Tanesco kulipisha nguzo ya umeme Tshs 27,000/- ni kweli au mbwembwe?

kasindaga

Senior Member
Sep 6, 2013
165
165
Mitandaoni tangu awamu iliyopita Waziri wa Nishati alisema kuanzia sasa nguzo za umeme wa chini (Lv) Tanesco ni bure ila Kodi ya serikali kila mteja Tshs 27000/- lazima ilipwe.

Je, kibiashara Tanesco inawezekana?Tangu tamko hilo litolewe Usambazaji wa umeme imekuwa tatizo. Hilo tamko lilizingatia nini au mbwembwe tu za kupigiwa makofi? Je Tanesco inazalisha nguzo? Kama hapana mwekezaji mwenye shamba la miti atakubali kushusha Bei ya nguzo?

Tupate ufafanuzi ili tuichukie Tanesco au Waziri na Wizara yake
 
Hapa dawa ni kuwapiga chini TANESCO na kufunga solar kila nyumba, viwanda n.k. wanaviburi mno hawa viumbe, wameota mapembe.

Tushirikiane kwa pamoja kufunga umeme wa solar
 
Mambo mengine ni kutudanganya tu ,wametangaza ila tumechoka kusubiri nguzo ,wakiongea kurahisisha mambo utadhani nguzo ni Kama migomba
 
Bado haijakaa vizuri akilini huyu Mh Kalimani aliposema nguzo bure alikuwa anamaanisha nini? Tanesco analo shamba la nguzo? Au mbwembwe?
 
Back
Top Bottom