TANESCO kugawanywa katika kampuni tatu (gazeti la majira)

GAGL

JF-Expert Member
Aug 5, 2010
390
395
Serikali inapanga kuigawa TANESCO katika makampuni matatu.

1. Kampuni ya uzalishaji.

2. Kampuni ya usafirishaji.

3. Kampuni ya usambazaji.

Nisaidieni hapo kwenye makampuni mawili ya mwisho, nashindwa kuona tofauti ya kimsingi ya kiutendaji kati ya makampuni haya mawili.
 
nafikiri kusafirisha na kusambaza ni tofauti

kusafirisha - mfano kutoa umeme kidatu na kuleta hapa dar
kusambaza - mfano umeme ukiwapo substations za dar na kupeleka majumbani/viwandani kwa watumiaji
 
nafikiri kusafirisha na kusambaza ni tofauti

kusafirisha - mfano kutoa umeme kidatu na kuleta hapa dar
kusambaza - mfano umeme ukiwapo substations za dar na kupeleka majumbani/viwandani kwa watumiaji
ha ha ha!1 hii kali
inabidi kuwe na kampuni la wafunga luku,madereva,etc
walikiligawanya itakuwa ngumu sana kuliendesha kutokana na urasimu,hapo linagawanywa ili liwe weak then mafisadi wafanye mambo yao. nothing new hapo cha kuwasaidia wa tz.mifisadi ni mijitu mibaya sana
 
Serikali inapanga kuigawa TANESCO katika makampuni matatu. 1. Kampuni ya uzalishaji. 2. Kampuni ya usafirishaji. 3. Kampuni ya usambazaji. Nisaidieni hapo kwenye makampuni mawili ya mwisho, nashindwa kuona tofauti ya kimsingi ya kiutendaji kati ya makampuni haya mawili.

Unashindwa kutofautisha mkulima anaesafirisha mazao mpaka sokoni kariakoo na mchuuzi wa pale kariakoo? basi wewe unamatatizo na unahitaji msaada.
 
nashauri ni vizuri ikgawanywa kwenye makundi mawili badala ya matatu tukabaki na i) Uzalishaji na ii) Usambazaji
I)Uzalishaji utafanya kazi ya kuzalisha umeme na kupeleka hadi kwenye substation zao na II) Usambazaji utafanya kazi ya kutawanya umeme kupeleka kwa watumiaji, uunganishaji na kusimamia mauzo. Hii iendane na mabadiliko makubwa ya uongozi naninashauri wale wote viongozi wa zamani wabaki kwenye kampuni ya uzalishaji kwa sababu ndio kazi wanaijua na hawana uwezo wa kuhudumia wateja kwa viwango vya kisasa.
Hii itaoingezea shirika udhibiti wa mapato na udhibiti wa rasilimali zake.
 
Hii kali, hawana mkakati wa kupunguza gharama za umeme wanachoangalia hapo kuna maswahiba hawajapata ubunge ndio wapewe ukurugenzi, Tanzania raha sana!!
 
Serikali inapanga kuigawa TANESCO katika makampuni matatu. 1. Kampuni ya uzalishaji. 2. Kampuni ya usafirishaji. 3. Kampuni ya usambazaji. Nisaidieni hapo kwenye makampuni mawili ya mwisho, nashindwa kuona tofauti ya kimsingi ya kiutendaji kati ya makampuni haya mawili.

Usafirishaji kutoka Kidatu kwenda Dar.,Iringa nk. na usambazaji kutoka Dar na Iringa vituo vikuu kwenda kwa mtumiaji/mlaji Gongo la mboto nk.
 
Generation,transmission,distribution
generation-uzalishaji wa umeme kama vile mtera dam
transmission- usafirishaji wa umeme kutoka mtera kwenda grid ya taifa
distribution- ugawaji toka grid ya taifa mpaka tandika!

I stand to be corrected tho!
 
Kama hii nik kweli itakuwa ni jambo zuri maana litanesco ni likubwa mno kisi kwamba ufanisi inakuwa kitendawili sometimes. Na kwa muundo huu ina maana utapeli utakuwa kiasi flani limited!
 
Serikali inapanga kuigawa TANESCO katika makampuni matatu. 1. Kampuni ya uzalishaji. 2. Kampuni ya usafirishaji. 3. Kampuni ya usambazaji. Nisaidieni hapo kwenye makampuni mawili ya mwisho, nashindwa kuona tofauti ya kimsingi ya kiutendaji kati ya makampuni haya mawili.

Usafirishaji = Transportation

Usambazaji = Distribution
 
1. Kampuni ya uzalishaji: AGREKOL, ARTMUS, IPTL, RICHMOND/DOWANS, SONGAS
2. Kampuni ya Usafirishaji: TANESCO
3. Kampuni ya Usambazaji: TANESCO
 
I cant wait to see watavyokuwa wanaruhushiana mipira. Na kwa hali ilivyo sasa sana sana itamuongezea mzigo mtumiaji wa mwisho. Wenzetu wanafanya hivi kwa ajili ya efficiency lakini kwa Tanznaia bado efficiecny ingewezekana mambo yote kuwa chini ya mwamvuli mmoja wa Tanesco chini ya serikali.

Serikali kutaka kujitoa kwenye Nishati Ni sanaa. Ona migodi inaingza mitambo yao ya uzalishaji umeme. hayo yote ni mapato ambayo yamepotea.

More than Five diffeerent entities zinazalisha umeme yet kuna mgao........!!!!!!!!!!!!. Huu umeme wa mafungu hautasaidia kabisa.

BOT pale wana magenretaor standbdy yanaweza kuzalisha umeme kukidhi matumizi ya mkoa wa singida na dodoma kwa pamoja. U can see jinsi sera mbovu zinavyo..... Ngoja niishie hapa

1. Kampuni ya uzalishaji: AGREKOL, ARTMUS, IPTL, RICHMOND/DOWANS, SONGAS
2. Kampuni ya Usafirishaji: TANESCO
3. Kampuni ya Usambazaji: TANESCO

Mfumo huu utawasaidia hao wazalishaji kuendelea kula fedha yote atakayokuwa anatengeneza msambazaji na msafirishaji kama ilivyop sasa tu
 
Unashindwa kutofautisha mkulima anaesafirisha mazao mpaka sokoni kariakoo na mchuuzi wa pale kariakoo? basi wewe unamatatizo na unahitaji msaada.

Hapa unatuchanganya, maana nyanya zinasafirishwa kwa mafuso toka Ilula na Moshi hadi Kariakoo shimoni, sasa umeme utasafirisha kwa usafiri upi? Tafadhali nieleweshe zaidi
 
Back
Top Bottom