TANESCO kufanya ukarabati wa kituo cha kufua gesi Ubungo II, baadhi ya maeneo ya Dar, ZNZ na Pwani kukosa umeme

NGolo Kante

Member
Feb 28, 2017
80
131
TAARIFA YA UKARABATI WA MASHINE KITUO CHA KUFUA UMEME KWA GESI CHA UBUNGO II

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa kuanzia Januari 9, 2019 hadi Februari 13, 2019 utafanyika ukarabati kwenye mitambo ya kuzalisha umeme ya kituo cha Ubungo II.

Ukarabati huo utahusisha ubadilishaji wa vipuri ili kuiongezea ufanisi mitambo hiyo.

Kutokana na ukarabati huo baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani pamoja na Zanzibar yataathirika kwa kukosa huduma ya umeme.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza


IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
 
Hivi inamaana Tanzania hatuna redundancy ya mitambo kabisa? Yaani hatuna ya akiba ili iliyopo ikiharibika tuwashe ya akiba? Inamaana Marekani na ulaya huwa hawafanyi hizo maintanance? Mbona umeme huwa hawatangazi kukatika wakati wa matengenezo, si muwahamishie tu kwenye line nyingine ya umeme toka Kinyerezi?
 
Na joto lote hili wanataka kutukatia umeme?

Halafu mbona hawajasema ni maeneo yepi yatayokosa umeme..!!!!
 
Tanesco bado kazi zao wanafanya Kizamani sana halafu kama umeme wanaugawa bure hawako kiushindani . Watu wote watakaokosa huo umeme kipindi hicho cha matengenezo wasingekosa ela kiasi gani ingeingia tanesco ?
 
Back
Top Bottom