TANESCO ilishindwa kufikia malengo ya kuwaunganisha wateja waliolengwa mwaka 2018

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Uunganishwaji wa wateja katika huduma muhimu ya nishati ya umeme na TANESCO kumeonesha kupungua kutoka mwaka 2015/16 na kufikia chini ya malengo mwaka 2017/18 kabla ya kuanza kupanda tena mwaka 2018/19.

TANESCO wametaja kutokuwepo kwa malighafi kuwa ni sababu ya kushindwa kufikia malengo mbali na kuwa na mradi wa umeme vijijini(REA) ambapo wametaja malighafi kuchelewa, uhaba wa usafiri, bajeti finyu na kutokuwa na nguvu kazi.

Hata hivyo katika uwezo walionao wametaja kumiliki mkongo na rasilimali huku wakiwa na washindani wachache kutokana na sheria.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom