TANESCO: Ili upate umeme kwa mwezi Agosti, nunua wa zaidi ya Tsh. 2,000/-

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Shirika Umeme nchini (TANESCO) limesema Wanachi hawataweza kununua umeme wa chini ya Tsh. 2,000 kwa mwezi huu

Limesema ni ili Wananchi waweze kulipa kodi ya majengo ya mwezi Julai (Tsh. 1,000) na Agosti (Tsh. 1,000)

Shirika hilo limefafanua kuwa Tarehe 20 Agosti ni kuanza kwa makato lakni kodi ni kwa ajili ya mwaka huu bajeti ambao umeanza mwezi Julai 2021

AD58F2F9-62B0-4793-9531-09962CB648A7.jpeg
 
Kupitia ukurasa wake wa Twitter shirika la umeme Tanzania limewataka watanzania kununua umeme zaidi TSh 2000 ili kupata unit za umeme.

2000 hiyo itakatwa kama tozo ya nyumba ya mwezi wa 7 na wa 8

Tanesco.jpg
 
Daah! Nilitaka kununua units 16 za 2000 nashangaa mauza uza haya kumbe yashaanza kufanya kazi.. 😭

Screenshot_20210821-122458.png
 
Shirika Umeme nchini (#TANESCO) limesema Wanachi hawataweza kununua umeme wa chini ya Tsh. 2,000 kwa mwezi huu

Limesema ni ili Wananchi waweze kulipa kodi ya majengo ya mwezi Julai (Tsh. 1,000) na Agosti (Tsh. 1,000)

Shirika hilo limefafanua kuwa Tarehe 20 Agosti ni kuanza kwa makato lakni kodi ni kwa ajili ya mwaka huu bajeti ambao umeanza mwezi Julai 2021

View attachment 1901215
Mimi nimelipia kodi ya majengo kwenye ofisi za TRA mwezi January mwaka huu na risiti ninayo,Sasa mmetangaza kukusanya Kodi ya majengo kupitia LUKU, mifumo hii miwili ya Tanesco na TRA inaweza kugundua kuwa mnanichaji mara mbili? Huu si ni wizi wa kitaasisi ulioidhinishwa na Bunge?.
 
Wakikujibu unitag
 
Swali langu, ni je hiyo 2,000 inakatwa kila ukinunua umeme au ukishakatwa mara ya kwanza ndani ya mwezi husika ukinunua tena hukatwi mpaka mwezi ujao?
 
Napendekeza kila mtanzania akatwe 1,000 kila mwezi kama kodi ya kumiliki laini. Hii itaongeza mapato ya nchi
 
Endelea kuwa busy na CHADEMA tu nasikia kuna kulipia 1,000 kama kodi ya kumiliki laini na pia Idara ya maji nayo kuna kama 2000 inawekwa pale.
Mwaka huu lazima tuheshimiane tu. Ww endelea kuwa busy na CHADEMA tu.
Bado Visimbusi navyo vinaongeza bei.
Ukijakushituka 100mb unanunua kwa shilingi 10,000
Majinga chadema yanasema anaupiga mwingi
 
Back
Top Bottom