Tanesco kufungua zabuni ya ununuzi mitambo keshokutwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco kufungua zabuni ya ununuzi mitambo keshokutwa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Mar 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Ofisi za shirika la Umeme nchini Tanesco zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam.  Shirika la Umeme nchini (Tanesco), linatarajia kufungua zabuni ya ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 60 mkoani Mwanza Ijumaa ya wiki hii, wakati ile ya mtambo wa kuzalisha megawati 100 katika kituo cha Ubungo itafunguliwa Aprili Mosi, mwaka huu.
  Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud aliliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana alipozungumza nalo juu ya mchakato wa zabuni hizo.
  "Ufunguzi wa zabuni ya mtambo wa megawati 60 utafanyika Machi 26 na ile ya megawati 100 utafanyika Aprili mosi," alisema Badra kwa ufupi. Zabuni za mitambo hiyo zilisitishwa kwa muda miezi mitatu baada ya Serikali kubaini kasoro kadhaa.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...