YeshuaHaMelech
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 2,597
- 37
Elizabeth Ernest na Mwanaidi Abasi
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema haijulikani ni mgawo wa nishati hiyo ambayo mkoani Dar es Salaam, imekuwa ikipatikana kwa njia hiyo, utamalizika lini.
Kauli hiyo inakuja huku mgano huo ulioathiri shughuli mbalimbali zikiwezo za uchumi ambazo uendeshaji wake umekuwa ukitegemea umeme, ukiwa umeingia katika wiki ya pili.
Mgawo huo ulioanza takribani wiki mbili zilizopita unadaiwa kuwa umesababishwa na ubovu wa mitambo katika gridi ya taifa.
Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud aliiambia Mwananchi juzi kuwa mgawo huo utamalizika wakati wowote bila kutaja muda halisi.
"Mgawo utamalizika muda wowote kuanzia leo (juzi) kwa sababu sijui ni lini mitambo iliyoharibika itakuwa imekamilika,"alisema.
Alisema mgawo huo umetokana na ubovu wa mitambo ya umeme iliyoko Tegeta, jijini Dar es Salaam na kwamba mafundi wanaendelea na jitihada za kuifanyia matengenezo ya mitambo hiyo.
"Kwa sababu bado mitambo inaendelea kutengenezwa, sijui mafundi watakamilisha lini matengenezo hayo na ni vigumu kwa mafundi kusema kama matengenezo hayo yatamalizika lini,"alisema.
Masoud alisema sababu kubwa ya kufanyika kwa mgawo huo ni ubovu wa mitambo ambayo kwa sasa iko katika matengenezo na kwamba itakapokamilika ndipo watakapo sitisha mgawo huo.
Hivi karibuni shirika hilo lilitoa taarifa kuwa mgawo wa umeme, umetokana na kuharibika kwa baadhi ya mitambo ya Songas iliyopo Ubungo, jjini Dar es Salaam.
Pia taarifa hizo zilisema kupungua kwa kina cha maji katika mabwawa ya Pangani na Kihansi na kuisha kwa mafuta katika mtambo wa IPTL, kumechangia kuongezeka kwa tatizo hilo.
Source: