TANESCO Karatu, Arusha kukata umeme kila ifikapo saa moja jioni tatizo nini?

Mna tabia ya kukata umeme punde mvua inaponyesha. Hili tatizo lipo hasa Arusha mitaa ya Moshono.
Je mvua ikinyesha nonstop mwezi mzima tutabaki Bila huduma?
 
Mna tabia ya kukata umeme punde mvua inaponyesha. Hili tatizo lipo hasa Arusha mitaa ya Moshono.
Je mvua ikinyesha nonstop mwezi mzima tutabaki Bila huduma?
SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA KUKATIKA KWA UMEME

1. Utangulizi
Kwa muda mrefu kumekuwa na uelewa kutoka kwa wateja wetu kuwa kila umeme unapokatika TANESCO WAMEKATA. Nimeona ni vyema tukatoa
Maelezo kwa ufupi ili wateja wetu waelewe sababu za kiufundi na zisizo za kiufundi, zilizo ndani ya uwezo wa TANESCO na zisizo ndani ya uwezo wa TANESCO.

2. Sababu za TANESCO Kukata Umeme

TANESCO itakata tu umeme endapo kuna sababu zifuatazo BILA kuwataarifu wateja:-
a) Kuna mali inaungua (Mf. nyumba, kiwanda au mtambo)
b) Kuna mtu kanaswa na umeme.
c) Dharura emergencies (imeelezwa hapo chini namba 4)

3. TANESCO itakata umeme baada ya kuwataarifu wateja - Planned Interruptions endapo:-

a) Kuna matengenezo Kinga yaliyopangwa kufanyika ili kuimarisha miundombinu Planned Preventive Maintanance (Mf. Kubadili nguzo zilizooza, kubadili waya chakavu, kubadili transfoma ili kuongeza uwezo wa umeme nk)
b) Matengenezo ya kila mara Routine Maintanance (Mf. Kukata miti inayogusa line za umeme, kukagua vikombe na vifaa vingine kwenye line)
c) Kumuunga mteja mkubwa kwenye line ya msongo mkubwa wa umeme 11kV au 33kV

4. SABABU zinazoweza kusababisha umeme kukatika kwa dharura Emergency cases nyingi ni Unplanned Interruptions

a) Za kiasilia Natural Calamities (Mf. Radi kupiga transfoma, mvua au upepo mkali kuangusha nguzo, kukata waya, miti au minazi au matawi ya miti kuangukia line, mafuriko, wanyama kama komba, nyani, nyoka, kunguru kunasa kwenye mifumo ya umeme nk.

b) Hujuma za kibinadamu Sarbotage
(Mf. Transfoma kuibiwa mafuta, kuibwa nyaya za umeme, nguzo kuchomwa moto na kuanguka, nguzo kubwa kuibiwa vyuma na kuanguka, magari kugonga nguzo za umeme na kuanguka, malori marefu kwenda juu kukata waya za umeme, wateja kukata miti ikaangukia kwenye line nk.

Hizi ni baadhi tu ya sababu za msingi zinazoweza kusababisha umeme Kukatika. Hivyo ieleweke kuwa sio kila KUKATIKA KWA UMEME -TANESCO wamekata ni suala pana linalohitaji kujua sababu. Wakati mwingine kwa maelezo hayo hapo juu, Umeme unakatika hata TANESCO inabidi kufuatilia mifumo ili kujua sababu za kukatika.

5. Hitimisho
Tunajua jukumu la TANESCO ni kuhakikisha wateja wanapata umeme wa uhakika, pia ni ukweli kuwa mifumo mingi ya TANESCO ni ya muda mrefu hivyo inahitaji ukaratabati wa mara kwa mara na uwekezaji mkubwa ambao sote tumeona jitihada zinazofanywa na Serikali ili TANZANIA iwe na umeme wa uhakika.

Tunaomba umma uelewe sababu hizi na kuwa kama viongozi tunaamini hakuna mfanyakazi wa TANESCO anaweza kulihujumu Shirika kwa kukata umeme bila sababu au kukata umeme bila kufuata maagizo na utaratibu wa kukata line uliowekwa. Sio kila mfanyakazi au fundi anaweza kukata umeme. Upo utaratibu tena wakati mwingine wa kimaandishi unaompa fundi ruhusa, kabla ya kukata umeme. Kama yupo na anafahamika ( Kama baadhi ya wateja wetu wanavyotuhumu) tunaomba ushirikiano wenu ili tuweze kumshughulikia kwa taratibu za kisheria na tutakuwa tumelisaidia Shirika na serikali kwa ujumla.

TANESCO
Tunayaangaza Maisha Yako
 
Back
Top Bottom