Tanesco hapakaliki.........Ni vita ya wazamani, wapya yaiva............ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco hapakaliki.........Ni vita ya wazamani, wapya yaiva............

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 14, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Ni vita ya wazamani, wapya yaiva Tanesco
  Monday, 13 December 2010 23:43

  Mwandishi Wetu

  BAADHI ya watendaji wa ngazi za juu ndani ya Shirika la Umeme (Tanesco) wameingia katika vita ya kuwania madaraka baina ya vigogo wa muda mrefu ambao wanabezwa kuwa ni SLP na wapya maarufu kama dotcom, Mwananchi imedokezwa. Habari kutoka ndani ya Tanesco zinadai kuwa mvutano huo umeanza kujitokeza kwenye mgawanyo wa madaraka, hasa idara ya mawasiliano ambako kila kundi linataka amtu wake aongoze idara hiyo muhimu.

  Kundi la kwanza ni la wafanyakazi wa siku nyingi ambao wamebatizwa jina la Sanduku la Posta, maarufu kama SLP, na jingine ni la wale walioajiriwa miaka ya karibuni ambalo limebatizwa jina la dotcom, likimaanisha matumizi ya mawasiliano kwa njia ya mtandao wa inteneti. Habari zaidi zinadai kwamba chini ya uongozi wa mpya wa Mkurugenzi Mkuu, William Mhando baadhi ya wakongwe walioondolewa katika nafasi za menejimenti na uongozi wa Dk Idris Rashid wanashinikiza kurejea katika nafasi walizokuwa nazo awali. Baada ya kuteuliwa kuongoza shirika hilo mwaka 2006, Dk Rashid alifanya uhamisho mkubwa wa maofisa wake waandamizi kwa maelezo kwamba walikuwa wemelundikana kwenye ofisi za makao makuu bila kazi yoyote.

  “Wengi wanaotaka kurejea hapa ni wazawa waliohamishiwa mikoani na Dk (Idris) Rashid, kwa hiyo huyu mkubwa mwenzao karudi... karudi na wao wanataka warudi. Hapa vita ni kubwa sana kati ya hao dotcom na SLP,” alibainisha mmoja wa watumishi anayefanya kazi makao makuu ya shirika hilo. Meneja uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alipoulizwa kuhusu hali hiyo alisema hawezi kuzungumzia mambo ambayo alidai kwamba “hayana ushahidi wowote”. “Hayo mnayosema mmeyapata wapi; mimi siyajui kama kuna ushahidi wa hayo makundi mnayodai kwamba yapo hapa kwetu basi twambieni…” alisema Badra na kuongeza kuwa Tanesco si mahali pa makundi.

  Wakati Badra akikanusha kuwepo kwa makundi hayo, idara anayoiongoza ndiyo inayodaiwa kukumbwa na jinamizi hilo kutokana na kuwepo kwa taarifa kwamba yeye (Badra) ameng’olewa, ili kumpisha meneja uhusiano wa zamani ndani ya shirika hilo, Daniel Mshana. Habari kutoka Tanesco zinadai kwamba Mshana, ambaye alihamishiwa ofisi za kanda ya Ilala miaka miwili iliyopita, jana alishinda katika ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, akisubiri kukabidhiwa ofisi yake mpya.Hata hivyo habari zinasema kuwa Mshana hakuweza kukabidhiwa ofisi hizo kutokana na sababu ambazo hazikuweza kufahamika mara moja.

  Mwananchi lilipowasiliana na Mshana kwa simu kutaka kujua kama amerejeshwa kwenye nafasi yake ya awali, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo na kumtaka mwandishi kuwasiliana na mkurugenzi mkuu wa Tanesco. “Kama ingekuwa katika personal level (suala langu mimi na wewe) tungeweza kuzungumza, lakini kama unataka kujua hilo basi muulizeni (mkurugenzi mkuu) MD, yeye si ndiye anayeteua watu bwana; muulizeni yeye maana mimi nisingependa kuonekana kwenye magazeti kesho (leo),” alisema Mshana. Naye Badra alisema hajapata taarifa rasmi za kuondolewa kwake katika nafasi hiyo na kwamba kutwa nzima ya jana alikuwa ofisini akiendelea na kazi. “Na mimi nimezisikia hizo taarifa kama wewe unavyosema, lakini sijapata taarifa yoyote kutoka kwa mabosi wangu kuhusu kuhamishwa au kuondolewa hapa. Niko ofisini na ninaendelea kama kawaida,” alisema Badra naye pia akilitaka gazeti hili kuwasiliana mkurugenzi mkuu.

  Kuhusu Mshana kufika makao makuu ya Tanesco kwa lengo la kukabidhiwa ofisi, Badra hakukubali wala kukanusha zaidi ya kusisitiza kutofahamu chochote kuhusu suala hilo. “Jamani, Mshana ni mfanyakazi wa Tanesco na yupo hapahapa Dar es Salaam, sasa kwani kama kafika hapa makao makuu ni dhambi,” alihoji. Taarifa za kung’olewa kwa Badra makao makuu na kurejeshwa kwa Mshana zilianza kusikika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita wakati meneja uhusiano huyo alipokuwa katika safari ya kikazi na waandishi wa habari katika mabwawa ya Kidatu na Kihansi mkoani Morogoro.

  Kutokana na taarifa hizo, Jumamosi usiku gazeti hili liliwasiliana na Mhando ambaye alisema: “Nani aliyemwondoa Badra… anayepaswa kumwondoa si mimi? Hayo ni majungu tu bwana hakuna kitu kama hicho.” “Badra ni mfanyakazi mchapakazi wetu na nijuavyo mimi hivi sasa yupo safarini na waandishi wa habari.

  Kwa hiyo hicho unachokisema hakipo. Kwa mara nyingine jana gazeti hili lilimtafuta Mhando kuhusu mkanganyiko uliosababishwa na Mshana kuonekana ofisini kwake kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutaka kukabidhiwa ofisi, lakini simu zake zote zilikuwa zikiita bila majibu. Hata hivyo, Mwananchi iliambiwa baadaye kuwa mkurugenzi huyo alikuwa na mkutano Ubungo na kwamba ulikuwa wa muda mrefu.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  inawezekana maana hata aliyekua mkurugenzi wa fedha wakati wa idrisa rashid alishajiondokea zake!rashid alikua na muelekeo mzuri wa kulinusuru shirika,alikuta hq wafanyakazi zaidi ya 300 pale ubungo walikua wanafanya nini?
   
 3. m

  mams JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Let us wait and time will tell everything!
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuinusuru nchi kwa matatizo ya umeme yasiyokwisha ni kuwachia kampuni binafsi ziwe na ushindani wa kibiashara na Tanesco kama ilivyofanywa kwa TTCL. Bila hivyo, Tanesco haitakaa sawa hata iweje. Pananuka uozo.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwani shirika kubwa kama hili halina policy ya uajiri hadi kunatokea blunders za aibu hivi?
  Then tunategemea kupata flow nzuri ya huduma katika hali ya migongano ya kimadaraka ya hivi?...
  Tukiletewa menejimenti za kigeni tunalalama, tukiwa wenyewe ndo balaa zaidi..huh!
   
 6. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Nadhani la Tanesco ni complicated zaidi kuliko ilivyokuwa kwa TTCL
   
 7. W

  Womtindo Member

  #7
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  vita yatoka wapi?ugomvi watoka wapi? si kwemye tamaa zenu wenyewe. magomvi na vita ni matokeo ya tamaa ya vyeo
   
 8. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Badra Masoud ni hawala wa Lowasa sasa kuna mgogoro wa maslahi
  Suala la udini halipo ila kuna suala la ufisadi na undugu wa kulindana
   
Loading...