Tanesco kukata umeme Kigamboni, tatizo nini?

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,994
10,497
Tanesco niliwaambia jana kuwa nyinyi ni kerroo tena keroo ya kupitiliza. Mmeshachukua umeme wenu huku kwetu kama kawaida yenu .

Sasa naomba mtueleze huu mgao ni rasmii au ndo mmechoka kuhudumia.
Nataka kujua mtaurudisha saa ngapi au vinginevyo niende kununua kiwese nijiandae kwa kibatali.

Yaani mnakera mnakera. Ukiuliza hivi utaniambia nikupe namba yangu itakusaidia nn??? Ndio itarudisha umeme? Msituzingue umeme huu tunaulipia hamtupi bureee

Eneo kuanzia kigamboni kibada mpaka mbgl saizi hakuna umeme.

RUDISHENI UMEME

TANESCO

CC: @JPMAGUFULI
F.U.A
 
Mnategemea mtangaziwe mgawo? Sii awamu hii. Hiyo ni kimyakimya tu. IPTL down, Symbion out. Kinyerezi mtambo mmoja. What do you expect.
 
Hawataki kusema wazi wazi ila mgao huo ni rasmi kwakuwa tumeshaanza kuuzoea kwa takribani mwezi sasa.

Waliposema wanahitilafu kwenye kituo chao cha Kinyerezi, kama hukuwaelewa ni kuwa 150MW zimetoka kwenye Grid na mpaka sasa hawajasema wamefikia wapi na nini mategemeo yao.

Baadhi ya vituo vyao vya kuzalisha umeme, havizalishi kwa asilimia zote bali karibu nusu ya uwezo wa kituo umepungua kutokana na kukosa matengezo sahihi ya mitambo.

Ajabu wakurupukaji wamekaa kimyaaaaa!!!
 
Mnategemea mtangaziwe mgawo? Sii awamu hii. Hiyo ni kimyakimya tu. IPTL down, Symbion out. Kinyerezi mtambo mmoja. What do you expect.
IPTL, Symbion hazikutuyumbisha ndugu kwakuwa bila hizo tulikuwa tuko stable.....umeisahau na Aggreko.

Kinyerezi + Vituo visivyozalisha to the fullest.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom