
Unakuta Jitu Jeusi Lina Gari ya Million 200, Nyumba ya million 300 lakin ndani Hana Generator hata ya million mbili wala Fire extinguisher ya Laki 5.

Watu wengi wanajali sana kuwa na vitu vinavyoonekana machoni kama magari ya kifahari, nguo za kifahari, nyumba za kifahari... lakini ukiwauliza vitu muhimu kama stand- by power supply, internet connection, etc hawana. Utakuta mtu ana biashara zake zinazohitaji mawasiliano ya internet akishatoka ofisini basi he is cut off
 
Back
Top Bottom