TANESCO inatunyanyasa sisi watu wa Vigwaza

rushanju

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
3,131
4,619
Kuanzi mwezi wa 5/2015 wapima njia ya msongo mkubwa wa umeme kutoka kinyerezi kwenda chalinze walipima nakutukataza tusifanye maedeleo yoyote kwa mdomo.

Chakushangaza hakuna karatasi yoyote waliyo tupatia ili baada miezi 6 tuweze kudai fidia. Ninapo andika uzi huu tunaelekea mwezi wa 3 tangia waondoke. Je endapo watatuletea hizo form walizo tuhaidi zitaanzia mwezi wa 5/2015 au zitaanzia tarehe zitakapoletwa? Je ni haki kuzuiliwa miezi 3 mitatu bila kuwa na ushahidi wowote?

TANESCO ni shirika kubwa na kongwe limepitia misukosuko mingi najua haliogopi malalamiko ya wanyonge kama sisi. Uchumi wa kati wa matumizi ya gas hauwezi kuja kwa mtindo huu. Kumbe watu wa mtwara walikuwa sahihi kugomea mradi huu wa gas.

Kusema kweli hamko wazi.

Nawengine wanaoguswa changia.
 
Ni kweli hata cc mlandizi hawakutupatia hushahidi wowote tupo tu hatujui atima yetu.asnte mleta mada
 
Tanesco ni wanyanyasaji sikatika mitambo tu, bali hata katika customer care. Ni matapeli hujawahi kusikia.
 
Si kweli kwamba tanesco wameshindwa kuyapatia ufumbuzi hayo matatizo,cha muhimu wasilisheni malalamiko rasmi kwa hatua na sio kulalamika mtandaoni,najua ni wasikivu na wanaelewa na watachukua hatua
 
Si kweli kwamba tanesco wameshindwa kuyapatia ufumbuzi hayo matatizo,cha muhimu wasilisheni malalamiko rasmi kwa hatua na sio kulalamika mtandaoni,najua ni wasikivu na wanaelewa na watachukua hatua

Ndugu yangu dunia ya sasa uwazi ndiyo njia pekee yakuonyesha matatizo ya wananchi. Kama ni kulalamika tumeisha lalamika sana. We basi tu. Inaonekana kuna harufu ya siasa!
 
Kaka Rushanju tunashukulu kwa malalamiko yako. Naomba nikukumbushe kuwa TANESCO sio Shirika la mtu binafsi ni Shirika la Umma na lina simamiwa kwa mujibu wa Sheria zote za nchi kuliko hata unavofahamu wewe. Tunakuomba kabla ya kulalamika mitandaoni na kuupotosha umma ni vyema hata ungeuliza kwenye Serikali yako ya Vigwaza kuhusu utararibu na kwamba mpaka sasa nini kinaendelea. Taratibu za kulipa fidia ya ardhi ina taratibu zake. Tunakuomba uisome kabla ya kulalamika. Tanesco walichokifanya ni hatua za mwanzo kabisa katika kutekeleza Sheria hiyo na Serikali ya Vigwaza wanalielewa hilo. Mwenye mamlaka ya mwisho kuhusu kubadilisha matumizi ya ardhi ni Mhe Rais. Pia ipitie sheria ya kuhamisha watu kwenye ma kazi yao " Land settlement" ndipo uje na hoja. Ubarikiwe sana.
 
Kaka paschal tanesco inafanya kazi kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu,hivyo ni vyema ukawasiliana na viongozi wa serikali katika eneo lako kuliko kupotosha umma kupitia mtandao,kwa kuwa hadi sasa tanesco waichokifanya ni hatua z awali tu,na pia zipo taratibu za kulipa fidia zipo na serikali hapo vigwaza wanalielewa hilo vzr.mm binafsi ni mkazi wa hapa sasa sioni hoja ya msingi hapa kwa kuwa ndio jambo lenyewe limeanza na mwenye mamlaka ya kubadili matumizi ya ardhi ni Rais pekee.
 
Nashukulu sana ndugu pinpilojr. Kwa ufafanuzi mzuri napia niwaombe watanzania tusiwe wepesi Wa kulaumu bila kuatilia taratibu ni hakika mtoa mada haujaenda ofisi za serikali za mitaa kuulizia taratibu zinefika wapi. Na pia tanesco ni shilika la uma ambalo liko chini ya serikali kwaiyo linafata sheria na taratibu za nchi jamani tupunguze lawama zaid I tunapaswa kulisaidia kulipa shirika letu ili liweze kufanya vizuri zaidi. Ni hayo tu kwa leo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom