TANESCO kuachana na Symbion na Aggreko?

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,873
Inadaiwa Bodi ya wakurugenzi ya TANESCO imepania kuachana na Mikataba ambayo inaonekana kuwa mzigo kwa shirika kati yake na Makampuni ya Symbion Power na Aggreko mwezi Oktoba 2014, kutokana gharama kubwa zisizoshikika toka kwa Makampuni haya.

Nini hatma ya TANESCO?

Tunao mbadala wa makampuni haya?

Tutarajie mgao mkubwa kuelekea 2015?

Tumepata uhakika baada ya kupatikana kwa gesi?
 
tanesco ni janga lingine kwa taifa
Wakiweza kuvunja hii mikataba tutafungua ukurasa mpya, lakini wasiwasi wangu ni kama tunao mbadala wa makampuni haya ambayo kiukweli yanatia hasara kubwa sana japo yanasaidia.

Kumbuka, ni mwaka jana tu tuliambiwa kuwa TANSECO wanailipa kila siku Symbion Power milioni 152 na katika kila sh.100 zinzoingia TANESCO, sh.86 inaelekwzwa kwenye malipo hayo!
 
Kwa kiasi fulani kupanda kwa bei ya umeme kunachangiwa sana n mikataba hiyo oliyoingiwa kati ya TANESCO na makapuni hayo ya kitapeli.
 
Kwa kiasi fulani kupanda kwa bei ya umeme kunachangiwa sana n mikataba hiyo oliyoingiwa kati ya TANESCO na makapuni hayo ya kitapeli.
Na kwa kiwango kikubwa watanzania wenyewe tunachangia kwa kukomaa na siasa ambazo zinatuondoa kwenye mambo ya msingi na kuacha mambo yaende kama yanavyokwenda.

Imagine, 152million kila siku kisha zidisha kwa siku 365 na hapo ni Symbion Power tu!
 
Simple, Wavunje mikataba na tuwe tayari kwa matokeo yake.

Sidhani kama hakuna mbadala wa huu unyonyaji.
Na wala sioni sababu ya kusubiri mwaka zaidi. Siamini kama kiasi kinacholipwa kwa Symbion ni kiasi ambacho ni stahiki.

Tunaihitaji nishati, hili halina mjadala lakini Nishati hii ikipatikana kwa maumivu kiasi hiki na kupelekea kufikiria kupandisha bei ya umeme huku raia wa kawaida akiumia na hata kutishia wawekezaji kufikiria kuja TZ ni kuliangamiza Taifa.

Watanzania nadhani mpaka mtu awatie vidole kwenye macho ndo wanashtuka kuwa anawachokoza!
 
Ni aibu kwa nchi yetu kuwa na taasisi mbovu kama TANESCO. Viongozi wake wapo, wanajua mikataba mibovu ilivyo,wamekaa kimya tu.
 
Ni aibu kwa nchi yetu kuwa na taasisi mbovu kama TANESCO. Viongozi wake wapo, wanajua mikataba mibovu ilivyo,wamekaa kimya tu.
Mind games; Think again!

Siasa zimeingia kila sehemu. Tutazuiwa na wanasiasa kuongelea hata baadhi ya issues na usishangae kuwa unaweza kuwa branded 'msaliti' au 'unatumiwa' au 'hii hoja yetu' na wale wanufaika wanazidi kunufaika kutokana na kugawanyika kwetu!

Tunatakiwa kurejea kwenye mstari. Tunajenga nyumba moja, tusigombanie fito. Wanawekeza kwenye ujinga wa wachache, wanakatisha tamaa wale wenye kuweza kuyaona madudu na kuyakemea critically
 
Nimewahi kujiuliza,

Kama tukiamua kuvunja mikataba alafu tukaamua kukubali ujinga kwa muda lakini wenye gharama nafuu kwa kununua umeme kutoka nchi za jirani ili ibaki mikoa michache kutumia gridi ya taifa.

Nadhani kulaumiana sasa hakutabadili kitu zaidi ya mawazo mapya.
 
Na wala sioni sababu ya kusubiri mwaka zaidi. Siamini kama kiasi kinacholipwa kwa Symbion ni kiasi ambacho ni stahiki.

Tunaihitaji nishati, hili halina mjadala lakini Nishati hii ikipatikana kwa maumivu kiasi hiki na kupelekea kufikiria kupandisha bei ya umeme huku raia wa kawaida akiumia na hata kutishia wawekezaji kufikiria kuja TZ ni kuliangamiza Taifa.

Watanzania nadhani mpaka mtu awatie vidole kwenye macho ndo wanashtuka kuwa anawachokoza!
Hapo ndo kwenye tatizo
hizo capacity charges zingeweza hata kuinunua hiyo mitambo kabisa
 
Wakiweza kuvunja hii mikataba tutafungua ukurasa mpya, lakini wasiwasi wangu ni kama tunao mbadala wa makampuni haya ambayo kiukweli yanatia hasara kubwa sana japo yanasaidia.

Kumbuka, ni mwaka jana tu tuliambiwa kuwa TANSECO wanailipa kila siku Symbion Power milioni 152 na katika kila sh.100 zinzoingia TANESCO, sh.86 inaelekwzwa kwenye malipo hayo!

Hawataweza, labda kutokee miujiza. Ukiangalia hata muundo sasa hivi ni kama makampuni haya binafsi yamepewa Kandahar zao za kuzalisha umeme. Tumeshuhudia jinsi serikali ilivyoachana na mpango wake wa wali wa kujenga kituo cha kuzalisha umeme Mtwara na badala yake wakaingia Mkataba na Symbion. Je wataachana nao ki vipi na nini mbadala wa hii?
 
Ikiwa waliisaini na mpaka ifikapo October 2014 itakuwa bado ni mikataba hai, hapo tutajiingiza katika gogoro lingine kama lile tililojiingiza na Dowans ya Al Adawi. Mpaka leo tunalipa kwa gharama kubwa sana, kwa kujidai kwetu kutaka kuvunja mkataba wa Kimataifa. Tutawalipa tu.

Lakini ikiwa mpaka ifikapo hapo October 2014 tutakuwa tumemaliza nao mkataba basi itakuwa ni sawa na hatuna lawama.

Ikumbukwe kuwa mikataba ya Aggreko na Symbion ni mikataba ya dharura mpaka pale tutakapoweza kujikimu na umeme wa uhakika. Kuna miradi mingi ya muda mrefu ambayo inatekelezwa kwa sasa. hakuna sababu kwanini tuendelee na mikataba ya dharura pale tutapokuwa tunajiweza wenyewe.

Isitoshe, ni rahisi sana kwa Symbion na Aggrekko kutuuzia mitambo yao kwa bei nafuu pale tutapokuwa tunajiweza kwa umeme wa uhakika na hiyo mi jenereta yao ikabaki kwetu kwa dharura tu, kwani mpaka wakati huo watakuwa wamesharudisha fedha zao na mifaida kibao.

Waafrika tuone hivi hivi tunajuwa sana kuongea, kupanga na kupangua lakini hatujuwi kutekeleza. Leo mchukuwe Mtanzania yeyote umuulize kuhusu ligi ya mpira wa Uingereza, basi utamkuta anaijuwa hiyo ligi na namna timu inatakiwa iwe kuliko Mourinho. Hiyo si kwenye mpira tu, ni kila pahali, tunajuwa kila kitu kwa midomo yetu lakini kutenda? Ng'oo.

Nchi hii muumba dunia na ardhi alitujaaalia kila kitu chema, maji mengi, madini mengi, ardhi nzuri inayo-limika miezi 12 kwa mwaka, misitu mizuri, mbuga nzuri, milima mizuri, mabonde mazuri, watu wazuri, wanyama wazuri. Kwa ufupi katupa pepo ya duniani, lakini kitu kimoja hatukupewa, nacho ni akili. Akili hatuna.

Binaadam hakosi kasoro na kasoro yetu ni akili.

Wakati sisi tutaanza kuwa na umeme wa uhakika (miaka 50-100 ijayo), kumbuka kuwa mpaka sasa ni 14% tu ya Watanzania wenye umeme tena sio wa uhakika, wenzetu watakuwa hawana haja ya maviwanda ya umeme, majumba na maviwanda yanayohitaji umeme yatakuwa yanajizalishia yenyewe umeme (haya yameshaanza kwa wenzetu, kuna majumba mapya huko yanajizalishia yenyewe umeme na ule wa ziada wanawauzia gridi zao) Hapo sasa.

Self-sufficient Urban Buildings | BETTER WORLD // ENGINEERING

Sosoljip is a Self-Sufficient Net Zero Energy House in South Korea | Inhabitat - Sustainable Design Innovation, Eco Architecture, Green Building

MenoMenoPiu Unveils Plans for Wind-Powered Alvar Aalto Campus Otaniemi | Inhabitat - Sustainable Design Innovation, Eco Architecture, Green Building
 
Hofu kubwa ni je itavunjwa kweli ? Maana hao Viongozi ndiyo wafanyabiashara hapo.
 
Hizo gharama za kuvunja mikataba ziwekwe wazi na ikibidi ziwasilishwe bungeni ili watanzania wote tujue.

Vile vile kuna umuhimu wa kupitisha sheria itakoyolazimisha watu wote wanaoandaa na wale wanaoingia mikataba mibovu na ya kinyonyaji kwa niaba ya watanzania majina yao yatangazwe hadharani.
 
Wakiweza kuvunja hii mikataba tutafungua ukurasa mpya, lakini wasiwasi wangu ni kama tunao mbadala wa makampuni haya ambayo kiukweli yanatia hasara kubwa sana japo yanasaidia.

Kumbuka, ni mwaka jana tu tuliambiwa kuwa TANSECO wanailipa kila siku Symbion Power milioni 152 na katika kila sh.100 zinzoingia TANESCO, sh.86 inaelekwzwa kwenye malipo hayo!

Tunayo machaguo mawili tu kuwezesha Watanzania walipie umeme katika viwango stahiki; kuvunja mikataba na kuwa tayari kukabiliana na kesi au kuendelea kuumia kwa miaka iliyobaki takribani 10!

Kwa kiasi fulani kupanda kwa bei ya umeme kunachangiwa sana na mikataba hiyo oliyoingiwa kati ya TANESCO na makapuni hayo ya kitapeli.

HUO NDIYO UKWELI. Ndiyo maana napingana na pupa ya utekelezaji wa miradi ya PPP kwenye sekta zote kwa mkupuo wakati historia na uzoefu wetu katika Ubinafsishaji na mikataba ya PPP za awali (Reli-TRL, Ndege-SAA, TANESCO-Net Group Solutions, etc) zote zinaonyesha hakuna tulipofanikisha kuongeza ufanisi wala kuboresha huduma au kuboresha maisha ya mwananchi.

Invisible kwenye hili la TANESCO mzimu mkubwa ni IPTL na ndiyo iliyo na concession ya muda mrefu na capacity charge kubwa. Hivyo kugusa Symbion Power na Aggreko kunaweza kusilete noticable relief kwa mtumiaji. Na kwa upande wa Symbion Power sioni uwezekano kabisa wa Serikali yetu (hasa ya chama kinachotawala) kupata ujasiri wa walau kuingiwa na wazo la kuvunja mahusiano na Symbion Power katika miaka hata 10 ijayo!

Kunielewa vema unapaswa kuvuta kumbukumbu ya malengo yaliyotimizwa katika ziara ya Obama ya mwezi July mwaka huu. Jibu la haraka ni kwamba kugusa Symbion Power unamaanisha kukata mrija wa mabilioni ya Millenium Challenge Account na kukwamisha miradi mikubwa ambayo serikali inaikamilisha kuitumia kama turufu kwenye chaguzi kuu zijazo. Hii ni kiboko na karoti, punda anasogeza mzigo!

[video=youtube_share;UPMFuTX_-L8]http://youtu.be/UPMFuTX_-L8[/video]
 
Inadaiwa Bodi ya wakurugenzi ya TANESCO imepania kuachana na Mikataba ambayo inaonekana kuwa mzigo kwa shirika kati yake na Makampuni ya Symbion Power na Aggreko mwezi Oktoba 2014, kutokana gharama kubwa zisizoshikika toka kwa Makampuni haya.

Nini hatma ya TANESCO?

Tunao mbadala wa makampuni haya?

Tutarajie mgao mkubwa kuelekea 2015?

Tumepata uhakika baada ya kupatikana kwa gesi?
Mikataba yote hiyo ni ya kinyonyaji kupindukia. Tanesco inaweza kuwa na mitambo yake na kuachana na kupe. Hata hivyo inabidi kwanza kuwakomesha mafisadi tanesco na serikalini wanaoingia mikataba kuwatoa damu wananchi. Tanesco ikiongozwa kiadilifu gharama za umeme zisizobebeka na wananchi zinaweza kushuka hata kwa nusu.
 
Shirika la tanesco liuzwe kwa shirika la umeme la Zambia. Watanzania tutaufaidi umeme kwa bei poa

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom