Tanesco-hawajui lini utaisha mgao wa umeme!!!!

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,534
2,000
Tanesco: hatujui mgawo utaisha lini Send to a friend Thursday, 02 December 2010 21:28 0diggsdigg

badra%20masoud.jpg
Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud

Elizabeth Ernest na Mwanaidi Abasi
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema haijulikani ni mgawo wa nishati hiyo ambayo mkoani Dar es Salaam, imekuwa ikipatikana kwa njia hiyo, utamalizika lini.

Kauli hiyo inakuja huku mgano huo ulioathiri shughuli mbalimbali zikiwezo za uchumi ambazo uendeshaji wake umekuwa ukitegemea umeme, ukiwa umeingia katika wiki ya pili.

Mgawo huo ulioanza takribani wiki mbili zilizopita unadaiwa kuwa umesababishwa na ubovu wa mitambo katika gridi ya taifa.

Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud aliiambia Mwananchi juzi kuwa mgawo huo utamalizika wakati wowote bila kutaja muda halisi.

"Mgawo utamalizika muda wowote kuanzia leo (juzi) kwa sababu sijui ni lini mitambo iliyoharibika itakuwa imekamilika,"alisema.

Alisema mgawo huo umetokana na ubovu wa mitambo ya umeme iliyoko Tegeta, jijini Dar es Salaam na kwamba mafundi wanaendelea na jitihada za kuifanyia matengenezo ya mitambo hiyo.

"Kwa sababu bado mitambo inaendelea kutengenezwa, sijui mafundi watakamilisha lini matengenezo hayo na ni vigumu kwa mafundi kusema kama matengenezo hayo yatamalizika lini,"alisema.

SOURCE:Mwananchi 03/12/2010

:target:
Mimi nashangaa sana kwa nchi kubwa kama Hii Kucentralize kila eti kiko Dar Es Salaam, Hii inatia wasi wasi sana juu ya upeo wa viongozi waliong'ang'ania dola, Tatizo kama hilo lililotoke hapa Dar, Ingewezekana kabisa lisiathiri Shughuri zingine kUle Dodoma, Mwanza, Arusha nk.
Tuna mabwawa, Mi Diesel power Plants, Songosongo nk. Lakini naona vyote vinaelekezwa Bagamoyo/Dar
Nimewahi pia kusema mengi watu kuhusiana na mambo haya ya Int. Airports kuwepo Mwanza, Viwanda nk Watu wakapaka wakisema natangaza Ukanda!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom