TANESCO Iringa wawajibishwe kwa kusababisha kifo cha mwanafunzi

Copy1

Member
Feb 10, 2016
96
143
Laiti kama wangeitikia wito wa zile simu toka kwa wananchi wanaoishi jirani na shule ya msingi Mkimbizi, zilizowapigia kwa wingi kuwaomba waje warekebishe nyaya zilizodondoka chini katika njia inayotumiwa na watoto leo tusingekuwa tunaongea haya

Laiti kama wangemsikiliza jirani yule aliyeamua kuwafuata hadi ofisini kwao na kuwaomba waje watoe hizo nyaya, leo tungekuwa tunawapongeza.

Ni hivi:-

Juzi Tarehe 15 March, kulitokea kifo cha mwanafunzi wa darasa la pili wa shule ya msingi Mkimbizi iliyopo Iringa manispaa.

Unaambiwa TANESCO walikuwa wamepigiwa simu zaidi ya mara 20, juu ya nyaya hizo, kuanzia jana yake (Tarehe 14) saa 9 mchana mara tu baada ya mvua kubwa kudondosha nyaya hizo.

Walipigiwa simu, na jibu lao lilikuwa ni tunakuja, siku ikaisha, asubhi mmoja wa majirani akaamka na kwenda ofisi za TANESCO Iringa ili kuwaomba waje warekebishe au watoe nyaya hizo zilizopo chini, lakini jamaa wakasema wapo kwenye kikao.

Masaa mawili baadae bado wapo kwenye kikao, na ilipofika saa nne ndipo majanga hayo yalipotokea.

Mungu amlaze pema peponi mtoto huyu, lakini, ili kutenda haki ni lazima serikali hii sikivu ifuatilie uzembe huu uliotokea na kutoa adhabu kali kwa wahusika wote, ili liwe fundisho.

Haiwezekani Mnapigiwa simu na hadii kufuatwa kwamba kuna dharura lakini bado mnaacha hadi masaa takribani 20 na zaidi yanapita na hakuna hatua iliyochukuliwa, sasa hapo nini maana ya Emergency?

Si kuna kitengo cha emergencey hapo? Eti kuna kikao mnakaa nini, nyaya zipo chini tangu jana na hakuna hatua mnayochukua?

TANESCO IRINGA WAWAJIBISHWE KWA KUCHANGIA KIFO CHA MWANAFUNZI HUYU
 
Back
Top Bottom