Tanesco: hatujui mgawo utaisha lini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco: hatujui mgawo utaisha lini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by YeshuaHaMelech, Dec 3, 2010.

 1. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Elizabeth Ernest na Mwanaidi Abasi
  SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema haijulikani ni mgawo wa nishati hiyo ambayo mkoani Dar es Salaam, imekuwa ikipatikana kwa njia hiyo, utamalizika lini.

  Kauli hiyo inakuja huku mgano huo ulioathiri shughuli mbalimbali zikiwezo za uchumi ambazo uendeshaji wake umekuwa ukitegemea umeme, ukiwa umeingia katika wiki ya pili.

  Mgawo huo ulioanza takribani wiki mbili zilizopita unadaiwa kuwa umesababishwa na ubovu wa mitambo katika gridi ya taifa.

  Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud aliiambia Mwananchi juzi kuwa mgawo huo utamalizika wakati wowote bila kutaja muda halisi.

  "Mgawo utamalizika muda wowote kuanzia leo (juzi) kwa sababu sijui ni lini mitambo iliyoharibika itakuwa imekamilika,"alisema.

  Alisema mgawo huo umetokana na ubovu wa mitambo ya umeme iliyoko Tegeta, jijini Dar es Salaam na kwamba mafundi wanaendelea na jitihada za kuifanyia matengenezo ya mitambo hiyo.

  "Kwa sababu bado mitambo inaendelea kutengenezwa, sijui mafundi watakamilisha lini matengenezo hayo na ni vigumu kwa mafundi kusema kama matengenezo hayo yatamalizika lini,"alisema.

  Masoud alisema sababu kubwa ya kufanyika kwa mgawo huo ni ubovu wa mitambo ambayo kwa sasa iko katika matengenezo na kwamba itakapokamilika ndipo watakapo sitisha mgawo huo.

  Hivi karibuni shirika hilo lilitoa taarifa kuwa mgawo wa umeme, umetokana na kuharibika kwa baadhi ya mitambo ya Songas iliyopo Ubungo, jjini Dar es Salaam.

  Pia taarifa hizo zilisema kupungua kwa kina cha maji katika mabwawa ya Pangani na Kihansi na kuisha kwa mafuta katika mtambo wa IPTL, kumechangia kuongezeka kwa tatizo hilo.
  Source:
   
 2. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hadi ufisadi utakapoisha nchi hii
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  These ******!!!!!!!!
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  I dont buy this crap kwani mjini hapa hakuna mafuta kiasi cha kuifanya mitambo IPTL ishindwe ku-operate au waseme tu wameshindwa kuwalipa hela za mafuta
   
 5. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kazi kweli...na bado tuna miaka mitano.
  Mungu atusaidie kuvumilia haya maumivu wakati tukitafuta jinsi ya kuondokana na umaskini ktk nchi tajiri kama hii.
  One day...the day is coming!
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Kwenye kamapeni CCM walisemaje kuhusu migao ya umeme?
   
 7. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2010
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Hii inaonyesha jinsi gani watu wanavyofanya kazi kwa kubahatisha;kwasababu kitaalamu hawa mafundi wanatakiwa waitathmini kazi kujua mahitaji na kujua itachukua muda gani kutekeleza kazi hiyo.Sasa hii habari ya kuwaambia wananchi hatujui muda gani tatizo litakuwa limeisha si kauli nzuri hata kidogo.
  Na kama ni hivyo ina maana Tanesco hawajui tatizo ni nini na wanatakiwa kufanya nini!!Labda ili kuwepo na ufanisi ni bora shirika libinafsishwe na kuruhusiwe wawekezaji kataika sekta ya umeme kama yalivyo makampuni ya simu dhidi ya TTCL;hapa nafikiri akili zitarudi katika mstari.
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu TANESCO iliacha kuendeshwa na wataalamu toka alipokufa yule SALVATORY MOSHA miaka ile ya kale....Baada ya hapo wanasiasa waakichukua Rasmi wakiongozwa na JK huyuhuyu mnae mlilia hapa
   
Loading...