TANESCO jana mmewaweka wakazi wa Ubungo masaa 14 bila umeme. Je, ni haki?

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,185
2,000
Nasikitishwa na haya TANESCO wanayofanya siku za hivi karibuni dhidi ya wakazi wa Ubungo.

Imekua ni kawaida yao kukatakata tu umeme tena kwa zaidi ya masaa ya kawaida.

Hivi unaweza vipi kukata umeme kwa masaa 14? Hivi kweli ndo tupo uchumi wa kati?

Kwanini mnadhorotesha juhudi za Mheshimiwa Rais? Ubungo ilipo mitambo ya umeme ya kisasa ni pa kukosa umeme kwa masaa 14 kweli?

Kusema kweli siku za karibuni wakazi wa Ubungo wamekua ni wahanga wakuu wa kero za kukatiwa umeme kwa masaa marefu zaidi nashindwa kuelewa ndo mambo gani haya TANESCO wanayafanya utadhani huo umeme tunapataga bure!

Aibu kwenu TANESCO! Mnakwamisha dhamira njema ya mheshimiwa Rais!
 

Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
1,992
2,000
Kama ni Planned maintenance sioni shida mkuu? Si mlipewa notice ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom