Tanesco Ifunda: Ni kweli sayansi eneo hili imechemka kwenye uchawi?

Hii kitu niliisikia Bungeni. Mbunge wa mali asili na utalii akisistiza tutangaze kile kama kivutio cha utalii.
Mkuu ningepata hayo maelezo ya miti kukatwa leo kesho inarudi kama ilivyokua Mwanzo nadhani hapo unataka kunisafirisha baba. Ninaamini kabisa hili tukio lingekua moja ya 7 wonders of the world! au nimekosea?
Hapana si kweli kwamba miti ikikatwa leo inaota kesho yake.
 
Kwanini wana JF tusifanye utafiti wetu wa kwanza kisayansi. Watu waanze kuandaa proposal ya utafiti huo tukifsanikiwa tunaeza kutoa jibu moja kwa jamii yetu kama tulivyofanya kwenye DOWNS, RICHMOND nk
 
Mimi nataka kuleta researchers tuje tu film documentary, hapo tuntest hizi sayansi za kiafrika.Nitajieni exact location. Mimi siamini supernatural powers za aina yoyote.

Hii itakuwa njia nzuri ya kutest hizi habari scientifically. Inawezekana kuna mi Higgs Bosom particles ime concentrate hapo kwenye dimension ya 26 wabongo tunadhani uchawi.

Arthur C. Clarke alisema "Any sufficiently advanced technology is indistinguishablee from magic" . Pengine tunachosema ni uchawi/ suprnatural phenomena ni teknolojia tusiyoijua tu.

But most probably hamna chochote.
 
That is my village nawakati umeme unapita maeneo hayo nilikuwa mwanafunzi. Pale chini kuna njiapanda inaitwa njiapanda ya Mlolo. Inakwenda shule moja inaitwa Wenda.
Back to the point; Maneno hayo hata sisi wakati tunakuwa tulikuwa tunayasikia. Ila ukweli kabisa hakuna anaweza kutoka mbele na kuthibitisha labda TANESCO tu. Ninachokumbuka ni kuwa umeme ulivyofika pale process ilichukua muda mreefu sana kuliko maeneo mengine na baadhi ya watu wakasema wameshindwa kufikia muafaka na wenye makabuli. Kuhusua ajali huenda limekuwa eneo baya miaka ya hivi karibuni maana pale barabara imenyooka mpaka unavyokaribia Tanangozi.

Mkuu mimi siamini nguvu za giza kabisa ila kama kweli ni kijijini kwako na hujui sababu nitakulaumu sana. akaulingana na maelezo yaliyotolewa hapa nadhani mtu yeyote mdadisi atashawishika kujua kulikoni? Ulaya waliendelea kwa ajili ya udadisi...
 
The dude is using understatements to say "There is nothing supernatural here"
 
Mkuu mimi siamini nguvu za giza kabisa ila kama kweli ni kijijini kwako na hujui sababu nitakulaumu sana. akaulingana na maelezo yaliyotolewa hapa nadhani mtu yeyote mdadisi atashawishika kujua kulikoni? Ulaya waliendelea kwa ajili ya udadisi...
I will take trouble ya kufuatilia. Maana nyaya huwa ninaziona pale. Nina miaka kadhaa sijafika huko lakini hii hainiondolei wajibu wa kufaham nini kilitokea. Nitafuatilia kwa wenye makaburi au wazee wa kijiji then nitakuja na jibu. Ukweli kabisa ni udhaifu kutokuweza kutoa maelezo ya kutosha juu ya eneo husika.
 
Next level tunashukuru kwa mchango wako ila ulichoeleza sio kweli. Ukweli ni huu nyaya za umeme zilipitishwa vizuri bila matatizo yoyote, hakuna nyaya zilizo katika wala mfanyakazi aliyekufa. Kituko ilikuwa ni baada ya kuwasha umeme, upande mmoja wa makaburi umeme uliwaka upande wa pili umeme haukuwaka. Baada ya kupima iliionekana kabla ya kuvuka makaburi umeme upo ila baada ya kuvuka tu umeme hakuna. Ndio wakaamua kuchepusha nguzo upande wa pili wa barabara umeme ukawaka hadi leo.
 
here say!!!!! nilisikia kuwa mpango ulikuwa ni wa kuhamisha makaburi lakini ilishindikana baada ya negotiations za muda mrefu na wale ndugu (line ya machifu). pia nilisikia kuwa mwanzoni nyaya zilifungwa kama kawaida kupita juu ya yale makaburi lakini umeme haukuweza kupita. waligundua ni pale baada ya ku trace all the way. tehetehe
hivyo that was the option
Pale hamna cha Mpango wala nini maamuzi ya serikali hayawezi kuzuiwa na raia tu" Unamkumbuka ASKOFU kakobe na waumini waliogoma kabisa na kujitolea kulinda!
Kimsingi Pale kuna Lile Kaburi kuna roho iliyosimikwa na kama kuhamishwa basi ni kwa utaratibu usio wa kughushi "Matambiko N.k"
1. Kabla ya Tanesco tanroads walifanya dharau na kutaka kupitisha kwa nguvu, Kuna caterpiller Vijiko vilivunjika na baadaye lilianguka na kuright off palepale lakini kipande cha kaburi hakikutoka hata mchanga tu! wakaipitisha pembeni kidogo bila kuliathiri Kaburi lile.
2. Tanesco nao waliweza kupitisha nyaya kwa shida sana na kwa ubishi wa kibabe Kipindi hicho wawekaji walikuwa wanapandisha nyaya na matusi kibao! hivyo walikuwa tayari wameshakosea tangu mwanzo (matusi si tatizo). umeme ulikwenda lakini kufika pale haukuendelea. Na ndipi ujanja hamna ilibidi wakwepeshe Kuelekea upande mwingine.
3. kuna gari lingine liliwahi kuanguka pale wakati huo wa kutengeneza barabara likiwa na mbishi mmoja nalo lilikwisha kabisa lakini hakuna kipande cha kaburi kilitoka.
So, thats my here say about kaburi la Tanangozi Iringa japo sijui kwa sasa kama nguvu hiyo bado ipo, lakini that was the true story!
 
Next level tunashukuru kwa mchango wako ila ulichoeleza sio kweli. Ukweli ni huu nyaya za umeme zilipitishwa vizuri bila matatizo yoyote, hakuna nyaya zilizo katika wala mfanyakazi aliyekufa. Kituko ilikuwa ni baada ya kuwasha umeme, upande mmoja wa makaburi umeme uliwaka upande wa pili umeme haukuwaka. Baada ya kupima iliionekana kabla ya kuvuka makaburi umeme upo ila baada ya kuvuka tu umeme hakuna. Ndio wakaamua kuchepusha nguzo upande wa pili wa barabara umeme ukawaka hadi leo.
Mligo huo ndo ukweli kwa kifupi.
Jamani hizi zilikuwepo ila dhambi zimezidi ndo maana zinayeyuka. Hawa watu tulikuwa tunaweza kuomba hata mvua, leo bure kabisa huwezi hata ufanyeje
 
1992 kulikuwa na mradi kupeleka umeme Tanangozi kutoka kitwilu Iringa,Sio kweli umeme haukuweza kupita au watu walikufa au miti ilikatwa na siku ya pili kuota,ki michoro umeme ulitakiwa upite juu ya makaburi hayo,kuna supervisor mmoja mwenye asili ya kihehe aliyekuwa anasimamia mradi huo anaitwa Said Nyanguli yeye alimshauri Menjeja wa Tanesco wakati ule Ndg Kileo wa kuwepe yale makaburi kwa madai ya yule supervisor kipindi barabara ya Tanzam inatendegenezwa miaka ya 70 kuna makatapila yaliharibika watu walikufa ,
Kwa hiyo isije wakati wanaptisha nyaya zao yakatokea matatizo ndipo meneja huyo akakubaliana naye wa ya kuwepo hayo makaburi,meneja huyo amestaafu Tanesco na anaishi Iringa ndiye anaye jua ukweli wote.
Sio kweli kwamba umeme uligoma au kuna watu walikufa .waliya kuwepa tu yale makaburi
 
Wewe si unajua wabongo tunavyopenda kupandishia disc za mambo ya uchawi, hata mtu akiona image yake kwenye kikombe cha maji anakwambia kuna kitu kaona.
 
hope kakobe anataka kutumia fomula hiyo sasa kwa tanesko hiyo story naisikia sana watu wa barabara walishindwa kuyaamisha kwa mauzauza waloyaona tanesko nao same walewalozikwa pale bado roho roho zao zipo active bana kakobe ajifunze tecknolojia hiyo simple
 
jamani, pale umeme ulishidwa kupita kabisa nhdo maana waliuchepusha,hata bara bara yasemekana mchezo ulikuwa ni huo huo,na kuna gari liliwahi kuangukia pale gari lilikuwa nyang'anyang'a lakini kaburi hata rangi tu haikuchubuka
 
Hizi habari za kizushi na myths tu. Hazina ukweli wowote! Umeme pale unapita bila matatizo. Ila ni migogoro tu ya watu wenye mawazo kama kakobe. Kwenye issue ya kakobe kama TANESCO wange bow down na kukubali yaishe basi baadaye ingekuwa stori kuwa askofu kakobe alizuia umeme kupita pale.

Hakuna mahali duniani kitu kama hiyo ipo. Kama supernatural zipo na ziwepo lakini si kwenye hiyo case ya makaburi. Kwa sababu ya ku-preserve tu historia ambayo iko associated na makaburi hayo na ikatokea contractor alikuwa ni anayejali historia na mila za watu hakupenda kushindana na raia. Gharama ya ku divert ile line ya umeme ni ndogo ukizingatia migogoro ambayo ingetokea. Watu huwa wanachukua nafasi kuhujumu na kudai eti ni mauza uza.

Hakuna kitu kilichozuia umeme kupita juu ya yale makaburi ni maamuzi ya contractor tu aliyejenga kutopenda ligi na ubishi. Tatizo letu watu mara nyingi mtu akizungumzia kitu kinachosema hapa ni uchawi au nguvu za ziada zilitumika watu huwa hatuhoji, tunakubali whole sale bila kuuliza kwa sababu hizi imani zimejikita vichwani mwa watu wengi hadi inatia kinyaa.
 
Naona Mods wanasinzia huu ni udaku sawa tu na Magogoni wanayomtumia yahaya. Hayo makaburi yapo pale zaidi ya miaka 40. Tanzania bila ushirikina inawezekana waambieni wabunge/mawaziri waache safari za usiku kwenda Bagamoyo et al.

Mods peleka kwenye udaku hii.
 
Hizi habari za kizushi na myths tu. Hazina ukweli wowote! Umeme pale unapita bila matatizo. Ila ni migogoro tu ya watu wenye mawazo kama kakobe. Kwenye issue ya kakobe kama TANESCO wange bow down na kukubali yaishe basi baadaye ingekuwa stori kuwa askofu kakobe alizuia umeme kupita pale.

Hakuna mahali duniani kitu kama hiyo ipo. Kama supernatural zipo na ziwepo lakini si kwenye hiyo case ya makaburi. Kwa sababu ya ku-preserve tu historia ambayo iko associated na makaburi hayo na ikatokea contractor alikuwa ni anayejali historia na mila za watu hakupenda kushindana na raia. Gharama ya ku divert ile line ya umeme ni ndogo ukizingatia migogoro ambayo ingetokea. Watu huwa wanachukua nafasi kuhujumu na kudai eti ni mauza uza.

Hakuna kitu kilichozuia umeme kupita juu ya yale makaburi ni maamuzi ya contractor tu aliyejenga kutopenda ligi na ubishi. Tatizo letu watu mara nyingi mtu akizungumzia kitu kinachosema hapa ni uchawi au nguvu za ziada zilitumika watu huwa hatuhoji, tunakubali whole sale bila kuuliza kwa sababu hizi imani zimejikita vichwani mwa watu wengi hadi inatia kinyaa.
Ndugu yangu hivi selikali ya tz unayoifahamu tena enzi za nyerere ingeshindwa kuling'oa kabuli tu eti kisa ndugu hawataki? na umeme unapita juu na kaburi liko chini vinahusiana nini? amini usiamini lile tukio ni la ukweli.tena watu wa hapa Iringa walikuwa na hamu barabara itanuliwe mbaka kule waone itakuwaje safari hii?
 
4.jpg

Kaburi la Martin Kiyeyeu eneo la Malolo kilomita 30 kutoka Iringa kuelekea Mbeya ni maarufu kwa kisa cha kweli pale mafundi wa umeme waliposhindwa kupitisha waya wa umeme juu ya kaburi hilo. Walipojaribu kufanya hivyo waya zilikatika. Ndio sababu unaweza kuona hapo mbele waya zimekatisha barabara! Haya kuna wataalamu wa kutupa ufafanuzi wa kisayansi?! Kwa hiyo sayansi ya nguvu ya Giza ina nguvu kuliko sayansi ya Mzungu?
Je ni kweli hili kaburi limeondolewa?

Back
Top Bottom