TANESCO: Hakuna Mgao wa Umeme

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
"Hakuna tatizo la mgao wa umeme, ili kuwe na mgao wa umeme ina maana umeme unaozalishwa unakuwa haukidhi mahitaji.

Kwa sasa tunazalisha MW 1,600 na matumizi ya kiwango cha juu ya umeme kilichorekodiwa wiki iliyopita ni MW 1,273.42" Maharage Chande, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

"Katika kuleta umeme kwa wateja wetu kuna mambo matatu :- 1. Kuzalisha umeme 2. Usafirishaji umeme 3. Usambazaji . Matatizo mengi ya kukatika umeme yanatokana na eneo la usambazaji" Maharage Chande, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

"idadi ya wateja imeongezeka zaidi kutaka kuunganishiwa umeme, na katika robo ya kwanza tumewaunganisha wateja 150,000 kutoka kwenye lengo la kuwaunganisha wateja 75,000"

"Sisi ni shirika la huduma, kazi yetu ni kutoa huduma kwa wateja, tuna kazi kubwa ya kutoa huduma kwa wateja. Hatuhitaji ile uwe na rafiki unayemjua ndipo upate huduma kwa haraka, na kwenye tumeongeza ufanisi kwa kuwa na matumizi ya mifumo zaidi kuliko mikono" Maharage Chande

Hakuna heshima kubwa kama kupata nafasi ya kulitumikia Taifa lako. Thamani yake ni kubwa sana katika hilo " Ndg. Maharage Chande, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Akihojiwa katika kipindi cha #JotoKalilaAsubuhi kinachorushwa na EFM

Hapo bwana maharage ameongea kisiasa zaidi kuliko uhalisia uliopo.
 
Mgao ni kweli hakuna, kama mtaani umeme unakatika hiyo ni kawaida tu wakati wa bedui ulikuwa unakatika.

Tumwache mama afanye kazi!
 
Nimefuatilia hiyo interview lakini hoja yake kwamba eti Tanesco imezidiwa na waombaji umeme, ambao wameongezeka baada ya bei ya kuunganisha umeme kushuka, sijaikubali. Kama wateja wamewazidi kulingana na staff wao waliopo kwa nini wasi outsource kama wenzao wa kampuni za simu?

Tuna graduates kibao mtaani mpaka masters wako jobless, wanashindwaje kuwachukua kama vibarua wawasaidie ku process maombi huko mtaani na wawalipe kulingana na wanavyosajili maombi kwa ufasaha? Siku hizi kuna program unaweka kwenye smartphone kama vile ODK ambayo inaweza kupiga picha nyumba, mwombaji, kuchukua location/coordinate na hata mchoro ukishaandaliwa pia unapiga picha, na file lote linatumwa kwenye server huko Tanesco Wilayani au Mkoani.

So kijana akiwa na smartphone, pesa ya kukodi bodaboda, posho yake plus quick short training wanasajili maombi nchi nzima na kuyaingiza kwenye database yao kila mkoa au wilayani, na kumjulisha kila mwombaji kwa meseji kwamba maombi yake yamekamilika na lini afanye malipo na lini atafungiwa umeme.
 
"Hakuna tatizo la mgao wa umeme, ili kuwe na mgao wa umeme ina maana umeme unaozalishwa unakuwa haukidhi mahitaji.

Kwa sasa tunazalisha MW 1,600 na matumizi ya kiwango cha juu ya umeme kilichorekodiwa wiki iliyopita ni MW 1,273.42" Maharage Chande, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

"Katika kuleta umeme kwa wateja wetu kuna mambo matatu :- 1. Kuzalisha umeme 2. Usafirishaji umeme 3. Usambazaji . Matatizo mengi ya kukatika umeme yanatokana na eneo la usambazaji" Maharage Chande, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

"idadi ya wateja imeongezeka zaidi kutaka kuunganishiwa umeme, na katika robo ya kwanza tumewaunganisha wateja 150,000 kutoka kwenye lengo la kuwaunganisha wateja 75,000"

"Sisi ni shirika la huduma, kazi yetu ni kutoa huduma kwa wateja, tuna kazi kubwa ya kutoa huduma kwa wateja. Hatuhitaji ile uwe na rafiki unayemjua ndipo upate huduma kwa haraka, na kwenye tumeongeza ufanisi kwa kuwa na matumizi ya mifumo zaidi kuliko mikono" Maharage Chande

Hakuna heshima kubwa kama kupata nafasi ya kulitumikia Taifa lako. Thamani yake ni kubwa sana katika hilo " Ndg. Maharage Chande, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Akihojiwa katika kipindi cha #JotoKalilaAsubuhi kinachorushwa na EFM

Bado mna msimamo huu Tanesco?
 
Back
Top Bottom