Tanesco Kulikoni?

jacobae

Member
Oct 29, 2007
68
1
Wandugu wapendwa hivi kuna tatizo gani mimi sijaelewa, tuliambiwa kutakuwa na mgao wa saa kumi lakini naona huu wa karibu saa 24 kuna tatizo gani, hapa nilipo tangu jana saa kumi na mbili jioni hadi muda huu haujarudi na maeneo ambayo ulikuwepo wamechukua... ni mgao tu huu huu au kuna tatizo lingine? Tujuzane wenzangu!
 
Nafikiri swala la TANESCO mda wa kulizungumza umeshapita na huu ni mda wa nyongeza, kinachotakiwa ni kunyesha kwa vitendo kuwa tumechoka. Nimerudi home jana saa 17:30 nikaambiwa umeme umekatika saa moja asubuhi, hadi saa hizi bado haujarudi.
 
Hakuna kingine NiDOWANS MPYA inatengenezwa! tayari kuna AGRRECCO anarudi kwa kasi namkataba Mheshimiwa Mkubwa Sana Mhando kakataa katakata kuusema hadharani!
Jamnai yatakiwa tuanze kama TUNISIA!
Mheshimiwa Daktari, Rais, Mwenyekiti, Amiri Jeshi Mkuu yeye yupo Buzy na trip za nje as if Tanzania iko shwari kama vile tuko PEPONI!
Ni lini tutaacha huu ukondoo?
 
Kweli haya ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania. Inabore kwa kweli.
Mkuu, hii kitu sasa imezidi, nafikiri watanzania tutafute namna ya kuheshimiana na kila mtu kutimiza wajibu wake.
Tanesco na serikali yao wanatunyanyasa kwa kweli.
 
Mkuu, hii kitu sasa imezidi, nafikiri watanzania tutafute namna ya kuheshimiana na kila mtu kutimiza wajibu wake.
Tanesco na serikali yao wanatunyanyasa kwa kweli.
Mkuu ni kweli kabisa... Kuna msemo usemao bubu akizidiwa huongea naona ndiko tunakoelekea sasa...
 
Back
Top Bottom