TANESCO kimewaka, jenereta lalipuka Ubungo!

Watakuwa wamezima makusudi kupotezea lile tukio lililotokea uwanjani wakati wa kukabidhiwa kombe
 
Jamani hii ni ajali kama zilivyo ajali nyingine. Ndiyo tuna mgao wa umeme ndani ya Tanzania lakini kwa hili ni ajali. Hakuna kilicho kamili chini ya anga hili, ni hekima kuelewa kwamba hata mitambo inapata ajali. Hakuna sababu za msingi za kuitupia lawama CCM na serikali iliyopo madarakani, hali kama hii inaweza kutokea hata Chadema ikiwa madarakani. Tuwe na mambo ya msingi ya kulalamika. Nawakilisha.

Lazima uwe na back up plan mkuu usitetee uzembe. Ni lini Tanzania imekua makini na kitu chochote? Ata mlipuko wa Mbagala ulikua bahati mbaya (ajali) kwani ni hatua gani zilichukuliwa ili kuepusha mlipuko mwingine ? The answer is none; baada ya muda mlipuko mwingine ulitokea and no body say a thing? Usitetee uzembe ndugu yangu; kama nchi inaongozwa na mtu ambaye anategemea mvua zinyeshe ndio Tanzania ipate umeme wa kudumu, then that tells you something. Try to connect the dots here!!!
 
Hahaha! haya ndio madhara ya kusikiliza radio na kuangalia TV ya CLOUDS Fareed ni presenter aliyebobea na huonekana CNN nakuandika pia vitabu.
anhaa, sasa Fareed Zakaria ame present mlipuko wa Ubungo leo?

Nadhani wewe ndio umedhurika na ulimbukeni na uzungukuku kiasi kwamba unashtuka na kucheka kusikia mtu hajali kumjua Fareed Zakaria, unasubiri mhindi aliyezamia Marekani ambae si ajabu hajawahi hata kufika Africa, let alone Tanzania, akuchambulie matatizo ya Africa wakati kwenu kumewashinda. Tuko na mada ya Ubungo umeme umelipuka jamani, who gives a rat's ass about Fareed Zakaria na wageni wa CNN?
 
Rudi nyuma kidogo upate wapi Fareed kaingia kwenye mjadala huu na relevance ya kum-quote.
 
Rudi nyuma kidogo upate wapi Fareed kaingia kwenye mjadala huu na relevance ya kum-quote.
Hana relevance yeyote hapa Fareed Zakaria wa CNN, aliingizwa pale nilipom quote Kichuguu, utadhani CNN wamechambua matatizo ya umeme ya Tanzania kwa kiiiiina! Tuko gizani saa hizi, I can care less about wageni wa Fareed Zakaria wa CNN, yeye mwenyewe ya kwao yamemshinda kakimbia ma Punjab huko.

Message is, usicheke mtu akikwambia hamjui au hajali kuhusu Fareed Zakaria, una sound kama limbukeni, sio kila Mtanzania anaamka asubuhi kuangalia Sunday shows za CNN za Marekani, mengi hayatuhusu, CNN hawaielewi crisis ya nishati Tanzania kama sisi wenyewe, tusisubiri foreigners watuchambulie matatizo yetu.
 
Duu, kweli wee Mkuu una akili sana. Nimekukubali.

Jamani TANESCO na wizara ya Ngeleja umeme umewashina. Mi na ona bora waanze tu kuuza kuni na mkaa tujue moja kuwa 'TZ bila umeme inawezekana' na turudi zetu kwenye ujima.
 
Hana relevance yeyote hapa Fareed Zakaria wa CNN, aliingizwa pale nilipom quote Kichuguu, utadhani CNN wamechambua matatizo ya umeme ya Tanzania kwa kiiiiina! Tuko gizani saa hizi, I can care less about wageni wa Fareed Zakaria wa CNN, yeye mwenyewe ya kwao yamemshinda kakimbia ma Punjab huko.

Message is, usicheke mtu akikwambia hamjui au hajali kuhusu Fareed Zakaria, una sound kama limbukeni, sio kila Mtanzania anaamka asubuhi kuangalia Sunday shows za CNN za Marekani, mengi hayatuhusu, CNN hawaielewi crisis ya nishati Tanzania kama sisi wenyewe, tusisubiri foreigners watuchambulie matatizo yetu.
Pole sana ndugu yangu;

Ni kweli; Zakaria hakuzima umeme Ubungo na wala hana relevance yoyote kwenye mlipuko huo. Hata hivyo, maoni yake kuhusu matatizo ya Afrika yana relevance kabisa; kuwa matatizo hayo yanatokana na uongozi mbovu wa juu, ambao huambukiza uongozi wa ngazi za chini. Nadhani unajua kuwa milipuko ya aina zote na mioto hapa Tanzania hutokana na uzembe wa viongozi katika ngazi husika, na wala hatujawahi kuona mtu yeyote akiwajibishwa kwa matukio ya namna hiyo. Bila kusubiri ripoti au tume wala nini, kuna probaility kubwa sana kuwa mlipuko huo wa Ubungo ni matokeo ya uzembe wa mtu fulani, ila kwa vile uzembe ni jadi iliyojengwa kutokana na viongoziwetu wa juu, basi jambo hilo litaishia vivyo hivyo. No Action!!.
 
Leo nilikuwa namsikiliza Fareed Zakaria wa GPS akiongea Afrika. xMmoja wageni wake alisema Afrika ina raslimali nyingi sana (ambayo ni kweli) lakini tangu bara hili lipate uhuru imekuwa na balaa la kuwa na uongozi mbovu. Ame single out nchi chache sana za hivi karibuni, Rwanda na Nigeria (sasa hivi), kuwa zimeanza kuona neema ya kuwa na uongozi mzuri. Alinichekesha sana aliposema kuwa uongozi mbovu ni kama ugonjwa unaoambukiza (contagious). Kiongozi mmoja wa juu akiwa mbovu basi wote wanaofuata chini yake wanakuwa wabovu. Tanzania nadhani tunasumbuliwa na ugonjwa huo.
Nadhani Fareed Zakaria alikuwa sahihi kabisa. Sasa kama nchi ama rais anashindwa kutatua issue ndogo kama umeme jiulize kuna kitu gani hiyo nchi itajivunia?
 
JK ameonekana ubungo songas plant, mafundi wa songas jasho tupu wanavyokimbizana umeme utarusi muda si mrefu ujao stay tuned
Ameonekana songas kwani yeye amekuwa fundi umeme kabeba spana namba ngapi.
 
Nimejaribu kuangalia uwanja wetu jinsi ulivyo mkubwa na maelfu ya watoto,walemavu na wazee,watu na mali zao na vibaka na purukushani zao,sasa unafikaje chini kutoka jukwaa la juu ukizingatia watazamaji wengine ni wageni pale uwanjani...inasikitisha sana na naamini kama Ngeleja hatajiuzulu kwa hili basi kamwe hakuna waziri atakayekuja kufanya hivi katika serikali hii ya wahuni
 
nimeota leo usiku kikwwete anajiuzulu na ngeleja pamoja baada ya wananchi kulalamika kwa kitendo cha kukata umeme wakati watu wanamsubiri mwali na maandano yameanzia taifa mpka ikulu kushinikiza mkuu na waziri wake wajiuzulu.
Afu ishu inakuja je nani atakaendesha hili gari lililojuu ya mawe? na nini kifanyike tutokane na hii adha?
 
Miaka 6 serikali haijui suluhu ya tatizo. Viongozi wapo busy kuwavutia wawekezaji. Hivi ukitaka kuwekeza Tz halafu ukaona kombe linatolewa kwa taa za NOKIA na mishumaa ya Pakistan utathubutu kutumbukiza mtaji wako? Utajiuliza kuna kiongozi anafikiri kweli, maana hao wa uwanja wa taifa hawakufikiria mgao na muda wa mchezo (plan B)

Hli la umeme lina hujuma! mara ukame, mara bwawa lina matope, mara songas wanasafisha mitambo, mara kudra za mwenyezi ili mradi tu kila anayemaliza chai na maandazi (bilion 19 vitafunio) anafungua mdomo. Tusubiri asubuhi hii Badra atakuja na shairi gani.

Richmond ilipoumbuliwa mgao ukapamba moto ili Dowans waingie kazini. Dowans waliposhtukiwa Al-hadaiwi akaja na kuongea na waandishi wa habari kinyemela,baada ya kuondoka songas ikaleta tabu, mara January akaenda Dowans. Iliposhtukiwa mgao ukauma. Mambo yakatulia kidogo, ikaja symbion mambo kimya, alipotua Hillary na kuthibitisha symbion mgao ukaanza kuuma tena.
Kuna jambo hatulijui lakini lipo !
 
waku hata mm niko kijiji sijaona umeme siku ya 4,huku ndo wamesahaulika kabisa!!!!
 
Ndugu zangu, TZ hakuna tatizo la umeme...hili mnaloita tatizo ni kitu kimetengenezwa na wajanja..ni biashara ya wakubwa kujipatia fedha...mtasikia mengie ngojeeni tu. Mbona tukiwa serious kwamba sasa tunaandamana umeme unapatikana?
Umesema ule ukweli mkuu!Mimi pia nilishasema tatizo la umeme halitaisha kwa sababu limefanywa kama dili la mafisadi.Ni kweli cdm wakichimba mkwara wa maandamano umemee utawaka na hakutakuwa na mgao mpaka tena pa kitulia wataanza tena.Nadhani wananchi tumelogwa na haya magamba maana kwa mwenye akili timamu hawezi kuvumilia huu upuuzi!
 
Kwanza kabisa si kweli kuwa kuna jenereta lililipuka jana Ubungo. Kama hiyo ingetokea basi ingekuwa ni disaster isiyosemekana. Kama mtu hajui sababu ya gridi kuachia ni vema akasema na si kupotosha.

Si kwamba natetea ama napingana na wachangiaji wengine bali nataka kuliweka wazi hili kiufundi.
Kilichotokea jana ni "trip" ya mojawapo ya mashine katika mojawapo ya mitambo ya kuzalishia umeme pale Ubungo. Hali hii ilisababisha "overload" katika gridi ya taifa. Grid Control operators walishindwa kuikabili hali hiyo kwa haraka (wangeweza kuondoa baadhi ya feeders ili kupunguza hiyo overload). Hii ikasababisha main grid breaker kuachia kwa sababu ya overload (na hiyo ni mojawapo ya protection).

Ku-energize grid kunatakiwa kuanzie na mtambo wa Kidatu ambao wengi tunajua kuwa kina cha maji kimepingua sana huko hivyo hilo lilikuwa tatizo lingine. Vituo vingine haviwezi ku-energize grid hadi pale Kidatu itakapowashwa.
 
hongera tanesco, heko chama cha magamba (CCM) asante richmond, daima tutakukumbuka dowans, symbion hata mama clinton anakujua..TANZANIA BILA UMEME INAWEZEKANA(!!???)
 
Back
Top Bottom