TANESCO janga la taifa!

wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
7,454
4,374
pamoja na kutoa huduma mbovu kwa mgao na bei juu.

pia ni wakala wa ufisadi ktk iptl, richmond, dowans, escrow.
 
kwa nn hili shirika lisivunjwe na kutangaza mufilisi kama linashndwa kujiendesha lenyewe

kuliko kuendelea kutia hasara
 
Mletamada unatugharimu ujue?
Mimi na familia yangu tuskiapo tu! Neno Tanesco huwa tunatapika! (vomitin)
Ona hasara uliyonipa! Umetutapisisha Kuku unnecessarly !
 
pamoja na kutoa huduma mbovu kwa mgao na bei juu.

pia ni wakala wa ufisadi ktk iptl, richmond, dowans, escrow.
Hao jamaa wanatutoza shilingi 6,734 kwa kila mwezi, kwa kile wanachokiita service charge, ambapo ukizidisha mara 12, unakuta kila mteja wa TANESCO anatozwa shilingi 80,808 kwa mwaka!

Muda mrefu nimekuwa nikijiuliza hivi hii tozo tunayokamuliwa na TANESCO wakitumia jina la service charge, wao TANESCO wanazitumia kwa matumizi gani hasa?

Lakini baada ya hii skandali ya Escrow kubumbuluka ndiyo nimeanza kufumbuka macho, kumbe hicho kitu kinachoitwa gharama ya service charge ni dili ya watawala wetu wakishirikiana na shirika hilo la umeme, kufanikisha mpango wao wa kutuibia sisi wananchi mchana kweupe!
 
Shida sio shirika bali ni hii tabia ya kuwapa nafasi watu waliokwistaafu kuwa wajumbe na wenyeviti wa bodi ili waendeleze umchwa wao kwani walikotoka walizoea kula bila kunawa.
Pia kitendo cha wanasiasa kuruhusiwa kufanya biashara kunawafanya kuwatengenezea watendaji wa tanesco majanga ili wawaogope na kuwapa tenda zinazoiumiza hadi sasa.
Nini kifanyike ni kuifuta bodi yote na kuacha kuwateua wastaafu kuyaongoza mashirika ya umma na futa tenda zote zinazofanywa na makampuni ya wanasiasa na kununua kwa kufuata sheria ya manunuzi ya umma ili kuiokoa.
Zingatieni hayo na kutokuliuza shirika hilo kwani wanasiasa wana nia ya kulinunua kwa bei poa.
 
katika biashara inayolipa ni hii ya kuzalisha na kusambaza umeme, ukichukua familia ya kawaida inatumia kwh 100 kwa mwezi sawa na shs 36000 ukijumlisha na service charge ni shs 42,000/= kwa mwezi, ukiwa na mtambo kama wa iptl unauhakika wa kupata bil 42 kwa mwezi, wakati gharama za uendeshaji ni bil 4 tu! na hapo unatumia diesel.

kule vijijini watu walianza kusambaza umeme kwa kutumia majenereta ya 15kva, vijiji vyote vilivyoanza hii biashara vimepelekewa umeme wa muhongo tena unaunganishiwa kwa elfu 30 tu, lengo ni kuwapiga vita hawa wajasiliamali wa umeme.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom