Tanesco kuamua kama wana-Arusha kumwona Dr. Slaa "live" Movenpick..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco kuamua kama wana-Arusha kumwona Dr. Slaa "live" Movenpick.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Oct 23, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Imekuwa ni tabia ya Tanesco hapa Arusha kutunyanyasa sisi wakaazi wa Arusha kwa kutukatia umeme mara kunapokuwepo shughuli nyeti ya Chadema na Dr. Slaa na hata huwa hawatuombii msamaha....kwa vurugu zao hizo.......

  Kwa mara ya kwanza Chadema walipozindua kampeni zao Dar-Es-Saalam, hawa jamaa zetu wa Tanesco walitukatia umeme na walipoona akina Tindu Lissu na Mabere Marando wamekwisha kuongea wakaturudishia umeme.......Walitunyima kufaidi matukio hayo muhimu ambayo yaliwaghadhibisha TBC1 hata wakakata matangazo kwa muda hivi....

  Sina uhakika leo kama Tanesco watakuwa na huruma nasi hapa Arusha ukizingatia JK maji ni shingoni na kamwe CCM wasingependa tuendelee kujifunza mengi kutokana na nasaha ambazo Dr. Slaa angetupatia leo kutoka hapo Movenpick na ni live kupitia ITV channel yetu ya wanyonge.........CCM hawataki midahalo lakini vile vile hawapendi wengine wa upinzani wafanye hiyo midahalo sasa sijui tuwaeleweje....

  Ninajua Tanesco hapa Arusha itakuja na visingizio vya kuwa umeme hautoshi na ya kuwa saa hizo ni "peak hours" lakini walipotukatia siku Chadema wanazindua kampeni zao hazikuwa ni "peak hours".........kwa hiyo Tanesco wasituletee bughudha hii..........
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mwaka wao huu CCM hawapinduki yaani kila mahali tight vibaya sana...hahaaaa JK uraisi sio lelemama mwanakwetu
   
 3. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  ITV ka vp warekodi kipindi na warushwe siku zinazofuata.
   
 4. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Nilichofanya tu leo asubuhi ni kuhakikisha generator langu linafanyakazi maana sintavumilia kutokumwona rais wangu DR.SLAAAAAAAAAAAAAAA akiongea LIVE na nisimwone, sijui sana lakini hata Tanesco nadhani wamewachokaa hawa chichiem.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Uongo mbaya eneo langu umeme haukukatwa lakini kuna jaama yangu alipoanza kusilikiliza mdahalo alijikuta yuko gizani sasa sijui ni nini kilitokea........Jana kwa mara ya kwanza nilijiona ni mtanzania kweli.....Eh Mwenyezi Mungu kisikilize kilio cha watoto wako utpe Dr. Slaa aje kutupunguzia kero kibao hapa nchini hususani za umasikini......
   
Loading...