Tanesco inapoteza hela nyingi kwa siku , mfumo wa luku haufany kazi. Jengo!

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
843
1,363
Kutokana na jengo kubomolewa mifumo ya luku imekuwa dusturbed na haifanyi kazi toka jana saa 2 asubuh. Hii ni kutokana na upishaji wa jengo kubomolewa. Tanesco ambayo huwa inauza takribani bil3.5 za luku kwa siku inatarajia kukosa kiasi kikubwa mpaka mfumo utakapo kaa sawa siku ya jumanne

Shida hizi
 
Kwamba una hela ya kununua huduma lakini huduma haipo.

Nina hela za kuweka LUKU kwenye nyumba yangu, lakini tangu jana malipo ya LUKU yameshindikana.

Siyo tatizo letu ni tatizo la sevice provider. Huduma ya LUKU haipo kwa siku 2 sasa. Huipati kwa mtandao wowote.

Huwezi ku charge simu, huoni TV, kwa ujumla hali siyo nzuri kwa wote walioishiwa LUKU jana na watakaoishiwa wakati wowote hata sasa.
 
Mkuu jaribu mara kwa mara kununua kwenye simu, Mimi jana usiku nilibahatisha baada ya kujaribu kama mara tano hivi kila baada ya dakika 15-20, Ndio nchi yetu hiyo tuvumilie.
 
Kweli huduma hii haipatika na sijui kama ni baadhi ya maeneo au ni nchi nzima, na hii ni matokeo ya kuumbuliwa mchana kweupe kwani walijitahidi Sana kutudanganya ya kuwa kuvunjwa kwa jengo la Tanesco haitoathiri shughuli zetu za kila siku kitu ambacho siyo kweli.
 
Hii nchi wanaijua wenyewe. Tuliambiwa umeme unakatika kwa vile wanabadilisha mitambo
Sasa LUKU haipatikani na hapo sijui wana badilisha network!!!????¿ TANESCO ni moja kati ya mashirika yanayo jitaji kubomolewa na kuanza upya...
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUHAMISHA MIFUMO YA LUKU

Tunawataarifu Wateja wetu kuwa, kutokana na kazi ya ubomoaji wa jengo la Ofisi za TANESCO Makao Makuu, Ubungo linaloendelea, leo Desemba 09, 2017 kutakuwa na kazi ya kuhamisha Mifumo ya LUKU (Servers).

Kutokana na kazi hiyo Wateja wetu hawataweza kununua umeme kati ya saa 4 usiku hadi saa 7 usiku.

Ahsanteni kwa ushirikiano wenu.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo:
Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd

twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Desemba 09, 2017
 
Kwa aloyeshuhudia servers zikihamishwa atuambie
 
Kwamba una hela ya kununua huduma lakini huduma haipo.

Nina hela za kuweka LUKU kwenye nyumba yangu, lakini tangu jana malipo ya LUKU yameshindikana.

Siyo tatizo letu ni tatizo la sevice provider. Huduma ya LUKU haipo kwa siku 2 sasa. Huipati kwa mtandao wowote.

Huwezi ku charge simu, huoni TV, kwa ujumla hali siyo nzuri kwa wote walioishiwa LUKU jana na watakaoishiwa wakati wowote hata sasa.

Afadhali umeleta uzi bwana ili tujadiliane....

Mimi nilishtuka jana around saa 12jioni kuwa nimebakiwa na unit 1.5 nikajaribu kununua kwa M-PESA....

Hela ilikwenda bila kupata "tokens" na baada ya kama masaa mawili, MPESA wakarudisha hela na ujumbe wa...

"huduma hii haipatikani kwa sasa, tafadhali jaribu tena badaye"...

Nimejaribu several times, the same naletewa ujumbe huu huu...

Tumelala na kuamka umeme ukawa umeisha kabisa na nyumba yote kimya. Nimejaribu kununua tena leo asubuhi ya leo around saa 3, nikaletewa ujumbe huohuo....

Nikawapigia Vodacom kutaka kujua tatizo ni la mtandao wao wa MPESA au ni system LUKU - TANESCO. Wakasema, system yao haina tatizo ila haina mawasiliano na mtandao wa LUKU....

Nikaenda kwenye vibanda vya MaxMalipo, nikatoa hela lakini jamaa hawakunipa umeme lakini pesa ikawa imemezwa kwa maelezo kuwa "system iko down"...

Na kwa kuwa nilikuwa nawahi ibadani kanisani, ilibidi niachane na hiyo kitu kwa wakati ule. Nimetoka na kupitia huko kuchukua umeme wangu, ndo nimekuta wameshaprint risiti yenye tokens...

Kuja nyumbani kuingia tokens kwenye Luku meter yangu, lahaula kumbe umeme nao ulishakatika toka sijui saa 5asb na haieleweki utarudi lini na saa bhaji!!.

Ama kweli, Tanesco ni sheedah kwelikweli....

Sasa niko na kijikaratasi tu cha namba zile 20 za kuingiza kwenye LUKU yangu nasubiri na game za leo za EPL ndo kali kinoma....

Arsenal vs Southampton

Liverpool vs Everton

Manchester United vs Manchester City...
 
Kwani hawakujiandaa. Wasituletee mambo ya kivivu. Maana walikuwa na notisi
 
Back
Top Bottom